Unagundua ,wale uliokuwa unawaita kina anko na baba wadogo enzi ukiwa mtoto ndiyo umekuwa wewe sasa kwa machalii/ma ankoli.
Mbaya zaidi wale kina anko na baba wadogo ambao ulikuwa unawaomba Hela ya kalamu na daftari kwa ajili ya matumizi ya shule alafu walikujibu hawana au watakupa siku nyingine kisha ukawaona wakuda na kuwasemea kwa mama yako.
Wale kina anko na wajomba waliokuwa wanakuja kusalimia kwenu miss ya jioni kisha wanaambiwa na mama yako wasiondoke hadi wale,wewe ukawaona kama wakuda wanamaliza msosi wenu.
Hao jamaa wote Leo ndiyo umegeuka wewe sasa.
Ukiona simu za wajomba na watoto wa dada unasonya n kusema " Hawa wapuuzi wanadhani Hela zinaokotwa tu Huku mjini".
Mungu atuhurumie wanaume.
Maisha yetu,wazazi wetu,watoto wetu,wanawake na ndugu zetu,wote hao maisha yao yanatutegemea sisi tuokoe jahazi na mbaya zaidi ramani zimepotea tunakwenda bila dira. Tunasubiri kudura ya Mungu tu kutunusuru!!
Mkuu pole sana. siku yako inakuja.