Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Unaweza kudhani magari yameegeshwa au kuna maandamano ya magari, lakini uhalisia ni kwamba gari zinasubiri kujaziwa gesi.
Hali hiyo ipo leo Jumanne Oktoba mosi, 2024 kwenye kituo cha kujazia gesi ya magari Tazara jijini Dar es Salaam, ambako msululu wa magari umeanzia kwenye kituo hicho hadi kuelekea kwenye mataa ya Tazara (umbali wa mita 400).
Mwananchi Digital ilifika eneo hilo na kuzungumza na baadhi ya madereva waliokuwa wakisubiri kujaziwa gesi, baadhi yao walisema wamekesha kituoni hapo.
“Nipo hapa tangu saa tisa alasiri ya jana, mpaka sasa sina uhakika wa kupata huduma kwani mbele yangu kuna bajaji zaidi ya 50,” amesema mmoja wa madereva hao.
Baadhi yao wameeleza kuwa wamezunguka vituo vyote kuna shida, cha Uwanja wa ndege hakifanyi kazi, cha Ubungo pia kina shida. Huku wakazi wa Kigamboni wakilazimika pia kuja Tazara ambako kuna pampu moja, kwani hawana kituo cha kujazia gesi hata kimoja.
Soma Pia: Dkt. Mwigulu: Tusamehe ushuru wa magari ya umeme na Gesi