Msomi anapokuwa mwanasiasa

Msomi anapokuwa mwanasiasa

Exaud J. Makyao

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2008
Posts
1,518
Reaction score
24
Kwa mtazamo wangu, wataalamu wetu wasomi wanapoingia katika siasa huwa wanasahau kanuni na miongozo ya Elimu yao.
Wengi hujikuta hawaelewiki tena kama na wataalamu wasomi.
Hata wakiandaa kwa mfano, bajeti za nchi, huziweka katika sura ya kisiasa.Tutafanikiwa kwa mwenendo huu kweli?
 
Nawakumbuka,
MASUMBUKO LAMWAI,
MKULLO,
SARUNGI,
LIPUMBA,
MWAKYUSA, NK.
 
..kuna uwezekano wamechoka na masuala ya kisomi-somi ndiyo maana wamehamia kwenye siasa.

..nimewahi kusikia kwamba Waisraeli walimpendekeza Albert Einstein kuwa Waziri Mkuu kwanza wa Israel.

..pia Raisi wa kwanza wa Israel ni mwanasayansi aliyebobea akiitwa Chaim Weizmann " the father of industrial fermentation."

..sidhani kama ushiriki wa wasomi wetu ktk siasa ni kitu kisicho na manufaa kwa taifa letu.
 
Kwa mtazamo wangu, wataalamu wetu wasomi wanapoingia katika siasa huwa wanasahau kanuni na miongozo ya Elimu yao.
Wengi hujikuta hawaelewiki tena kama na wataalamu wasomi.
Hata wakiandaa kwa mfano, bajeti za nchi, huziweka katika sura ya kisiasa.Tutafanikiwa kwa mwenendo huu kweli?
Sijaelewa swali lako au mjadala wako? Kwani Mwanasiasa ni nani na msomi ni nani? Kwa mawazo yangu wanasiasa ilibidi wawe wasomi wazuri ili tuepukane na matatizo tuliyonayo sasa hivi. Kama wanasiasa wetu wanafanya madudu wanayofanya sasa hivi basi usomi wao haujawakolea.

Wasomi si lazima wawe wanasiasa lakini wanasiasa lazima wajitahidi wawe wamesoma, au wajisomeshe!
 
Mkuu kitu gani kinawapeleka kwenye siasa?

elimu yao iko palepale na wanajua kua wanakosea au wanapatia, ubongo haubadiliki! same person, same scholar, same politician,same brain!
 
Kwa mtazamo wangu, wataalamu wetu wasomi wanapoingia katika siasa huwa wanasahau kanuni na miongozo ya Elimu yao.
Wengi hujikuta hawaelewiki tena kama na wataalamu wasomi.
Hata wakiandaa kwa mfano, bajeti za nchi, huziweka katika sura ya kisiasa.Tutafanikiwa kwa mwenendo huu kweli?

Enzi zetu ukimaliza kidato cha sita kwenye msururu wa kujaza unachotaka siasa haipo. Hivyo unapita kwenye sheria, utabibu,ualimu kuelekea kwenye siasa. Wakiweka chaguo la siasa labda wengi watachagua mara moja badala ya kupita njia ndefu..
 
Nini huwamaliza kitaaluma?

Unapoingia kwenye siasa huwezi kuwa na mawazo independent kwa maana kuna miongozo, sera, ilani na mfumo ambao uko established.Msomi mwenye kustahili kuitwa msomi anatakiwa awe na mawazo yake na kuwa tayari kwa paradigm shift kutegemeana na anaamini nini ( conviction).Ili u survive as a politiciam inabidi uwe tayari kutelekeza fikra huru na kuungana na wenzio - CO-OPTATION!
IF U CANT BEAT THEM, JOIN THEM.
 
Kwa mtazamo wangu, wataalamu wetu wasomi wanapoingia katika siasa huwa wanasahau kanuni na miongozo ya Elimu yao.
Wengi hujikuta hawaelewiki tena kama na wataalamu wasomi.
Hata wakiandaa kwa mfano, bajeti za nchi, huziweka katika sura ya kisiasa.Tutafanikiwa kwa mwenendo huu kweli?

