Msongamano mkubwa wa Malori ya Mizigo Dar-Chalinze kwa sasa ni matokeo ya Ubia (PPP) Bandari ya Dar es salaam-David Kafulila

Mwanahabari Huria

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2025
Posts
406
Reaction score
308
Katika mhadhara wa umma Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA), Mkurugenzi wa PPPC Bwan David Kafulila alieleza kuwa tangu kuanzishwa kwa mfumo wa ubia, serikali imefanikisha miradi yenye thamani ya takribani trilioni 6, na mwaka 2011 pekee miradi hiyo ilikuwa na thamani ya shilingi trilioni 2.5. Hadi sasa, miradi ya ubia imefikia thamani ya zaidi ya shilingi trilioni 8.5, ikionyesha ukuaji wa kasi na mchango mkubwa wa sekta binafsi katika maendeleo ya taifa.

Kafulila alitaja uwekezaji mkubwa wa TAZARA ambapo zaidi ya asilimia 60 ya uwekezaji huo upo Tanzania. huku Tanzania akiwa ni mnufaika mkubwa kuliko Zambia kwa sababu ina ukanda wa bahari, wakati takribani asilimia 90 ya biashara ya dunia hufanyika kupitia bahari. Aliongeza kuwa Tanzania ina ukanda wa bahari wenye urefu wa zaidi ya kilomita 1,400, na bandari ya Dar es Salaam imekuwa lango kuu la biashara kwa nchi nyingi ikiwemo Malawi, Zambia na DRC.

Alifafanua kuwa faida ya kijiografia pekee haitoshi, bali inahitaji uwekezaji mkubwa ili kuibadilisha kuwa faida ya kiuchumi. Alisema kuwa uwekezaji katika bandari, reli na barabara ni muhimu ili mizigo inayofika bandari ya Dar es Salaam iweze kusafirishwa kwa haraka na ufanisi, ikilinganishwa na bandari za Mombasa au zinginezo.

Kafulila alisisitiza kuwa ufanisi wa bandari ni sharti ili Tanzania iweze kufaidika kikamilifu na nafasi yake ya kijiografia.

Kafulila alieleza kuwa tangu kuanzishwa kwa mfumo wa ubia katika bandari, shughuli za usafirishaji zimeongezeka zaidi ya mara tatu katika muda mfupi. Alisema kuwa hii ni ushahidi wa namna PPP inavyoongeza ufanisi na kupanua huduma za bandari. Hata hivyo, alionya kuwa changamoto bado zipo na zinahitaji suluhisho endelevu ili kuhakikisha kuwa uwekezaji huu unakuwa wa kudumu na wenye tija kwa taifa, "Kibaha-Chalinze msongamano wa malori umeongezeka "
Akihitimisha, Kafulila alitaja mradi wa China Civil Engineering Construction (CCC) unaofufua reli ya TAZARA, ili kurahisisha usafirishaji wa mizigo kwenda Zambia na DRC kupitia bandari ya Dar es Salaam. Alisema kuwa bahati ya Tanzania siyo tu kuwa na bandari, bali kuwa na bandari katika Bahari ya Hindi, ambayo ndiyo kitovu cha biashara ya dunia.

Your browser is not able to display this video.
 
Aache ujinga; msongamano ni matokeo ya miundombinu mibovu pumbavu zake
 
Yaani kama mkuu wa kaya anayefurahia watoto kwenda chooni mara kwa mara akidhani ni shibe, kumbe hajui watoto wanaumwa matumbo ya kuhara!!
 
Viongozi wa awamu hii wanamavi kichwani.msongamano wa malori sababu ni ufinyu wa barabara zetu na si vinginevyo.

..fedha za kujenga viwanja vya afcon zipo.

..halafu fedha za kujenga barabara na miundombinu itakayosaidia bandari zetu hakuna.

..kwanini hawakuitisha ppp kujenga viwanja vya Afcon halafu miundombinu ya umma tukajenga wenyewe?
 
Ni aibu kubwa mtu kutoa maelezo ya kipumbavu kwa kiwango hicho, kadri idadi ya watu inavyoongezeka obviously na ukubwa wa mahitaji unaongezeka hivyo miundo mbinu inapaswa kuwa inapanuliwa kitu ambacho hakifanyiki hence huu msongamano ambao yeye analeta utapeli kuwa msongamano ni mafanikio wakati kiuhalisi msongamano una-reflect kufeli kwa mipango ambayo kama ingefanyika kwa usahihi na kwa wakati ingeondoa msongamano.
 
Msongamano wa malory ni matokea ya udhaifu katika mipango yetu wala sio suala la mafanikio ya ppp
 
Wewe jenga hoja acha maneno
 
Naona hajaeleza kwanini tuliamua kuiua Tazara, na sasa tunaikwepa Sgr ili malori yetu yabebe mizigo kwa gharama za wananchi ambapo kila mwaka tunakarabati barabara kwa gharama kubwa kuliko faida.
 
Ni kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…