Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Haijawahi kuwa sera ya Marekani chini ya Rais wa Republican au Democrats kuchochea wanawake wapewe madaraka katika nchi za Africa, hili jambo watu wanalirudia rudia sana kuonyesha kwamba Wamarekani wameturubuni Waafrika kuwapa watu uongozi kwa kigezo cha jinsia yao huko wao wakiwa hawafanyi hivyo.
Mkutano mkubwa wa kijinsia duniani ulioleta maazimio na mabadiliko mengi ya kitaifa kwa wanawake ulifanyikia Beijing China, mikutano mengine yote mikubwa mitatu ya kimataifa iliyotangulia huo haikuwahi kufanyikia Marekani.
Suala la Diversity Equity and Inclusion (DEI) na usawa wa kijinsia bado ni mjadala mkali kwa Wamarekani wenyewe wakiwa wamegawanyika nusu kwa nusu, kama nyie mmekubali kwa wengi wenu kama taifa ni nyie wenyewe tusiwasingizie Wamarekani.
Je ni Wamarekani ndio waliotuambia inabidi tuwe na viti maalumu vya ubunge na udiwani katika katiba yetu?? Kama ni kweli ilikuaje tukalikubali hilo mapema haraka haraka sana halafu mengine wanayotuambia tukayakataa?? Kama ni wao walitushinikiza nini kinatochuzuia kuondoa hayo matakwa ya kijinsia baada ya kujua waliturubuni??
Tuwajibike kwa mambo yetu tuache kutumia Wamarekani kama kichaka cha kujifichia matatizo yetu.