Msuva hana muda mrefu atarejea Nyumbani

Christopher Wallace

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2015
Posts
1,479
Reaction score
3,788
Wakuu huu ni ukweli na ukweli lazma usemwe, Winga machachari wa Yanga na Taifa Stars anakwea pipa kwenda kucheza soka huko nchini Morocco. Sioni ni jinsi gani Msuva anaweza akumudu kumaliza miezi 6 nje ya Tanzania, kwa style yake ya soka na nilivyomshuhudia kwenye michuano ya Cosafa ni wazi kuwa, dirisha dogo la usajili lijalo Msuva atakuwa amerudi zake Bongo tayari kabisa kumwaga wino wake wa kuendelea kukipiga aidha Yanga au Simba.

Najua povu litawatoka ila huo ndio ukweli na mimi ni mjumbe na siku zote mjumbe hauwawi.

Nawasilisha...
 
usimuhukumu kwa cosafa,mwalimu hakuweza kuunganisha rasilimali watu uwanjani hivyo ufanisi ulikuwa mdogo,hakuna mchezaj aliye-peform
 

Huwatakii mema wenzio.
 
Ukijiona una wivu wa namna hii alafu wewe wa kiume basi jua kua makosa yalifanyika wakati wa uumbaji ulitakiwa uwe upande wa pili.
 
Mbona Watanzania tuna roho za chuki kiasi hiki,ebu tumuache msuva akajaribu bahati yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tuachage ushabiki maandazi kwenye mambo ya msingi. mimi ni simba damu lakini nimefurahi kuona msuva anapata timu nje ya nchi. na kwa muonekano tu msuva anaonekana ni mpambanaji na yupo makini ukimlinganisha na akina boban, tegete na ngasa. hawa watatu walifanya uzembe wa kuendekeza simba na yanga wakaacha ulaji nje wakarudi kuwafurahisha viongozi wa simba na yanga matokeo yake wachezaji wa nchi nyingine waliowaacha nje wanaanza kuingia ligi kubwa kama EPL, LA LIGA wao huku wanaitwa veterani wakiwa bado wadogo na muda si mrefu ndo ndo itawahusu. msuva nenda kapambane ili uwe mfano kwa wachezaji wengine wanaokuwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…