Msuluhishi wa kesi ya waliokuwa wafanyakazi wa TBL atoa maamuzi yenye utata

Msuluhishi wa kesi ya waliokuwa wafanyakazi wa TBL atoa maamuzi yenye utata

Jana tarehe 14/ 09/ 23 Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ametoa maamuzi yenye utata kwenye shauri la usuluhishi lililokuwa mbele yake. Wafanyakazi wa zamani wa kampuni ya Bia Tanzania (TBL) waliishtaki kampuni hiyo wakiituhumu ubadhirifu wa mabilioni ya pesa za Mfuko wa Hisa za Wafanyakazi wake.

Waliibua utata wa mkataba wa mfuko huo wakidai wadhamini waliweka masharti ya kuhalalisha ubadhirifu walioufanya wakiwatuhumu wadaiwa kwa ubadhirifu wa zaidi ya Sh83 bilioni ziliokuwemo katika mfuko huo.

Jaji FAUZ Twaib katika maamuzi yake amesema wanaostahili kulipwa ni wale tu waliokuwapo kati ya tarehe 24 Novemba 2011 na Desemba 2017.

Lakini mfuko huu ulianza mwaka 1998, sijui ni sababu zipi zilizopelekea maamuzi hayo. Ruling yenyewe hii hapa
Walishalipwa?Maana naona makampuni mengi yanalalamikiwa,wakiwemo T.C.C
 
Rudia kusoma hukumu, iwapo kesi imeanza kusikilizwa zaidi ya miaka 5 iliyopita na ilianzia mahakama kuu ikaamuriwa lipelekwe kwa Arbitrator (Msuluhishi) aliyependekezwa na kukubaliwa na kila kundi lenye kulalamika na kwamba lilete ushahidi wakiwakilishwa na mawakili nguli. Kwa sasa hicho ni kilio cha kutapatapa kwenye social media ili kupata huruma ya wanajamii na yamkini wengi wao wasio na ufahamu wa mambo ya sheria. Hukumu haina rufaa hiyo ndio imeenda.
Rufaa ni Haki ya mtu mkuu!
 
Back
Top Bottom