Msomi wa Kesho na Safari yake changa ya kusaka Elimu

Mtoto mwenye akili utasikia baba anamtambulisha kama Binti/kijana wangu, akiwa mjinga utasikia mume anamwambia mkewe muonye mtoto wako huyo...

ndio desturi zetu hizo watz/waafrika.mara nyingi mtoto jeuri lawama zote huenda kwa mama yake.utasikia baba anamwambia mama,"safari hii mtoto wako asipo jirekebisha simlipii ada ya chuo nk".anasahau hata yeye ana mchango/wajibu wa kumfanya kuwa mtoto mwenye maadili bora ktk jamii.
 
ni binti yangu mwenye umri wa miaka 7,anasoma darasa la pili ktk shule moja ya watoto akina sie "kajamba nani" (watu wa kipato cha chini).

pichani ni mtihani wake wa somo la sayansi alio ufanya mwezi ulio pita,nimeona si vibaya kuuleta hapa ili nibadilishane mawazo na wazazi,walezi au wadau wa elimu kuhusu maendeleo yake.karibuni.

MK254
maina pita hapa useme kitu(ushauri),nimeona mara kadhaa unakosoa elimu yetu wanayo fundishwa watoto wa ktz kwamba ni duni na ya kwenyu ni bora.

Mkuu, nashukuru kwa kuweka hapa karatasi ya mtoto wako, lakini kuna mambo amabyo sielewi na huu mtihani.

Huyo Mwalimu anatoka nchi gani? Natumai si mwalimu kutoka Kenya.

Kwanini mwalimu anatumia maneno magumu ya kiingereza kwa kuwafundisha watto wadogo wa darasa la pili?

My goodness; huyu ni mwalimu kweli?
Mtoto mdogo anaelewa maana ya vaccination? Disinfectant? Hata anaweza tamka haya maneno kweli?

Sio kwa ubaya, lakini hii elimu na ya kumfanya mtoto akariri tu; cramming. Hili ndilo tatitzo la English medium. Ndio sababu unaona huyo mtoto kaanguka section D karibu yote. Unamtesa mtoto, kamtoe katika hilo shule.

Mwenyewe siwezi jibu swali number 17 na 18...

Mie hukasirishwa sana ninapoona elimu ya mtoto ikifanyiwa mzaha ili tu kuwafurahisha wazazi na kuwaonesha kuwa mtoto anaweza kusema kwa kiingereza.
 
kadoda11 Kama nilivyoahidi, hapa naleta mtihani wa mtoto wangu akiwa darasa la pili. Nakiri kwamba maswali wanayoulizwa watoto wetu hapa Kenya siwezi linganisha na yale niliyopitia enzi zangu.

HII HAPA SOMO LA COMPUTER
computer.jpg

HII HAPA SOMO LA LUGHA YA KIFARANSA
french.jpg
 
Last edited by a moderator:
Mkuu, nashukuru kwa kuweka hapa karatasi ya mtoto wako, lakini kuna mambo amabyo sielewi na huu mtihani.

Huyo Mwalimu anatoka nchi gani? Natumai si mwalimu kutoka Kenya.

Kwanini mwalimu anatumia maneno magumu ya kiingereza kwa kuwafundisha watto wadogo wa darasa la pili?

My goodness; huyu ni mwalimu kweli?
Mtoto mdogo anaelewa maana ya vaccination? Disinfectant? Hata anaweza tamka haya maneno kweli?

Sio kwa ubaya, lakini hii elimu na ya kumfanya mtoto akariri tu; cramming. Hili ndilo tatitzo la English medium. Ndio sababu unaona huyo mtoto kaanguka section D karibu yote. Unamtesa mtoto, kamtoe katika hilo shule.

Mwenyewe siwezi jibu swali number 17 na 18...

