PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 459
- 644
Mkazi wa Mtaa wa Isengo, Kata ya Iyela jijini Mbeya, Enelesta Pili, amepokea zawadi ya shilingi milioni moja kutoka kwa Dkt. Tulia Ackson baada ya mjukuu wake kuchapisha mtandaoni video ikimuonyesha akisuka mkeka wenye jina la Dkt. Tulia.
Enelesta amesema aliamua kuandika jina la Dkt. Tulia kwenye mkeka huo kutokana na kuvutiwa na kazi anazozifanya za kuwahudumia wananchi na kuchochea maendeleo katika jamii.
Kwa upande wake, mjukuu wake Getruda Kassim amesema alichapisha video hiyo mitandaoni kwa lengo la kutangaza kazi za bibi yake ili zipate soko na kuongeza mauzo ya bidhaa anazotengeneza.
Akizungumza baada ya kumtembelea Enelesta nyumbani kwake, Dkt. Tulia Ackson amemshukuru kwa ubunifu wa kuandika jina lake kwenye mkeka na kumkabidhi zawadi ya shilingi milioni moja. Pia alimpongeza kwa kutumia ususi wa mikeka kuhamasisha utunzaji wa mazingira na kuwataka wananchi kuendelea kutumia vipaji vyao kujiongezea kipato na kuchangia maendeleo ya jamii.