The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Mbunge wa Jimbo la Geita, Joseph Kasheku maarufu kama Musukuma, leo ameibuka katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Geita kwa lengo la kuchukua fomu ya kuwania ubunge kwa awamu nyingine.
Musukuma aliwasili katika ofisi hizo majira ya saa 9:35 alasiri, akiwa ameambatana na Katibu wake. Alipokelewa rasmi na Katibu wa CCM Wilaya ya Geita, Michael Msuya, ambaye alimkabidhi fomu ya kugombea ubunge wa Jimbo la Geita kupitia tiketi ya chama hicho tawala.
Hatua yake ya kurejea kuwania nafasi hiyo imeibua tafsiri mbalimbali kwa wanachama na wakazi wa Geita, wengi wakiona ni ishara ya kutaka kuendeleza miradi na ahadi alizozianzisha katika kipindi chake cha ubunge.
Hata hivyo, kilichoibua gumzo zaidi katika tukio hilo ni muonekano wake wa kipekee, uliowavutia na kushangaza wengi waliohudhuria, hali iliyofanya baadhi kumfananisha na ninja kutokana na vazi lake kubwa la koti akiwa amevalia na kofia ya koti hilo.