Mie hukasirishwa sana ninapoona elimu ya mtoto ikifanyiwa mzaha ili tu kuwafurahisha wazazi na kuwaonesha kuwa mtoto anaweza kusema kwa kiingereza.

mkuu
shule ina mchanganyiko wa walimu wa tz na nchi jirani ya kenya na rwanda.binafsi sina tatizo na hayo maneno (vaccination ,disinfectant) kwa mtoto wa darasa la pili,kwasababu mtindo wa ufundishaji/uwasilishaji unatofautana kati ya shule na shule japo mtaala waweza kufanana.

kwa mfano ktk hilo swali la 15 linaohusiana na AIDS,badala ya kutumia neno "vaccination" ungependelea watumie neno gani la mbadala?!

ila kuna ukweli kidogo hapo kwenye red,kwamba msisitizo mkubwa wa shule za english medium ni kumfanya mtoto aongee kingereza kuliko kumpatia maarifa/uelewa.wanalifanya hili kwa makusudi ili kuwafurahisha wazazi.
asante kwa comment yako mdau.
 
MK254
mitihani ya mtoto nimeiona though picha hazipo clear sana.
mtoto anaonekana yupo smart,naona hapo kapiga 93% kwenye somo la computer na 85% kwenye somo la french,congrats for her and you as a parent.

nimefurahi kwamba anacho fundishwa/soma mwanao ndicho wanacho fundishwa/soma watoto wa ktz ktk baadhi ya shule.shule anayo soma binti yangu hufundisha somo la ICT na french.ambapo walimu toka rwanda ndio hufundisha lugha hiyo ya kifaransa.ktk somo la ICT hufundishwa vitu vingi tu vinavyo husiana na teknolojia ya mawasiliano kama computer,mobile phones tv,radio nk.ipo siku nitaweka hapa mitihani yake ya french na ICT.

naomba hizo picha zako uzi-scan ili iwe rahisi kuzitazama.
 
Last edited by a moderator:
mkuu
shule ina mchanganyiko wa walimu wa tz na nchi jirani ya kenya na rwanda.binafsi sina tatizo na hayo maneno (vaccination ,disinfectant) kwa mtoto wa darasa la pili,kwasababu mtindo wa ufundishaji/uwasilishaji unatofautana kati ya shule na shule japo mtaala waweza kufanana.

kwa mfano ktk hilo swali la 15 linaohusiana na AIDS,badala ya kutumia neno "vaccination" ungependelea watumie neno gani la mbadala?!

ila kuna ukweli kidogo hapo kwenye red,kwamba msisitizo mkubwa wa shule za english medium ni kumfanya mtoto aongee kingereza kuliko kumpatia maarifa/uelewa.wanalifanya hili kwa makusudi ili kuwafurahisha wazazi.
asante kwa comment yako mdau.

Watanzania huwa mmebarikiwa na jambo moja..mlikuwa na Rais ambaye alikuwa mwana-filosofia wa Elimu. Umeshawahi kukisoma kijitabu cha Mwalimu Nyerere kinachoitwa Education for Self-reliance? Haya mambo tunayoyazungumzia ndio alikuwa akiongea kuhusu.

Umeuliza kuhusu vaccination; kwanini mtoto mdogo afundishwe kuhusu vaccination? Itamsaidia na nini?

Mtoto hawezi spell "Aids" kweli sio kumtesa yule mtoto kumfundisha mambo ya vaccination? Mtoto kweli anaweza elewa maana ya Acquired Immune-Deficiency Syndrome?

Na ikiwa ni lazima basi ajifunze kuhusu jambo hili, na afundishwe kwa lugha anayoelewa..aambiwe kuhusu "Chanjo." Hilo ataelewa kwa urahisi zaidi. Na Ukimwi - Ukosefu Wa Kinga Mwilini.

Ningekuwa nchi ya TZ, mtoto wangu hangekanyaga shule ya English medium hata siku moja. Hamjui baraka mlio nayo nyie.

Huu ni wakati wa mtoto kusoma hadithi, shairi, kujifunza michezo ya kuigiza ili kupanua ubongo wake. Kujifunza hisabati kwa undani na kufanya "Word problems" nyingi. Kwa kusema ukweli, sioni haja ya kumfundisha mtoto lugha ya Kifaransa.

