Synod
JF-Expert Member
- Oct 10, 2016
- 4,143
- 4,180
Ndio maana sisi huwa tunawaambia ndugu zetu wabongo, Kenya ndio Nchi pekee huu ukanda ambayo ni rafiki na ambao hawana unafiki kwa mambo hayo.
kama wale wa Pemba elfu zaidi ya sita wapo hapa Kenya bila vibali na badala ya kuwafukuza wanaomba serikali iwape vibali. Na serikali ina wasikiza tu!!
Wabongo wanaochukia Kenya huku wakitusi kwenye mtandao huu wa JF kwamba Kenya sijui Kibera, sijui ukabila, mjue wakenya ni wastaarabu na humfaa yeyote akiwa kwenye matatizo.
Hivi tudumishe upendo, mambo hadi Raisi wa Tanzania anaanza kusema kwenye jukwaa mambo kuhusu Kenya si vizuri. Nilimsikia juzi akisema kwamba, wakenya wasidhani kwamba kila kitu kizuri ni cha Kenya, na sikuweza kufahamu iweje Raisi huyu anaongea mambo kihivi.
Rwanda itawakimbiza Msumbiji, Malawi ndio hiyo kuna shida, Sasa mkianza Kenya kutakuwaje???
Mkuu umesahau kitu kimoja kuwa Kenya na Tanzania chuki yao iko kwenye suala la Maendeleo tu na sio vitu vingine,
Namaanisha kuwa nchi hizi mbili sasa hivi zinafukuzana sana kila moja ikijitahidi kuizidi nyingine!
Linapokuja suala la undugu, sisi bado ni ndugu na ndo maana Kenya ilikuwa ni moja ya nchi za awali kitembelewa na JPM