Kuna watu wanamajanga hapa duniani dah! Poleni asee mimi majanga yangu ni pale nisikie mtu anakwangua sufuria na kijiko au anasugua na mchanga na pengine nipite sehemu pana ujenzi halafu mtu anaburuza spade kwenye sakafu! Itabidi nikimbie au nizibe maskio.
Tatizo hilo hata mimi ninalo nikiona kanga ina vidoa vidogo kama nimetoka kuamka huwa naumia sana, nikiona kichuguu cha mchwa huwa nasisimka, ama udongo mweusi wenye vitundu vingi, hii thread yako umenifanya nianze kujisikia vibaya.
Ni Sawa na wale jamaa wa kujambishwa
labda aligege...dwamay kuna tukio baya sana limewahi kukutokea linalohusiana na vitundu vidogo vidogo.
Au lilimtokea mtu mwingine huku wewe ukishuhidia.
Jaribu kikumbuka matukio
Na wewe umeonekana ume comment!!
Safi sana, ila kiukweli hata kama sio tatizo la kisaikolojia ikatokea binadamu mwenzako kwenye ngozi au sehemu flani ya mwili ana vijitundu vingi vidogo vidogo mwili unasisimka kiana sema tu wengine ndio hivyo tatizo linakuwa kubwa, mie mwenyewe hapa baada ya kuweka hiyo nondo ya trypophobia nikasema ngoja niongeze maarifa kwa kuingia wikipedia si nikaona na picha nami nikasisimka aiseeHilo ni tatizo la kisaikolojia liitwalo "trypophobia". Angalia kwenye tovuti ya "trypophobia.com' kwa habari zaidi.
Mimi kuna yale mabox yanahifadhia vitu kama redio, tv na vitu vingine vya electronic meupe yanawekwaga kwa ndani ili hivyo vifaa visipate mtikisiko. Hayo mabox kwangu ni majanga haswa ukiyagusisha pamoja kama kuyasugua au kukata na kisu huwa najickiaga vibaya mno..
Kumbe kuna kila aina ya matatizo hapa duniani, mie hiyo ya vitundu mpaka nimwone mnyma au binadamu mwenzangu lakini hata hivyo na uwezo wa kujitutumua kuangalia though kuna asilimia kidogo ya mwili kusisimka kiasi nikashindwa kuendelea ila hilo la vitundu vingine inaelekea ni kubwa aisee ila ni kujitutumua kuangalia mwisho wa siku utazoea hiyo haliTatizo hilo hata mimi ninalo nikiona kanga ina vidoa vidogo kama nimetoka kuamka huwa naumia sana, nikiona kichuguu cha mchwa huwa nasisimka, ama udongo mweusi wenye vitundu vingi, hii thread yako umenifanya nianze kujisikia vibaya.
Hata mie kuna jamaa wangu anatatizo kama hilo. Mfano aliwa kuona picha flani ilikuwa mtandaoni ikionesha ngozi yenye vitundu vingi vingi kwamba ni madhara ya nguo za mtumba kitu kama icho, jamaa alikuwa distrubed sana. So its not only you man