Wazee
Niliutazama mjadala tangu mwanzo hadi mwisho. Niseme machache:
-Kwanza, nilishangaa kwa nini mjadala huo uliletwa na kamati ya Lubeleje badala ya kamati ya Masilingi inayohusika na mambo ya usalama na mambo ya nje. Uvumi ni kuwa serikali inamwona Lubeleje kuwa ni uchochoro wa kupitishia mambo yenye utata, na yeye huyachukulia kama msahafu.
-Dhana ya kupunguza madaraka ya Rais ni nzuri lakini si katika mambo ya ulinzi na usalama. Muswada ulikosea kuweka dhana ya kupiga kura katika baraza linalopendekezwa, kwa sababu, idadi ya baraza ni ndogo inayoweza kununuliwa na kuinfluence maamuzi.
-Ni wazi, Sophia, Werema na Lubeleje wameonyesha kukosa umakini, si katika hoja, bali hata katika drafting na kukosekana kwa sensitivity. Of course hili pia ni pigo kwa idara nzima ya usalama, kwamba waliacha kitu kama hiki kiende mbele. Ni aibu kwa baraza la mawaziri lililopitisha muswada huu uende bungeni.
Mwisho naomba kuwauliza wanasheria: Hivi hakuna constitutional implications za kukataliwa kwa muswada bungeni? Hii si dalili ya kukosa imani na Rais?