Mstaafu Kasinde Matata πŸ₯°

Kasie

Platinum Member
Joined
Dec 29, 2013
Posts
22,379
Reaction score
41,294
Wakulungwa hamjamboooo....!??

Ule wakati niliokuwa nausubiria kwa hamu sasa umefika. Hatimaye bibi Kasinde amestaafu na kulipwa stahiki yake kwa kuitumikia Jamuhuriya Muungano wa Tanzania kwa kipindi kisichopungua miaka 35.

Yaani waliosema pesa sabuni ya roho hawakukosea, mweeh mweeh yaani najikuta namtabasamia kila nnayepishana naye njiani.

Hapa natembea kwa mguu hadi Ocean Road nikashangae na bahari...

Magorofa nimeyashangaa hadi naona shingo inataka kwenda mrama sasa...πŸ˜…πŸ˜…









Karibuni tukale samaki wa baharini kwa wale walioko feri.

Update:

Wacha nimalizie matukio ambayo sikuyarusha kwa wakati..,,


Mjini kutamu nyieee.... acha tuu

Pamoja na kuwa nimestaafu shamba siendi ng’oo...😜


Wakulungwa si watu wazuri....

Walimtegea jiwe bi Kasinde, nilijikwaa ila sikuanguka... kiatu ndo kilipata hitilafu ikabidi nipate huduma kwa shushani...
 

Nije kukusaidia kutunza hela[emoji4]
 
Hongera bibi Kasinde
Karibu inyonga Kwa wajomba zako

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 

Hongera sana kwa utumishi wa mda mrefu,ila kuwa makini,kuna wimbi la watoto kuua wazazi linaendelea[emoji3]
 

Hongera sana Kasie, nakuombea maisha mazuri na marefu ya ustaafu baada ya kuitumikia Jamhuri. Kwa humu JF wewe ni kati ya watu wachache ambao siku zote uko positive, na unapenda wengine wafurahi. Kila lakheri Kasie.
 
Hongera Bibi Kwa kulitumikia taifa lako Kwa Miaka mingi hiyo,
Ila nakuomba Sana baada ya kuipata stahiki Yako Kaa mbali na
Motivation speakers hao wakiona ushapata papers watajidai wanakupa mbinu za kufuga kuku wapuuzie ukifika msimu wa mdondo zitapukutika zote!

NB: huo ni mfano tu
Enjoy yourself!
 
Bwana mi sijaelewa, eti umestaafu. Maandishi yako hayaoneshi chembechembe za uzee mbona.
 
Unaweza kuwa mtu mzima Ila siamini kama ni uzee wa kustaafu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…