Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
JESHI la Polisi nchini Msumbiji linamshikilia mwanaume mmoja baada ya kumkuta na kichwa na sehemu za siri za mwanaume ambaye amekiri kuuua mtu na kukata viungo hivyo.
Msemaji wa kamandi ya polisi ya Sofala, Dércio Chacate, amesema Watoto waligundua sehemu za miili hiyo kwenye mfuko wa plastiki katika wilaya ya Nhamatanda na kutoa taarifa kwa mamlaka.
“Mshukiwa alikiri kuua na kukata vichwa vya watu wengine watatu, uchunguzi unaendelea ili kuwakamata wanaodaiwa kuwa wapangaji na wanunuzi wa viungo hivyo” amesema Chacate.
Viungo vya mwili hutumiwa na baadhi ya wanaoitwa madaktari wa jadi kutengeneza dawa, ambazo kwa uwongo wanadai zinaweza kutibu magonjwa, kuondoa dalili mbaya na kuboresha maisha ya watu.