Msururu wa magari ya msafara wa Rais wa nchi moja masikini

Msururu wa magari ya msafara wa Rais wa nchi moja masikini

Showmax

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2022
Posts
6,592
Reaction score
12,707
Huu ni msafara wa raisi wa nchi ya Equatorial Guinea moja ya nchi masikini Afrika, ambayo ni sawa na mali binafsi ya dictator Nguema wakila matunda ya UHURU huku wananchi wake wakitopea kwenye umasikini.

Screenshot_20230320_184210.jpg
Screenshot_20230320_113238.jpg
 
Daah Mjapani katakana hapo harafu baadae wanatoa msaada kiduchu wa kujenga bara bara aisee Nchi za Afrika ni kiboko msafara wote huo wa nini?

Huku Wananchi wake wakipata tabu tuu hakuna huduma bora za afya,Elimu,umeme wala maji...
 
hapo unaweze kuta wanakwenda kuzindua mradi wa maji ambao ni msaada au mkopo kutoka kwa beberu huku gharama ya mafuta ya hayo magari inaweza kabisa kukamilisha huo mradi.
 
Lakini putin yeye ndo anakanyaga gia, bado tunasafari ndefu sanaaa. Hivi huu utaratibu wa kutembea na msafara mkubwa nani aliuanzisha 🤔🤔🤔
 
Lakini putin yeye ndo anakanyaga gia, bado tunasafari ndefu sanaaa. Hivi huu utaratibu wa kutembea na msafara mkubwa nani aliuanzisha [emoji848][emoji848][emoji848]
Dogo Putin anazingua sana Ulimwengu. Namfananisha na Faisal kwenye soka la bongo
 
Trump akisema shithole countries inabidi tutawaliwe tunakuwa wakali kama mbogo!
 
Dogo Putin anazingua sana Ulimwengu. Namfananisha na Faisal kwenye soka la bongo
Hamna mkuu, me naona Putin anataka kuleta usawa, yaani kusiwepo na kiranja wa dunia.Maana inavyosadikika USA ananyonya baadhi ya nchi hasahasa nchi za kiarabu na Africa
 
Bado sijaona tofauti ya huo msafara na msafara wa Magufuli hususani akiwa kwenye ziara mikoani. Kwa hilo, huyo rais na Magufuli ni ndugu wa mbwembwe za misafara.

Kwa mfano, kwa wastani msafara wa Magufuli ulikuwa na vitu vifuatavyo.
-Magari ya hadhi ya VX yasiyopungua 50
-Ambulance za kisasa 2
-'Jammer' 2
-Helikopta za kisasa za kiusalama 2
 
Back
Top Bottom