Kumfundisha mtoto kwa lugha asiyoelewa, ni kumfanya mtoto awe na Intellectual dependency. Inauwa creativity ya mtoto kabisa. Mwalimu anapouliza "when do we have a bath" Mtoto Kasema Morning, Afternoon, and Evening. Kweli mtoto kaelewa swali? Na mwalimu anataka jibu gani? Watu huoga wakati tofauti tofauti. Lakini, mwalimu anataka mtoto ampe jibu la kukariri. lile ambalo waliimba na kukariri darasani. Hatakati mtoto ajifikirilie.

Ushawahi kujiuliza ni kwanini unampata Injinia mzima na ile elimu yake ni ya nadharia tu? Ushawahi jua kuwa 50% wa software engineers huko Apple hawana degree? Kwanini sisi waafrika na hizi degree zetu zote hatuwezi hata kuunda baiskeli bila msaada wa mchina ama mzungu?

Hebu tazama video hii...Hii ndio Elimu ningependa Wakenya tuwe nayo - sio matajiri pekee.

https://www.youtube.com/watch?v=87qkZraVuew&feature=youtu.be
 
Kumfundisha mtoto kwa lugha asiyoelewa, ni kumfanya mtoto awe na Intellectual dependency. Inauwa creativity ya mtoto kabisa. Mwalimu anapouliza "when do we have a bath" Mtoto Kasema Morning, Afternoon, and Evening. Kweli mtoto kaelewa swali? Na mwalimu anataka jibu gani? Watu huoga wakati tofauti tofauti. Lakini, mwalimu anataka mtoto ampe jibu la kukariri. lile amablo waliimba na kukariri darasani. Hatakati mtoto ajifikirilie.

Ushawahi kujiuliza ni kwanini unampata Injinia mzima na ile elimu yake ni ya nadharia tu? Ushawahi jua kuwa 50% wa software engineers huko Apple hawana degree? Kwanini sisi waafrika na hizi degree zetu zote hatuwezi hata kuunda baiskeli bila msaada wa mchina ama mzungu?

Hebu tazama video hii...Hii ndio Elimu ningependa Wakenya tuwe nayo - sio matajiri pekee.

https://youtu.be/87qkZraVuew

mkuu post yako ipo too general,ila nimeipenda kwani itazidi kupanua mjadala kuhusu elimu ya watoto wetu.niwie radhi sina nafasi kwa sasa, nitarudi baadae kidogo kuendelea na mjadala.nimebaini wewe ni mdau wa elimu hasa.asante sana.

CC MK254 OLESAIDIMU et al
 
Watanzania huwa mmebarikiwa na jambo moja..mlikuwa na Rais ambaye alikuwa mwana-filosofia wa Elimu. Umeshawahi kukisoma kijitabu cha Mwalimu Nyerere kinachoitwa Education for Self-reliance? Haya mambo tunayoyazungumzia ndio alikuwa akiongea kuhusu.

Umeuliza kuhusu vaccination; kwanini mtoto mdogo afundishwe kuhusu vaccination? Itamsaidia na nini?

Mtoto hawezi spell "Aids" kweli sio kumtesa yule mtoto kumfundisha mambo ya vaccination? Mtoto kweli anaweza elewa maana ya Acquired Immune-Deficiency Syndrome?

Na ikiwa ni lazima basi ajifunze kuhusu jambo hili, na afundishwe kwa lugha anayoelewa..aambiwe kuhusu "Chanjo." Hilo ataelewa kwa urahisi zaidi. Na Ukimwi - Ukosefu Wa Kinga Mwilini.

Ningekuwa nchi ya TZ, mtoto wangu hangekanyaga shule ya English medium hata siku moja. Hamjui baraka mlio nayo nyie.

Huu ni wakati wa mtoto kusoma hadithi, shairi, kujifunza michezo ya kuigiza ili kupanua ubongo wake. Kujifunza hisabati kwa undani na kufanya "Word problems" nyingi. Kwa kusema ukweli, sioni haja ya kumfundisha mtoto lugha ya Kifaransa.

Kumfundisha mtoto kwa lugha asiyoelewa, ni kumfanya mtoto awe na Intellectual dependency. Inauwa creativity ya mtoto kabisa. Mwalimu anapouliza "when do we have a bath" Mtoto Kasema Morning, Afternoon, and Evening. Kweli mtoto kaelewa swali? Na mwalimu anataka jibu gani? Watu huoga wakati tofauti tofauti. Lakini, mwalimu anataka mtoto ampe jibu la kukariri. lile ambalo waliimba na kukariri darasani. Hatakati mtoto ajifikirilie.

