Msondo ngoma wanadai walipwe mil 300 na WCB

Msondo ngoma wanadai walipwe mil 300 na WCB

Acheni utimu iachieni mahakama ifanye kazi yake, maana naona watu wanawafanya km msondo wajinga na hawajui kitu.
Hayo mambo yakifika mahakamani hizo Sheria zitawekwa mezani na kuangaliwa yupi yupo sahihi kwahiyo hakuna haja ya kujibishana na mshindi.
 
wazee walitakiwa kupewa chochote japo si 300M as long as WCB ni family yao kwa kua daimond alimsaidia muasisi wa bendi mzee Gurumo... Wangetakiwa wafanye kindugu zaidi ya kukimbilia mahakamani..
 
Hapo hakuna kesi yoyote..
Hio kesi siku ya kwanza tu hakimu ataipiga chini.
Kwanza kabisa hao msondo ngoma hawana Hati miliki ya hicho kionjo..
Kama wanayo basi kesi watashinda..
Hivi unaweza toa wimbo hujausajili BASATA? tena hawa wana CHAMUDATA unafkir huko kote hawakupitia?
 
Naona watu wanajadili hili suala kwa hisia zaidi kuliko uhalisia wa sheria za haki miliki...za kitaifa na kimataifa ni hivi:

1) Protection ya copyright ni automatic i.e sio lazima uisajili kazi yako ndio ipate legal protection la hasha..hii ni tofauti na ishu kama vile Trade marks na patents/innovations/inventions hizi ili zipate ulinzi kisheria ni lazima zisajiliwe katika mamlaka husika,ili mtu mwengine akitumia kimakosa (bila idhini) uweze kumshtaki na kumdai fidia kwa kutumia trademark/uvumbuzi yako/wako kibiashara...

Huku kwenye copyright kinachohitajika ni msanii kuweza kuipublish kazi yake tu kwa umma basi,legal protection after that comes into play automatically no need for registration. Kwa hiyo kinacholindwa na sheria ni "expression of idea and not the idea itself" kwa mfano,umetayarisha kazi yako ya sanaa kisha ukaiweka ndani,lets say, kitabu cha riwaya ikawa bado hujakitoa kwa jamii ili watu waione hiyo kazi yako. Na baadae mimi nikaja kwako na kukiona hicho kitabu nikakichukua bila ridhaa yako nikaenda kukikopi chote half jina la mtunzi nikaweka langu baada ya muda mfupi nikawahi kukitoa kwa jamii kabla yako.

Katika mazingira kama hayo basi sheria itanilinda mimi mwizi na sio wewe original writer hii ni kwa sababu sheria na jamii now inanitambua mimi ndo kama original owner of the work coz ndo kwa mara ya kwanza waliiisikia/kuiona kutoka kwangu...sasa hata wewe ukija kuclaim baadae kwamba ile kazi ilikuwa ni ya kwako, watu wataona unatafuta kiki tu...rejea ishu ya diamond na dayana nyange kwenye wimbo wa "Namba one Orig."

2) Ili kuonekane kuna breach of copyrighted work for the purpose of enforcing it for compensation...lazima wrongdoer awe amecopy "the substantial part of the artistic work and not just little part". kwa mujibu wa sheria kinacho determine breach of copyright ni the extent/substantiality of the said breach and not mere breach, kuna wadau wamesema hapo juu kwamba at least ifikie 20% ya copied work .na lazima hiyo kazi iliyokopiwa itumiwe na huyo wrongdoer for economic gain,mere fair use does not amount to breach of copyrighted work.

Kwa hiyo wazee wetu wa Msondo kwenye hii kesi yao hawataambulia kitu..kwa sababu sehemu wanayodai kuibiwa kazi yao ni nduchu sana kwenye kazi nzima ya Zilipendwa...yaani ni kule mwisho mwisho wa wimbo ktk kukazia kazia tu utamu wa beats.

All in all, so far hakuna haki iliyovunjwa kwa hao wazee...na hapo mimi nimetaja point moja tu ila kuna hoja nyingi hapo zitaibuka,ikiwemo umiliki wa huo wimbo/beats,kama kweli wcb wamecopy au ni mfanano tu wa mapigo ambacho ni kitu cha kawaida. Kama ni rahisi kiasi hicho nazani watoto wa marehemu Rajabu Marijani nao waje wawadai WCB hususani Harmonize kwa kutia kionjo kidgo cha wimbo wa Sina Makosa kule mwisho mwa wimbo wa Zilipendwa..."yelelelileleeeeee"

Mawakili wao ni ama hawajui vyema sheria za copyright au wanajua ila wanataka tu kula hela za maskini hao kwa kuwa vyuma vimekaza,hivyo hata ule ubinaadamu umewaondoka.
 
Lazima hakimiliki zilindwe,hakuna kumtetea muhalifu wa kazi za sanaa.
 
