Msomi ni nani

kama sdijakuelewa vile,,,kwani kamusi inasemaje.....na mnukuu mchangia hapo juuu alitoa viashiria vya neno msomi,,,,,
msomi , pl wasomi { English: intellectual }
noun

msomi , pl wasomi { English: learned person , pl learned people }
noun

msomi , pl wasomi { English: lecturer , pl lecturers } [derived: soma V]
noun

msomi , pl wasomi { English: reader } [derived: soma V]
noun ,

msomi , pl wasomi { English: scholar , pl scholars } [derived: Swahili -soma]
noun

5 distinct results returned (chanzo:THE KAMUSI PROJECT)
 

Kwahiyo kama utaenda darasani ukawa hukupata taaluma wewe sio msomi.
 
Ulichoandika hapa umeonyesha udhaifu wa kamusi katika kutoa maana. Huwezi kumjua msomi kama hujamnasibisha na fani fulani, aidha fundi, mwalimu, mwanashera au mfano wake. Kwai fundi gereji hasomi ? Lazima afundishwe ndiyo kazi aijue huenda akafundishwa darasani au sehemu ya kazi husika (site).

Au unafikiri kusoma mpaka ukae darasani kwenye madawati na mfungiwe Projector,au uvae joho na mfano wake ? Kuwaza kwa mtindo huu ni kuwaza kitoto mno. Kwa sababu historia inatunukulia wasomi na wanao rejewa katika fani mbali mbali hawakuwa na shahada, wala stashahada, wala shahada ya uzamili wala uzamivu. Mfano wa harakaharaka ni Shabaani Robert nakumbuka kama sijakosea aliishia darasa la nne (Mtanisahihisha hapa), lakini tunaambiwa yeye ndiyo baba wa Fasihi ya Kiswahili, na hawa wako wengi sana mpaka kwenye Sayansi,Falsafa na fani nyingine.
 
Enyi wasomi mlioko juu kama nyota, nani anayeingia mikataba ya kilaghai inayohatarisha rasilimali za nchi yetu kama siyo nyie?
 
SASA BASI KAMA KUSOMA MPAKA LA SABA SIO MSOMI,,,BASI MSOMI NIYULE ALIYE NA VETI VYA TAALUMA NA WALA SIO YULE AMBAYE KAFIKA CHUO NA AKASOMA LAKINI HAKUPATA CHETI CHA TAALUMA.
Kuwa na vyeti siyo usomi, usomi ni kile ulichobaki nacho. Wapo wasomi na wanazuoni kibao hawana vyeti. Hili nimelifafanua huko nyuma.
 
Jamani mimi na tatizo na maana ya mtu msomi, mtu kuitwa msomi anatakiwa awe na kiwango gani cha elimu? maana kijijini kwetu ukijua kusoma na kuandika tu wewe tayari msomi.

=====
Ukiachana na mimi niitwae Emmanuel Kasomi msomi ni mkubwa zaidi yangu kwa vile mi mdogo wananiita kasomi
 
KAKA MBONA HAPA UMECHANGACHA MSOMI NA MTAALUMA? TONGOA KWA MAKINI,,,DADAFURA KATI YA MSOMI NA MTAALUMA.
Mtaakuma anakuwa vipi si msomi ? Msomi ni jina lenye kuainisha sifa ya umahiri katika jambo fulani ni sawa na mtaalamu wa jambo fulani, mtu huwezi kuwa mtaalamu bila kusoma yaani kufundishwa na kufanyia kazi ulichokisoma. Kujua kusoma na kuandika huitwi msomi.
 
Neno msomi lina maana zaidi ya mmoja,
1.msomi kama mtu aliyesoma shule, yaani aliyesoma Hadi hatua fulani ya masomo ya elimu rasmi.
2.Msomi ni mtu yule aliyesoma mpaka hatua za juu za elimu rasmi hasa kuanzia hatua ya shahada, uzamiri mpaka udaktari wa falsafa na uprofesa .
3 .Msomi kama mtu aliyesoma elimu rasmi na ana ujuzi wa aina mbalimbali mfano uchumi,siasa, utamaduni, michezo, jamii, jiografia , sayansi na hata biashara,
NB:tofauti ya msomi wa maana ya kwanza na ya tatu ni kwamba Msomi wa tatu anakuwa ni (multi-cultural, inter displinary)anakuwa mtu aliyejenga shule halafu ana ujuzi wa mambo mengi Sana. Msomi wa maana ya kwanza anakuwa tu na elimu fulani lakini inajikita hasa kwenye kukariri, ila vyeti Ndio vitaonesha usomi wake
 
Nimekupata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…