Msumbiji Wamekodisha Bandari ya Nacala Kwa Malawi & Zambia Kwa Miaka 100. Tanzania Kupoteza Mteja namba 2 wa Dar Port


..Lissu ana pointi nyingi za kiuchumi tatizo waandishi wa habari wamekazia kumuuliza mambo ya udaku.

..Unakumbuka darasa alilosomesha kuhusu Mgogoro wa Israel na Palestina na kila mtu ukashangaa?

..Sasa wa'challenge waandishi wamuulize kuhusu sera za uchumi ndio utajua jamaa anaifahamu dunia.
 
Kilichokua kinatakiwa ni kujenga miundombinu ya bara bara na kupunguza kodi ya truck tractors ili watu wawe na trucks za kutosha kwa kupeleka mizigo huko sasa wenzetu TRA wanadhani wanawakomoa Watanzania kwa kuweka kodi kubwa huku wenye mizigo wakiona gharama kubwa ya usafiri na kuchelewa wanaona watumie watu wao au kuhama Bandari...
 
Soma mada yangu uelewe,nimekwambia lazima tuji engage na DRC kutafuta amani Kwa maslahi ya Tanzania hasa ya kiuchumi.

Ndivyo Mabeberu wanafanya
 
Kiukweli wakitekeleza hili wazo lao ni maumivu kwa nchi yetu Cha msingi TAZARA irudi iwe chini ya wachina maana ili waifufue na nchi yetu iwekeze zaidi kwenye viwanda kwa kutenga angalau hata mji mmoja nyanda za juu kUsini uwe wa viwanda hii itasaidia hizi nchi kuendelea kuja kuchukua bidhaa
 
NA KAZI IMEANZA HII ITASAIDIA SANA KUUA HATA HILI WAZO LA ZAMBIA NA MALAWI 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇China, Tanzania and Zambia to sign an Investment Framework for TAZARA

On September 4, 2024, TAZARA will take center stage in Beijing, China, as Mr. Hakainde Hichilema, President of Zambia, Mr. Xi Jinping, President of China, and Dr. Samia Suluhu Hassan, President of Tanzania, come together to witness the signing of the Investment Framework for the revitalization of TAZARA, the Government of Zambia has announced.
--------------------------------------------------------
China, Tanzania na Zambia kutia saini Mfumo wa Uwekezaji wa TAZARA

Siku ya 4 Septemba, 2024, TAZARA itapanda jukwaani mjini Beijing, China, huku Mheshimiwa Hakainde Hichilema, Rais wa Zambia, Mheshimiwa Xi Jinping, Rais wa China na Mheshimiwa Dk Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania, wakikutana kushuhudia kusainiwa kwa Mfumo wa Uwekezaji wa kufufua TAZARA, Serikali ya Zambia imetangaza.
----------------------------------------Translated by Google.
PRESS STATEMENT
For Immediate Release
PRESIDENT HAKAINDE HICHILEMA TO UNDERTAKE WORKING VISIT TO THE PEOPLE’S REPUBLIC OF CHINA TO ATTEND THE NINTH FORUM ON CHINA-AFRICA COOPERATION SUMMIT
The Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation wishes to inform the nation that Mr. Hakainde Hichilema, President of the Republic of Zambia, will undertake a Visit to the People's Republic of China from 30th August to 7th September, 2024 to attend the Ninth Forum on China-Africa Cooperation (FOCAC) Summit.
The Summit, held every three years alternately in Africa and China, will be convened from 4th to 6th September, 2024 in Beijing under the theme "Joining Forces to Promote Modernisation and Build a High-level China-Africa Community of a Shared Future." President Hichilema will join other leaders at the Summit in advancing common growth and mutually beneficial development for the African continent and China.
On 4th September, 2024, President Hichilema will hold a bilateral meeting with His Excellency Mr. Xi Jinping, President of the People’s Republic of China, furthering the longstanding and excellent bilateral relations between Zambia and China, as the two countries this year commemorate 60 years of diplomatic relations. During the meeting, President Hichilema, together with President Xi and President Samia Suhulu Hassan of the United Republic of Tanzania will witness the signing of the Investment Framework on the revitalisation of TAZARA. The President is later on the same day scheduled to grace the Zambia Power Development Forum at the Power China Headquarters.
President Hichilema will further hold strategic meetings, on the margins of the Summit, with Government officials and investors, which will ultimately yield tangible benefits for Zambia. The programme includes a bilateral meeting with representatives of the China Railway Construction Corporation and China-Non-Ferrous Metals Corporation on 3rd September, 2024 in Beijing.
Zambia and China share longstanding strategic relations based on common values and mutual respect. The two countries cooperate based on the Comprehensive Strategic and Cooperative Partnership, which was elevated by President Hichilema and President Xi during the State Visit to China in September 2023. This year's visit by the President is highly significant as it will build on the agreed decisions and allow for the consolidation of Zambia’s ties with China, including unlocking opportunities for investment and joint partnerships in key sectors such as energy, agriculture, infrastructure and mining. President Hichilema’s international engagements reinforce the Administration’s ongoing efforts of accelerating socio-economic development and creating equitable opportunities for the Zambian people.
President Hichilema is expected to return to Zambia immediately after his engagements.
(Original Signed)
Hon. Mulambo Haimbe, SC, M.P
MINISTER OF FOREIGN AFFAIRS AND INTERNATIONAL COOPERATION
29th August, 2024
#FOCAC2024
#ZambiaChinaRelations
#DevelopmentCooperation
#ForeignAffairsZambia
 
Moja taarifa njema kbs hii kwa ujasusi wa kiuchumi. Yericko Nyerere ambayo amekuwa akipigia chapuo. Reli ya Tazara ipo sijui kama tunataka reli nyingine.

