Mtoto yuko sawa kwa hapo ila mtihani nao una makosa komaeni na walimu. . . . .Mfano hapo kwenye "variaty". . . .na kwenye "ADS". . . . .
asante mkuu,ila handwriting yake naona haiko sawa.anahitaji mkazo zaidi,siridhishwi nayo.
hahaha nimepaona hapo mkuu,si unajua tena hizi shule za ada nafuu,umakini kwa walimu unakuwa madogo.ukimbana mwalimu wa hilo somo,atasingizia swala la maslahi duni.
Ha ha haaaa naelewa kaka. . . . Ingawa ukionesha kuwa uligundua watajitahidi kuwa makini ila iweke kama utani tu kwa kikao. . . . .Section D hajafanya vizuri ukimshughulisha zaid kwenye kujieleza na kuelezea atakuwa better kaka
section D kuanzia swali la 16-19 kaboronga vibaya sana,labda kwa kuwa majibu yalikuwa yanahitaji uundaji wa neno zaidi ya moja.
kwa mfano hilo swali la why do we boil water;kwa mtoto mwenye uelewa mzuri na uwezo wa kuandika,jibu lake laweza kuwa na mistari 5 au zaidi.hata hivyo nimefurahia concerned yako,bila shaka wewe ni mzazi/mlezi mwenzangu.
Lakini pia kumbuka ndio mwaka wake wa pili tu elimu ya msingi, usitegemee atembee kabla hajatambaa - atafika tu unapotaka.asante mkuu,ila handwriting yake naona haiko sawa.anahitaji mkazo zaidi,siridhishwi nayo.
ni kweli mamanzara,nimekuwa napigizana nae kelele sana kuhusu hopefully ata-improve kadili siku zinavyo endelea.asante kwa mchango wako.Lakini pia kumbuka ndio mwaka wake wa pili tu elimu ya msingi, usitegemee atembee kabla hajatambaa - atafika tu unapotaka.
ni binti yangu mwenye umri wa miaka 7,anasoma darasa la pili ktk shule moja ya watoto akina sie "kajamba nani" (watu wa kipato cha chini).
pichani ni mtihani wake wa somo la sayansi alio ufanya mwezi ulio pita,nimeona si vibaya kuuleta hapa ili nibadilishane mawazo na wazazi,walezi au wadau wa elimu kuhusu maendeleo yake.karibuni.
MK254 maina pita hapa useme kitu(ushauri),nimeona mara kadhaa unakosoa elimu yetu wanayo fundishwa watoto wa ktz kwamba ni duni na ya kwenyu ni bora.
View attachment 250734
View attachment 250735
Kwanza kabisa hongera kwa kuwa mzazi anayefuatilia mwanae kwa makini, ila nina issue na hayo majibu yake kwenye baadhi ya maswali, inaonyesha huwa binafsi hauhusiki kumuelimisha kwa mambo ya msingi. Usitegemee mwalimu afanye yote.
Hata hivyo naona anajaribu, halafu vipi mbona tena English, si kwani nilidhani mmeshamia Kiswahili mwanzo mwisho.
Muda usio mrefu nitayaleta hapa baadhi ya maswali wanayopata wanangu hapa Kenya, noma aisei. Kwanza nina mwanangu kwenye darasa la nane na binafsi nimeshindwa kumfunza hadi nimemlipia mwalimu awe anamsaidia kila akirudi nyumbani.
mkuu
huwa najitahidi kumueleimisha kadili nipatapo nafasi kwasababu mda wingi nakuwa ktk mizunguko ya kutafuta "mkwanja" wa kumlipia ada,chakula na mahitaji mengine ya muhimu ya kifamilia.
una issue na majibu yake kivipi mkuu?,kufafanua ili niapate kufahamu tatizo lilipo ili nianze kumkazania.
hapo kwenye kiswahili ni hivi sio shule zote zinafundisha masomo yote kwa kiswahili.ni zile za serikali tu.private schools nyingi hufundisha kwa kingereza isipokuwa kwa somo la kiswahili.
Kwa mfano tu hapo kwenye swali la "kwanini tunachemsha maji", hayo ni mambo ya kumfundisha nyumbani bila kusubiri mwalimu. Kuna mambo ya msingi ambayo mtoto anafaa kuyajua kinyumbani bila shule. Kwa mfano tu kwenye somo la mazingira, mimi huwa kila Jumamosi ni siku ya kukusanya makaratasi na uchafu wote kwenye compound. Watoto wangu wanahusika kwenye hili zoezi na wanajua sababu zake hata likaja kama swali shuleni, hawana haja ya mwalimu kuwafundisha.