"Hee mwanamama,baby mwanamama",darasa nae ajiandae,ila jamaa sijui ana bahati mbaya, bele9 na darasa wameiba vionjo vya saida ,kiba nae kairudia kimaso maso ya Issa matona lkn hawajatozwa hata shilingi, ila ndio hivyo MTU chake ngojea mahakama iamue .
Never know,huenda walishazungumza before
 
Msondo Ngoma maisha yao yote ya muziki hakuna aliyewahi kushika milioni ya pamoja, leo hii wamepanda bei ghafla? Haya.
Haki yao ni haki yao tu,ndo umuhim wa HAKI MILIKI HUO
Njaaa hizi ni shida kionjo m300 akat haya mauzo ya wimbo og hayakufka m1 huu ungese
Ulizia masuala ya HAKI MILIKI ndo utaelewa
Hebu acheni ujinga wale watu wamekaa wakabuni ni Kazi za ubunifu wao halafu mnasema Leo wananjaa acheni mapenzi ya kijinga lazima tuthamini Kazi za wazee wetu
Waelekeze hao hawaelewi
Acha wanyooshwe. Huwezi kuchukua tu sehemu ya wimbo wa mtu bila prior agreement. Ni dharau kwanza.
Tena sana,hapo lazima watayamaliza tu,ni KOSA
 
Mauzo Habari ndio Iyo ya Mwana Fa & Ay yalifika 2+ Billion...?mbona tigo wanatakiwa kulipa unapodai haki zako ukumbuke kutonyang'anya za wenzako.
_20170722_152450.JPG

Nakukumbuka sana Mkuu,kila napopata wasaa huwa nasoma HII.
Na nawarushia naowafaham
 
haleluya nayo rungu! laja. si unaiju ile i wanna know........ sijui nini huko
 
haleluya nayo rungu! laja. si unaiju ile i wanna know........ sijui nini huko
Huwezi kudai breach of copyright kwa mtu kutumia maneno kama halelluyah kwenye ngoma yako...Ikumbukwe Copyright law hailindi kila piece of work,kuna baadhi ya maneno ni free use,huwa hayana mmiliki binafsi ambae anajulikana.

Hicho kionjo cha Halellujah..iimetumika na wasanii wengi sana dunia...Techno pia ana ngoma ambayo mwanzo mwisho anaimba hilo neno halellujah,na kama ukiisikiliza kwa negative mind unaweza sema diamond kamkopi huyo Techno.
 
Eminem amelipwa USD 400,000+ na chama cha siasa huko ulaya kwa mambo haya haya,wametumia vionjo vyaje kwenye kampeni zao,ndugu yangu unaelewa thaman ya haki miliki wewe?
Umeifuatilia kiundani hiyo ishu ya Eminem hlf ukacompare na hili la Msondo? au umeona title tu ya hiyo habari hlf ukareach into your own conclusion bila kujua what exactly transpired?
 
Ila haikuwa fare na ni dharau kuchukua Kazi ya MTU ni sawa na wizi heri hata wangewaomba hata MTU anaweza kukupa bure usawa umekaba na wao wameiona hela hio. Pia wcb wapo kwenye music industry na wanafahamu ni kosa kuchukua Kazi ya MTU Mfano wao wangechukuliwa Kazi yao wangechukua uamuzi UPI?Cha msingi hapo wajirudi wawe wapole wawaite wenzao wakae chini wazungumze kitanzania.
 
Kuna ushawishi wa mawakili hapo na wahuni wengine ili wapige mapene ya nguvu.
Kijana kama Diamond kutumia vionjo vya wazee ni kutambua uwezo wao.
Kuna genge nyuma ya haya madai ya wanaodaiwa kuwa msondo.
 
Vyuma vimekaza ndo maana tumebaki Magari home ukigusa tu lami lazima uwe na akiba ya 30 tunawogopa wale wa rangi nyeupe kama mama mkwe,hata smartphone yako inabidi utaype kimakini neno moja moja ukienda race andaa milioni 7 wenyewe wanazitaka,Hivo msondo wameona hela iko nje nje hawawezi iacha kila MTU anaangalia wapi pana upenyo upate unafuu shoo zao hazilipi kama zamani biashara imebadilika.
 
Umeifuatilia kiundani hiyo ishu ya Eminem hlf ukacompare na hili la Msondo? au umeona title tu ya hiyo habari hlf ukareach into your own conclusion bila kujua what exactly transpired?
Eminem kuna chama kilitumia KIONJO cha wimbo wake,just kionjo tu,na niliskiliza instrument ya wimbo wa eminem na hiko kionjo na yeye hakujua ila aliambiwa tu ndo wakaanza kufatilia.
Na WCB wametumia KIONJO cha wimbo wa MSONDO just KIONJO tu.
Kwa kuhitimisha bOTH WCB na Kile chama cha New Zealand wametumia vionjo.
So tuaubiri kesi itakapoanza,au kama una la ziada kuwa JAMAA HAWAJATUMIA KIONJO CHA MSONDO?
 
Back
Top Bottom