Msomi na Mjinga katika Interview!

Msomi na Mjinga katika Interview!

Red Scorpion

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2012
Posts
5,736
Reaction score
4,252
Msomi na Mjinga walienda katika usaili, walipofika kabla hawajaingia wakakubaliana aanze Msomi kisha akitoka ampe majibu Mjinga ili wote wapate kazi.

Basi Msomi akaingia na maswali yakawa hivi:-

Msaili:- Tanzania ilipata Uhuru mwaka gani?

Msomi:- ilitakiwa iwe mwaka 1960 ila ikasogezwa mpaka 1961 kutokana na sababu mbalimbali..

Msaili:- Nani hasa alihusika na upatikanaji wa Uhuru huo?

Msomi:- Kuna watu wengi walihusika ila Mwl. J.K. Nyerere ndiye alikuja kumalizia.

Msaili:- Inasemekana ktk sayari ya Mars kunaviumbe wanaishi, je ni kweli?

Msomi:- Watu wengi wanasema hivyo lakini haijathibitishwa na wanasayansi.

Baada ya Msomi kutoka basi Mjinga akapewa majibu yote..

Kuingia ktk usaili maswali yakawa hivi:-

Msaili:- Tuambie ulizaliwa mwaka gani?

Mjinga:- Ilitakiwa iwe mwaka 1960 ila ikasogezwa mbele mpaka mwaka 1961 kutokana na sababu mbali mbali.

Msaili:- Mungu Wangu, BABA yako anaitwa nani?

Mjinga:- Kuna watu wengi walihusika ila Mwl. J. K. Nyerere ndiye alikuja kumalizia .

Msaili:- Hivi wewe ni chizi?

Mjinga:- watu wengi husema hivyo lakini haijathibitishwa na wanasayansi...
Haji
 
Back
Top Bottom