KERO Responded Mtaa wa Igalula - Sengerema tunasotea umeme, tunazungushwa na TANESCO miezi 10 sasa

KERO Responded Mtaa wa Igalula - Sengerema tunasotea umeme, tunazungushwa na TANESCO miezi 10 sasa

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Nimeona fursa ya kufanya shughuli za biashara katika eneo la Igalula, Sengerema, hasa kutokana na uwepo wa shughuli za Nyanzaga Mining, hivyo nikafungua Pub kwa lengo la kujiajiri na kuendesha biashara yangu.

Hata hivyo, kwa takribani miezi 10 sasa, TANESCO bado hawajafanikiwa kuufikisha umeme katika Mtaa wa Igalula, jambo ambalo limekuwa changamoto kubwa kwangu na kwa wakazi pamoja na wafanyabiashara wengine katika eneo hilo.

Suala hili lifike katika mamlaka husika ilitupate ufumbuzi, hiyo changamoto imekuwa ikituumiza wengi na kuturudisha nyuma kiuchumi.


Pia soma...

 
Habari, Ndugu Mteja, na pole sana kwa changamoto hii.

Kwa upande wetu, tumepokea taarifa yako na tunaifanyia ufuatiliaji wa kina kuhusu suala hili. Tutakurejea hivi karibuni kwa mrejesho, majibu na mwongozo stahiki mara baada ya kukamilisha ufuatiliaji.

Tunashukuru kwa uvumilivu, uelewa na ushirikiano wako.

Asante! ^GK
 
Nimeona fursa ya kufanya shughuli za biashara katika eneo la Igalula, Sengerema, hasa kutokana na uwepo wa shughuli za Nyanzaga Mining, hivyo nikafungua Pub kwa lengo la kujiajiri na kuendesha biashara yangu.

Hata hivyo, kwa takribani miezi 10 sasa, TANESCO bado hawajafanikiwa kuufikisha umeme katika Mtaa wa Igalula, jambo ambalo limekuwa changamoto kubwa kwangu na kwa wakazi pamoja na wafanyabiashara wengine katika eneo hilo.

Suala hili lifike katika mamlaka husika ilitupate ufumbuzi, hiyo changamoto imekuwa ikituumiza wengi na kuturudisha nyuma kiuchumi.


Pia soma...
Habari, Ndugu Mteja.

Tunashukuru kwa uvumilivu wako wa kutupa muda kufanya ufuatiliaji juu ya swala lako.

Tafadhali fahamu kuwa eneo la Igalula ni eneo jipya ambalo hivi karibuni limetengwa kwa ajili ya shughuli za uchimbaji. Kwa mujibu wa taarifa zilizopokelewa, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Sengerema ilifanya kikao na wananchi katika eneo hilo tarehe 23 Septemba 2026, kwa lengo la kubaini changamoto au malalamiko yanayohusu huduma. Hata hivyo, hakuna malalamiko yaliyowasilishwa wakati wa kikao hicho.

Aidha, hadi sasa ofisi yetu haijapokea taarifa ya maombi ya huduma kutoka kwa mteja katika eneo hilo ambayo hayajapatiwa huduma.

Iwapo bado hujahudumiwa au una changamoto katika kupata huduma, tunaomba upige simu kupitia namba ya huduma kwa wateja 180, bila malipo, au ufike katika Ofisi ya TANESCO Wilaya ya Sengerema kwa ajili ya kutoa taarifa na kufanyiwa ufuatiliaji na msaada stahiki.

Asante! ^FL​
 
Back
Top Bottom