Tatizo kubwa wanalokutana nalo hawa wasomi mara tu wakiingia katika siasa ama uwanja wa siasa ni mlolongo wa watu wasiojua nini cha kufanya ili kuendeleza nchi kimaadili ndiyo wengi katika ngazi nyingi na kila kona. Hivyo kila wakitoa hoja ama mawazo hupingwa, kudharauliwa na kuwekewa vikwazo katika utekelezaji wa yale mazuri wanayotaka kuya badilisha hapo walipo. Mwisho wake nao wanakuwa wamechanganyikiwa na kutojua nini cha kufanya na kuishia kujiunga na upuuzi huo ili nao washibishe matumbo yao na watoto wao.

Ndugu Makyao sijui wewe ni mtaalamu katika fani gani, lakini ninakuhakikishia kabisa ukiingia katika ulingo wa siasa hayo niliyaandika hapo juu ni lazima yatakukuta taka usitake. Na kama ni mbishi sana basi utapigwa kipapai watu watakusahu. Ninakumbuka kuna kamati iliundwa kushughulikia suala nyeti la taifa. Kamati hiyo ilikuwa na Sarungi, Mzindakaya, Ayubu kimbau, Nchimbi na John Komba. Ebu fikiria hapo Sarungi atasema nini ili aweze kueleweka?
 
Kwa mtazamo wangu, wataalamu wetu wasomi wanapoingia katika siasa huwa wanasahau kanuni na miongozo ya Elimu yao.
Wengi hujikuta hawaelewiki tena kama na wataalamu wasomi.
Hata wakiandaa kwa mfano, bajeti za nchi, huziweka katika sura ya kisiasa.Tutafanikiwa kwa mwenendo huu kweli?

Principals za taaluma na za siasa ni tofauti ndugu. You can't move to a different league, play the same way and still expect to win.
 
..kuna uwezekano wamechoka na masuala ya kisomi-somi ndiyo maana wamehamia kwenye siasa.

..nimewahi kusikia kwamba Waisraeli walimpendekeza Albert Einstein kuwa Waziri Mkuu kwanza wa Israel.

..pia Raisi wa kwanza wa Israel ni mwanasayansi aliyebobea akiitwa Chaim Weizmann " the father of industrial fermentation."

..sidhani kama ushiriki wa wasomi wetu ktk siasa ni kitu kisicho na manufaa kwa taifa letu.

Watu bana...hivi unajua kwa mfano Newt Gingrich ana PhD. na alikuwaga professor pale University of Georgia....au Tom DeLay (former House Majority Leader) kwa mfano..jamaa naye ana PhD. Na ukiangalia CV za masenenta na ma congessman na ma congresswoman wa Marekani utagundua wengi wao wameenda shule kikwelikweli.....

Kwa mtazamo wangu sioni ubaya wowote kwa mwanasiasa kuwa msomi na kinyume chake
 
Si ndiyo maana wana chagua viongozi ambao hawaja enda shule halafu waki chemsha wao ndiyo wakwanza kupiga kelele.
 
''''''''''''''''''''''''''''? Kwa mawazo yangu wanasiasa ilibidi wawe wasomi wazuri ili tuepukane na matatizo tuliyonayo sasa hivi. ;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;

Wasomi si lazima wawe wanasiasa lakini wanasiasa lazima wajitahidi wawe wamesoma, au wajisomeshe![/QUOTE]

INTE:""".,
Ipo taaluma ya siasa.
Wanasiasa watoke huko.
Wapige siasa zao.

Inakuwa jambo la kushangaza INJINIA, AU MWANASHERIA kujiingiza kwenye siasa kisha kuanza kufanya maamuzi yaliyo kinyume na taaluma yake.

Mfano:
-- Kuanzisha kiwanda au kutoanzishwa kunahitaji itikadi ya kisiasa.
--- Mtu anamuua mwenzake uamuzi unatolewa kisiasa.

Wanaoingiza hizo siasa katika hizi juhudi za maendeleo, ukichunguza unawakuta wataalamu wetu wa Uhandisi na sheria wamo ndani.
 
Pointless argument, mnataka wajinga wawe wanasiasa?....mwanasiasa siyo profession, mtu yeyote ruksa kuwa mwanasiasa as long as wanatetea maslahi ya wananchi..wengine wameingia huko kutetea haki za wananchi wao, kuna ubaya gani wakirudi kwa watu wao na kujaribu kuwasaidia....(wether they are doing a good job or not, thats another argument, but kusema wasomi wasiwe wanasiasa, is nonsense...)
 
Back
Top Bottom