Watanzania huwa mmebarikiwa na jambo moja..mlikuwa na Rais ambaye alikuwa mwana-filosofia wa Elimu. Umeshawahi kukisoma kijitabu cha Mwalimu Nyerere kinachoitwa Education for Self-reliance? Haya mambo tunayoyazungumzia ndio alikuwa akiongea kuhusu.
Umeuliza kuhusu vaccination; kwanini mtoto mdogo afundishwe kuhusu vaccination? Itamsaidia na nini?
Mtoto hawezi spell "Aids" kweli sio kumtesa yule mtoto kumfundisha mambo ya vaccination? Mtoto kweli anaweza elewa maana ya Acquired Immune-Deficiency Syndrome?
Na ikiwa ni lazima basi ajifunze kuhusu jambo hili, na afundishwe kwa lugha anayoelewa..aambiwe kuhusu "Chanjo." Hilo ataelewa kwa urahisi zaidi. Na Ukimwi - Ukosefu Wa Kinga Mwilini.
Ningekuwa nchi ya TZ, mtoto wangu hangekanyaga shule ya English medium hata siku moja. Hamjui baraka mlio nayo nyie.
Huu ni wakati wa mtoto kusoma hadithi, shairi, kujifunza michezo ya kuigiza ili kupanua ubongo wake. Kujifunza hisabati kwa undani na kufanya "Word problems" nyingi. Kwa kusema ukweli, sioni haja ya kumfundisha mtoto lugha ya Kifaransa.
Kumfundisha mtoto kwa lugha asiyoelewa, ni kumfanya mtoto awe na Intellectual dependency. Inauwa creativity ya mtoto kabisa. Mwalimu anapouliza "when do we have a bath" Mtoto Kasema Morning, Afternoon, and Evening. Kweli mtoto kaelewa swali? Na mwalimu anataka jibu gani? Watu huoga wakati tofauti tofauti. Lakini, mwalimu anataka mtoto ampe jibu la kukariri. lile amablo waliimba na kukariri darasani. Hatakati mtoto ajifikirilie.
Ushawahi kujiuliza ni kwanini unampata Injinia mzima na ile elimu yake ni ya nadharia tu? Ushawahi jua kuwa 50% wa software engineers huko Apple hawana degree? Kwanini sisi waafrika na hizi degree zetu zote hatuwezi hata kuunda baiskeli bila msaada wa mchina ama mzungu?
Hebu tazama video hii...Hii ndio Elimu ningependa Wakenya tuwe nayo - sio matajiri pekee.
https://youtu.be/87qkZraVuew