Mwanahabari Huria
JF-Expert Member
- Jan 29, 2025
- 406
- 308
Katika mhadhara wa umma Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA), Mkurugenzi wa PPPC Bwan David Kafulila alieleza kuwa tangu kuanzishwa kwa mfumo wa ubia, serikali imefanikisha miradi yenye thamani ya takribani trilioni 6, na mwaka 2011 pekee miradi hiyo ilikuwa na thamani ya shilingi trilioni 2.5. Hadi sasa, miradi ya ubia imefikia thamani ya zaidi ya shilingi trilioni 8.5, ikionyesha ukuaji wa kasi na mchango mkubwa wa sekta binafsi katika maendeleo ya taifa.
Kafulila alitaja uwekezaji mkubwa wa TAZARA ambapo zaidi ya asilimia 60 ya uwekezaji huo upo Tanzania. huku Tanzania akiwa ni mnufaika mkubwa kuliko Zambia kwa sababu ina ukanda wa bahari, wakati takribani asilimia 90 ya biashara ya dunia hufanyika kupitia bahari. Aliongeza kuwa Tanzania ina ukanda wa bahari wenye urefu wa zaidi ya kilomita 1,400, na bandari ya Dar es Salaam imekuwa lango kuu la biashara kwa nchi nyingi ikiwemo Malawi, Zambia na DRC.
Alifafanua kuwa faida ya kijiografia pekee haitoshi, bali inahitaji uwekezaji mkubwa ili kuibadilisha kuwa faida ya kiuchumi. Alisema kuwa uwekezaji katika bandari, reli na barabara ni muhimu ili mizigo inayofika bandari ya Dar es Salaam iweze kusafirishwa kwa haraka na ufanisi, ikilinganishwa na bandari za Mombasa au zinginezo.
Kafulila alisisitiza kuwa ufanisi wa bandari ni sharti ili Tanzania iweze kufaidika kikamilifu na nafasi yake ya kijiografia.
Kafulila alieleza kuwa tangu kuanzishwa kwa mfumo wa ubia katika bandari, shughuli za usafirishaji zimeongezeka zaidi ya mara tatu katika muda mfupi. Alisema kuwa hii ni ushahidi wa namna PPP inavyoongeza ufanisi na kupanua huduma za bandari. Hata hivyo, alionya kuwa changamoto bado zipo na zinahitaji suluhisho endelevu ili kuhakikisha kuwa uwekezaji huu unakuwa wa kudumu na wenye tija kwa taifa, "Kibaha-Chalinze msongamano wa malori umeongezeka "
Akihitimisha, Kafulila alitaja mradi wa China Civil Engineering Construction (CCC) unaofufua reli ya TAZARA, ili kurahisisha usafirishaji wa mizigo kwenda Zambia na DRC kupitia bandari ya Dar es Salaam. Alisema kuwa bahati ya Tanzania siyo tu kuwa na bandari, bali kuwa na bandari katika Bahari ya Hindi, ambayo ndiyo kitovu cha biashara ya dunia.