Ushawahi kujiuliza ni kwanini unampata Injinia mzima na ile elimu yake ni ya nadharia tu? Ushawahi jua kuwa 50% wa software engineers huko Apple hawana degree? Kwanini sisi waafrika na hizi degree zetu zote hatuwezi hata kuunda baiskeli bila msaada wa mchina ama mzungu?

Hebu tazama video hii...Hii ndio Elimu ningependa Wakenya tuwe nayo - sio matajiri pekee.

https://www.youtube.com/watch?v=87qkZraVuew&feature=youtu.be

Naomba kutokubaliana na wewe, fahamu watoto wa kisasa wana akili sana ukilinganisha na nyakati zetu, wana uelewa zaidi. Sioni kwa nini ubishe dhidi ya maneno yanayotumika kumfundisha mtoto. Huo mjadala wa matumizi ya lugha tumepitia kwa kina na hadi sasa nimekomaa na msimamo wangu kwamba ni jambo nzuri kumfanya mtoto awe mjanja wa lugha.
Watoto wangu wanaongea lugha yangu ya asili, Kikikuyu, lugha ya asili ya mke wangu Kiluhya, lugha yetu ya taifa Kiswahili, lugha yetu ya biashara Kingereza, lugha ya mtaa shen'g, lugha ya Kifaransa. Halafu ukiona maswali kwenye mitihani yao, unakubali kweli ni tofauti na wakati wetu, wapo sawa sana. Fhamu pia siku hizi kuna ubunifu mwingi sana ukilinganisha na zamani.
 
Last edited by a moderator:
Shule zetu zile sanyansi si inafundishwa kwa lugha ya kiswahili au sikuhizi mambo kuvunja yai no duski downi tena
 
Kama hutajali unaweza nipa jina la shule nina mtoto anatakiwa aanze grade 1. Ningependa ajifunze french, pia music instruments.
 
Watanzania huwa mmebarikiwa na jambo moja..mlikuwa na Rais ambaye alikuwa mwana-filosofia wa Elimu. Umeshawahi kukisoma kijitabu cha Mwalimu Nyerere kinachoitwa Education for Self-reliance? Haya mambo tunayoyazungumzia ndio alikuwa akiongea kuhusu.
hicho kijitabu niliwahi kukisoma ila ni siku nyingi kidogo.nyakati hizo,mwl. alijikita zaidi ktk dhana ya kuondoa UJINGA,MARADHI NA UMASIKINI.

katika kuondoa ujinga,mwl alisisitizia zaidi ktk kuwafanya watz wajue kusoma na kuandika,kilikuwa ni kipaombele sahihi ukichukulia kwamba ndio kwanza tanganyika ilikuwa inatoka ktk vuguvugu la kudai uhuru na watanganyike wengi wa wakati huo walikuwa hawana elimu ya msingi ya kujua kusoma na kuandika.mengine ni historia ila sidhani kama hicho kipaombele cha kuondoa UJINGA kina nafasi kubwa nyakati za sasa.

Umeuliza kuhusu vaccination; kwanini mtoto mdogo afundishwe kuhusu vaccination? Itamsaidia na nini?

Mtoto hawezi spell "Aids" kweli sio kumtesa yule mtoto kumfundisha mambo ya vaccination? Mtoto kweli anaweza elewa maana ya ?

Na ikiwa ni lazima basi ajifunze kuhusu jambo hili, na afundishwe kwa lugha anayoelewa..aambiwe kuhusu "Chanjo." Hilo ataelewa kwa urahisi zaidi. Na Ukimwi - Ukosefu Wa Kinga Mwilini
.
nadhani kulikuwa na sababu ya msingi kwa wizara ya elimu ku-introduce topic inayo husiana na maradhi ya UKIMWI ktk masomo ya shule za msingi hususani kwa darasa la pili au zaidi.moja ya lengo ni kuwafanya watoto wawe na ile basic awareness jinsi ugonjwa huo unavyo ambukizwa na tahadhari zake.maumbikizi ya ukimwi hayachagui muhusika anazungumza lugha gani,hivyo basi sioni tatizo kwa mtoto kufundushwa kwa kingereza ukizingatia kwamba ufundishaji haujajikita ndani kwenye hiyo "Acquired Immune-Deficiency Syndrome".ni introduction part tu mkuu.

