Msumbiji wameingiwa na wazimu wa kuwasaka Watanzania, hivi Wakenya tupo salama kule??

Mkuu umesahau kitu kimoja kuwa Kenya na Tanzania chuki yao iko kwenye suala la Maendeleo tu na sio vitu vingine,

Namaanisha kuwa nchi hizi mbili sasa hivi zinafukuzana sana kila moja ikijitahidi kuizidi nyingine!

Linapokuja suala la undugu, sisi bado ni ndugu na ndo maana Kenya ilikuwa ni moja ya nchi za awali kitembelewa na JPM
 
Wewe hata unajua unachokisema??
 

Haifai iwe na chuki.

Mara nilikasikia Watanzania wakisema eti Kenya tunamashauo na hutaka vitu vyao kama Kilimanjaro.

Chuki kama hii haina haja, Kenya hatujawai leta tetesi zozote juu ya jamhuri ya Jumuia Ya Tanzania, ama jirani wetu wowote!

Mbona Tanzania inavuruga urafiki??? Deal yoyote iwe Kenya ipo basi Tanzania imejitoa
 
Operesheni inayoendelea Msumbiji ni dhidi ya wahamiaji haramu wa kutoka nchi zote na sio Tanzania peke yake. Vyombo vya habari vya Tanzania vinaleta ushabiki maandazi kuonesha kuwa Msumbiji inalenga Watanzania tu. Mtindo huu wa kijinga wa vyombo vya habari unaweza ukaleta chuki kubwa kati ya watu wa Tanzania na watu wa Msumbiji.
Kuhusu Tanzania kuisaidia Msumbiji wakati wa kupigania uhuru, hii haiwapi Watanzania kibali cha kuingia Msumbiji kinyume cha sheria za Msumbiji.
 
Kwaiyo unamaanisha msumbiji ni Matajiri?
 

Ni kweli hivyo, lakini ulivyosikia kwenye hiyo simu aliyoipiga jamaa mmoja toka hizo sehemu akitoa tetesi kwamba sio kuwasaka tu, wanadhulimiwa, wanawake wakibongo kubakwa na askali zaidi ya sita. Wengine kuwekwa Jela na hata kuchukuliwa mali yao, huo sio msako tu bali, ni ukosefu wa haki za kimsingi kwa watu, hasa majirani. Naona hili jambo watu wa Msumbiji kidogo wamekosea.

Nadhani haya yote ni kwa sababu ya madini. Wamsumbiji wanaona ni kama Watanzania wananufaika kwa raslimali yakimsumbiji!!
 
Ni kweli neno chuki linaongeza ukakasi, pengine tutumie neno mbadala!

Lakini kuhusu hizo tuhuma nyingine, as long as zinahusu Kenya na tz, tuziache labda tutazijadili kwenye thread husika, tukikite kwenye hii hoja ya hawa watu wa msumbiji
 
Mkuu si kweli kwamba nchi ya kenya na tz zinafukuzana kimaendeleo never ever tz huwez ifananisha na ke bado sana yaani
 
Tanzania ndio nchi ya ajabu duniani na iliyojaa wajingaa wengi sana.

Yaani watanzania wanapigwa, wanabakwa na kufukuzwa kama mbwa huko Msumbuji halafu serikali ya Tanzania kupitia msemaji wake(Katibu Mkuu wa wizara) katika wizara ya mambo ya nchi za nje inasema "Hakuna tatizo lolote kwa msumbiji katika hatua hizo za kuwafurusha watanzania, ni mambo ya kawaida, na watanzania hao huenda walikuwa huko Msumbiji kinyume cha sheria nk."
 
Wakati mwingine nafikiria kimbelembele cha kuwasaidia msumbiji na SA tulikitoa wapi. Watu gani hawakumbuki fadhila.!?
Kweli shikrani ya punda ni mateke....
Mfadhili mbuzi.....
binafsi kimbembele ni chetu sisi,kwa nini tulitaka saidia wote at our expense,sisi wenyewe tuliyataka haya
 
Tunaomba Serikali itupatie majibu ya nini kinaendelea Mozambique. Serikali ifanye njia mbadala kuwasaidi wale ambao wako tayari kurudi Tanzania. Vipi Waziri Mahiga yupo wapi? Hata kama hawako kihalali huko international laws lazima zitumike huwezi kuwabaka wake za watu na watoto kiholela.
 

Wale jamaa wa Msumbiji naona ni wapuzi mno!! Hivyo ujinga gani huo wanaofanya, wanawake wao wakibakwa wangehisi vipi!!! Wapuzi wakubwa wale, mi huchukia sana watu ambao hawajui kuzingatia haki za kimsingi kwa wengine!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…