..
...leo tujadiliane hii kitu emotional rollercoaster. Pale mwenza wako (Psychological Abuser) anavyoutumia udhaifu wako. "Sleeping with the Enemy" ni sinema mojawapo inayotoa mfano mzuri wa hili.
Tujadiliane Ex- wife/husband/partner anapoendesha hisia zako atakavyo; -Swahili Slang- 'kuwekwa kidoleni,' 'kushikwa pembe,' 'kuwekwa mkononi,' etc na athari zake, kwa muda mfupi na muda mrefu.
Mbu ..Thanks a lot kwa hii mada. Kumbuka mada zako huwa zinatuumiza sana vichwa kwani zinalenga maisha halisi..
Mkuu..kuna kitu bado kinanisumbua..yaani maujanja yangu yote bado sijakubaliana na maana halisi ya mapenzi. Labda ni mshamba, au labda sijawahi kupenda au akili yangu bado imekumbatia maana ya mapenzi kuwa ni Myth. Yaani hakuna kitu kinaitwa mapenzi..au maana ya mapenzi inabadilika daima kama kinyonga...
Ninaposema mapenzi ni mysterious thing ni kwamba mambo yote yanayohusu mahusiano yanaendana na mazingira, feelings, wakati, umri, uchumi, dhiki, uchungu, furaha etc..
Kuna njia nyingi unaweza kuwa msukule wa mapenzi bila kujijua..na wakati ukiwa katika status hii ambayo inamahusiano na vitu nilivyotaja hapo juu..Yule mshiriki wa pili mara nyingi "EX" ana uwezo wa kushika remote control na kukuchezea atakavyo.. ni kwa sababu gani? hizi hapa..
First decision is always right! ..Ukitafakari sana huu usemi una ukweli..na katika mpenzi ni vigumu kumsahau mpenzi wako uliyemkabidhi moyo wako kwa mara ya kwanza..unahitaji kujenga mazingira kukwepa kishawishi cha kutosumbuliwa .. EX" akijua au kuona dalili toka kwako kuwa First decision or choice is always right! atakuchezea kwa remote control bila wewe kujijua..
Upendo wa kweli kwa watoto na uchungu wa mwana..Yaani ukitengana na mke/rafiki/mume mliopata na nae watoto ..msukule na jinamizi la watoto litakuandama.. ni uchungu wa mwana na wala sio wewe..na wala sio msukule..Utafanya chochote kile bila kujijua
Faith..tamaduni..mila .. etc... Mwenza wako anakudhalilisha ..anakupiga..lakini wazee, wachungaji na jamii inakupa moyo.."ndoa ni uvumilivu" zidisha maombi..yaani utabaki msukule..hadi maombi yako yawe ya kweli..
Uchumi na kukosa kujiamini..yaani ukifikiri kitachofuata ukitoka kwenye mahusiano kina kuacha hoi...utabaki unaogopa..na utakubali kukumbatia msukule bila kujijua....Hii ni moja ya weakness za binadamu ambazo ni`kuogopa changes au kuogopa ku-take risk!
Thanks again bro, Nawakilisha hayo....