Tuwatumie pirates hapo hapo kati waogope kabisa 😀😀😀 kupitisha meli zao.
 
DP si wapo vizuri?
Maana tulisikia hata rate ya kupakua mizigo ni ya speed ya hali ya juu,meli hazikai sana.

Au ulikuwa uongo? MAANA WW kila kitu unasifia.
 
Hii ni Bad News kwa watu wengi kuanzia mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA), DUBAI PORT WORLD(DP World), TANZANIA REVENUE AUTHORITY(TRA) pamoja na wadau wote wakubwa wa bandari ikiwemo Clearing and Forwarding Agent.

Yale magari mnayaona pale bandarini yamejaa asilimia kubwa ni Transit(Zambia, Malawi, Congo, Burundi, Rwanda) the same kwenye Makontena.

It's really a bad news ambayo Kila anayehusika anapaswa ashike kichwa na kutafakari tutaokoa vipi mapato yaliyokuwa yanaingia In terms of billions.?
 
Bora hilo litekelezwe haraka.
Hapa nchini hata mabilioni yenyewe yanayopatikana wanagawiwa machawa halafu chenji ndo zinapelekwa TARURA zijenge barabara za vumbi huku vyoo vya shule tunasubiri misaada ya COVID-19
Ila kwa kweli wa-Tanzania tumezidi ubabaishaji, longolongo, rushwa, ufisadi na Mambo mengine mengi sana yaliyo ya hovyo. Zambia wamefanya vyema kwa kuandaa Mpango mzuri wa kuwaepuka Watu wa hovyo ili Watu hao wa hovyo waweze kujifunza ustaarabu.

Hili litakuwa fundisho zuri sana kwa wahusika
 
Suala la kutafuta amani ya DRC kwa gharama zetu sahau kabisa mkuu, kifupi HATUWEZI LIMETUDHIDI KIMO.
 
Tutakuja kushituka hizo Bandari zimesalia kuhudumia Mikoa yetu pekee,washindani Wetu wamechukua keki.

Lazima tuingie kufanya mambo ya umafia Kwa maslahi ya Nchi
Wewe unamawazo mazuri sana,ila ccm wanamawazo ya kuiba na kufisadi mali za umma,hii nchi ili ipone ni kuondoa ccm madarakani tofauti na hapo hakuna la maana litakalofanyika.
 
Tatizo la Viongozi wetu mda mwingi wamewekeza kwenye siasa kila kitu,kuwaruhusu watu wenye akili ndogo ndiyo wabebe maono ya inchi hii yaani chawa, huku wakiwaacha wenye akili kubwa ilimradi tu wanapingana nao kisiasa
 
Malawi hawana hela wala uwezo wa kujengs reli hata kilomita 20

Pili kuna tishio la vita Mozambique la magaidi ni mwehu pekee aweza Ingia kichwa kichwa kuchukua bandari Mozambique
Vita inadhibitiwa,pesa zinakopwa kuna rafiki china atawajengea.

Acheni kujifariji dp world wameharibu uchumi wa nchi,mataifa yanaikimbia bandar ya DSM
 
Tuna hitaji kuanza na viwanda vidogo vya uzalishaji kwa bidhaa za ukanda wetu hasa malighafi Afrika tuna import sababu hatuna uwezo wa kuzigeuza malighafi kuwa bidhaa za mwanzo za uchakataji Tanzania tutumie huu mwanya.

Kwa namna hiyo itaweza chochea sekta ya uchukuzi. Tuchape kazi na iwe kazi kweli kuliko mabishano ya mpira, matamasha ya mziki stareh3 zisizo na tija, Tanzania inatakiwa tuingie kwenye sera ya viwanda na teknolojia hata ya awali na kati tuu tukisema tuendelee kuagiza tena tutadidimia. Faida ya uzalishaji wa ndani ni kubwa kuliko kuagiza.
 
Umasikini wakati kuna mikopo au hapa tz miradi mikubwa yote tumejenga kwa hela za kwenye mkoba wa samia?

Acha kujitoa akili
 
Zile sababu zilizozifanya nchi hizo ziwe tegemezi kwa Tanzania kwenye bandari kwa sasa zilishatoweka; hazipo tena.

Sababu#1: Kipindi hiko huko inakopita barabara kwa mujibu wa ramani aliyoweka mleta mada ChoiceVariable ukanda wore huo ndiko "waasi" wa RENAMO walikokuwa wametamalaki. Kusingepitika! Dar Port favored.

Sababu #2: Route mpya ya Lubumbashi - Lobito, Angola; mnakumbuka habari za "waasi" wa UNITA chini ya "gaidi" Dk. Jonas Savimbi? Basi hiyo route ndio ilikuwa HQ ya Savimbi na genge lake; kisingepita kitu - Dar Port favored!

Sababu #3: Route ya South Africa. Mnakumbuka enzi za ubaguzi wa rangi huko SA? Mnakumbuka harakati za Uhuru kule Namibia chini ya SWAPO? Mnajua nchi zote za Kusini mwa Afrika except "kibaraka mmoja" zilikuwa against uta wala wa makaburu kule SA na Namibia? Nchi hizo hakukupitika kabisa! Dar Port favored!

Ni sababu hizo zilizoi-favor bandari ya Dar es Salaam automatically! Kama hatukutumia fursa vizuri kipindi kile, badala yake wakawekwa mchwa ambao kazi yao ilikuwa kutafuna bila kuangalia kesho hizo fursa kwa sasa hazipo tena. Inabidi kutumia akili na sio "kuletewa mezani".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…