Ningekuwa nchi ya TZ, mtoto wangu hangekanyaga shule ya English medium hata siku moja. Hamjui baraka mlio nayo nyie.
hapa mkuu bado nashindwa kukuelewa,si ni nyinyi majirani zetu mnatucheka kila siku "watanganyika" kwa kutojua kingereza?!,kwamba hatuna confidence ya kujieleza kwa kingereza?!.tumeona bora tuchukue tahadhari mapema kwa kuwapeleka watoto wetu shule za english medium ili wanenu wasije wakawacheka wenetu huko ukubwani kwao,kama nyinyi mnavyo tucheka sie wazazi wao.:becky:

Huu ni wakati wa mtoto kusoma hadithi, shairi, kujifunza michezo ya kuigiza ili kupanua ubongo wake. Kujifunza hisabati kwa undani na kufanya "Word problems" nyingi. Kwa kusema ukweli, sioni haja ya kumfundisha mtoto lugha ya Kifaransa.
nakubaliana nawe ktk swala hilo michezo,hadithi,ushairi nk,kwa mfano shule ambayo anasoma binti yangu,wana somo linaloitwa vocational skills(VS),ambapo mambo yote yanayohusiana na talent za watoto yamejumuishwa humo ndani.kuhusu kifaransa naomba niunge mkono point ya MK254 hapo juu.
kwa kuongezea tu,siku hizi kuna shule tz,watoto wanafundishwa mpaka somo la lugha ya kijerumani na kichina.

Kumfundisha mtoto kwa lugha asiyoelewa, ni kumfanya mtoto awe na Intellectual dependency. Inauwa creativity ya mtoto kabisa. Mwalimu anapouliza "when do we have a bath" Mtoto Kasema Morning, Afternoon, and Evening. Kweli mtoto kaelewa swali? Na mwalimu anataka jibu gani? Watu huoga wakati tofauti tofauti. Lakini, mwalimu anataka mtoto ampe jibu la kukariri. lile ambalo waliimba na kukariri darasani. Hatakati mtoto ajifikirilie.

nakubaliana na wewe ktk hili,lakini tutizame na upande wa pili wa shilingi.hudhani kwamba kumfundisha mtoto kwa lugha yake pekee aliyo izoea kama kiswahili,kutamfanya ufungamane ktk kutafakari na kuchambua mambo kwa mapana yake?.

Ushawahi kujiuliza ni kwanini unampata Injinia mzima na ile elimu yake ni ya nadharia tu? Ushawahi jua kuwa 50% wa software engineers huko Apple hawana degree? Kwanini sisi waafrika na hizi degree zetu zote hatuwezi hata kuunda baiskeli bila msaada wa mchina ama mzungu?
huwa siamini uwezo mtu kitaaluma upo ktk vyeti vyake.

Hebu tazama video hii...Hii ndio Elimu ningependa Wakenya tuwe nayo - sio matajiri pekee.

https://www.youtube.com/watch?v=87qkZraVuew&feature=youtu.be
asante mkuu nitaitazama.
 
Last edited by a moderator:
MwendaOmo
nimetoka kutazama ile video,hongereni wakenya.ila nimeshtushwa na hao wanafunzi niliowaona,mmoja msomali na watatu wahindi.bila shaka shule wanayo soma(SCLP Samaj School) ni for kids coming from the elite class of kenya,correct me if i'm wrong.nilitegemea kuona wanafunzi toka mashinani machakos,embu,kisii,kakamega nk ambako asilimia kubwa ya wakenya wa kawaida inapatikana.kwanini ni watoto wa kihindi na msomali mmoja?,tena kutoka ktk shule moja tu ambayo karo yake ni kubwa?

ukipata nafasi itazame hii.

au tazama hii
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom