Mstaafu akifariki malipo yake ya kila mwezi hukoma baada ya muda gani?

Mstaafu akifariki malipo yake ya kila mwezi hukoma baada ya muda gani?

Wanajanvi naomba msaada. Ivi mstaafu akishafariki pesa alizokua anazolipwa kila mwezi huwa zinakoma baada ya mda gani? Haswa kwa sheria zao za mafao ya wastafu
Kwa mifuko ya hifadhi anahakikiwa Kila mwaka ila wale wa hazina ndio mpaka miaka minne au mitano...so pesa itakoma asipoenda kuhakiki
 
Analipwa miaka 12.5 baada ya kustaafu acha ubishi
Uoñgo ile ni formula tu wako walimu waliostaafu miaka ya 80 hadi leo wanalipwa pension wako kibao walimu,madaktari,manesi wafanyakazi wa bandari,TRA nk wako wazee kibao
Unaongea usichojua

Unaongea academically sio practical acha kukariri notes wewe elewa somo
 
Ninachofahamu ni kwamba mafao ni miaka 12.5 baada ya kustaafu.
Baada ya kufa sina uhakika ni muda gani.
Baada ya mstaafu kufariki? Mafao yake ya kila mwezi yanaishia hapo hapo. Kwani kila mwaka huwa anatakiwa kuhakikiwa macho kwa uso, kama atafariki baada ya uhakiki huo, familia isipotoa taarifa itaendelea kupokea mafao hayo hadi uhakiki mwingine utakapofika.
 
Uoñgo ile ni formula tu wako walimu waliostaafu miaka ya 80 hadi leo wanalipwa pension wako kibao walimu,madaktari,manesi wafanyakazi wa bandari,TRA nk wako wazee kibao
Unaongea usichojua

Unaongea academically sio practical acha kukariri notes wewe elewa somo
Una bahati sana yule mchawi alikumbuka kukuachia akili yako.
 
Wengine wanatumia alama za vidole kama unavyosajili simu wana vimashine vyao mtu ukienda hata uwe pacha wa Marehemu hutoboi unaweka dole kinatoka kitambulisho chako cha taifa sasa wewe kama siye dole tu hakitatoka
Kweli, wasije kuishia Segerea bure.
Heri wakaushe mpaka itakapokoma au watoe taarifa wasitishe
 
Hebu nisahihishe ile 12.5 kwenye formula maana yake nini?
Ulikoikota hiyo formula kaulize huko huko ila mafao ya kila mwezi huwa hayakomi hadi mstaafu afariki dunia hata awe na miaka mia wakati alistaafu akiwa ana miaka 60
 
Zamani hata miaka 5 ila sasa uhakiki wa face to face hutoboi. Labda mumtafute ndugu anayefanana naye awe anakwenda yeye kuhakikiwa

Uhakiki hufanyika kila baada ya mwaka mmoja na unafanyika kwa njia ya dole gumba. Hata ukifanana haikusaidii
 
Hebu nisahihishe ile 12.5 kwenye formula maana yake nini?
Hiyo miaka huwa ni kigezo cha chini cha mfanyakazi kuweza kuchangia michango ili kuwa na sifa ya kulipwa pensheni. Ndio maana serikalini/sekta binafsi mwisho wa umri wa kuajiriwa huwa ni miaka 45,ili aweze kuwa na miaka 15 ya kuchangia hadi ana stafu. Ndio maana kwenye fomula wanaitumia hiyo 12.5.
Miaka 12.5 ni kadilio tu la kuwa utaishi miaka 12.5 baada ya kustaafu. Ukitoboa hiyo 12.5 utaendelea kulipwa mpaka ufe
 
Back
Top Bottom