Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Ndugu yangu mmoja kasoma taazia niliyomwandikia Dr. Mayanja Kiwanuka (Ahmed Kiwanuka) na baada ya kusoma akaniletea picha ya kibao cha Mtaa wa Kiwanuka ulioko Upanga na akanieleza kuwa Mtaa wa Kiwanuka uko karibu na Barabara ya Mataka.
Hapo hapo nikamwandikia kumuomba aniletee picha ya kibao cha Barabara ya Mataka.
Akaniletea majibu kuwa kibao cha Barabara ya Mataka hakipo nitosheke na nyumba ambazo jina la mtaa limeandikwa.
Naamini wengi hamjui historia ya Chief Mataka.
Huyu Chief Mataka alipigana na Wajerumani na ni katika mashujaa walionyongwa na kuzikwa katika kaburi la halaiki.
Nimeingia Maktaba nimechomoa kitabu cha Abdul Sykes nimekwenda kwenya faharasha kutafuta jina hili la Mataka.
Nimemkuta kama nilivyotegemea.
Nakuwekea hapa uisome historia ya shujaa huyu wa Vita Vya Maji Maji kama nilivyomweleza katika kitabu hicho:
Chifu Songea bin Ruuf wakati alikuwa akikusanya nguvu za raia wake dhidi ya majeshi ya Wajerumani na huku akijaribu kupata ushirika wa machifu wengine katika sehemu za kusini ya Tanganyika na ng’ambo ya Mto Ruvuma katika Msumbiji akiwaandikia barua machifu wenzake kutafuta msaada.
Barua hii aliyomwandikia Sheikh, Sultan Mataka bin Hamin Massaninga inasema:
‘’Kwa Sheikh Sultan Mataka bin Hamin Massaninga.
Asalaam Aleikum,
Ninakuletea barua kupitia Kazembe.
Tumepata amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu kuwa Wazungu lazima waondoke nchini.
Tupo katika kupigananao hapa.
Naamini tumeshapatana muda mrefu, (kwa hiyo) niletee wanao, ili tufanye ushirikiano.
Nilitaka kukuletea mifugo kama zawadi, lakini sipo katika hali ya kuweza kufanya hivyo, kwa kuwa vita ambavyo Mwenyezi Mungu amevitaka vinaendelea.
Niletee watumiaji bunduki mia moja, na niunge mkono katika kulivamia Boma (Songea).
Ninakuletea chupa ya Mtume Muhammad, ambayo ndani yake ipo nguvu ya kuwashinda Wazungu.
Usiwe na shaka nayo, ina uwezo mkubwa.
Tutakapoliteka Boma (Songea), tutakwenda kwenye vituo katika Nyasa pamoja, mimi na wewe.
Hivi sasa tusahau ugomvi wetu wa zamani.
Chupa hii, na daíwa, imeletwa na Chinyalanyala mwenyewe, kiongozi wa vita.
Ameleta vilevile kombe, na anakupa salamu nyingi.
Endapo watu wako watakuja, Chinyalanyala mwenyewe atafika na atakupa vitu vingi vilivyo vitukufu.
Hassan bin Ismail anakusalimu.
Salam nyingi,
Sultan Songea bin Ruuf.’’
Mwalimu Hussein Bashir mwandishi wa vitabu kadhaa vyenye kusahishisha historia ya Zanzibar, Kilwa na kwengineko yeye katika utafiti wake wa Vita Vya Maji Maji alikwenda Liwale na alikutana na kitukuu cha Chinyalanyala anaitwa Omar Njala kifupisho cha Kinyalanyala
Omar Njala alimweleza mengi ya babu yake mkuu na kumfahamisha kuwa Bi Khadija Mkomanile anakuwa bibi yake.
Khadija Mkomanile ndiye kamanda pekee katika Vita Vya Maji Maji na alinyongwa na Wajerumani na amezikwa katika lile kaburi la halaiki pale Songea kwenye Makumbusho ya Maji Maji.
Askofu kutoka Misheni ya Peramiho aliyeletwa kuwabatiza mashujaa hawa kabla ya kunyongwa jina lake Yohannes Hafligger alimpa jina jipya Khadija Mkomanile.
Alimpa jina la Yacintha.
Nduna Abduraufu Songea Mbano mwandishi wa barua kwa Chief Mataka bin Hamin Massaninga