KERO Mtaa wa Kambarage, Shinyanga mjini taka zimeturundikia zaidi ya wiki tatu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mkazi wa Mtaa wa Kambarage, Manispaa ya Shinyanga. Ninaomba kufikisha kilio chetu kuhusu hali mbaya ya usafi ambayo imekuwa ikitusumbua kwa muda sasa kutokana na mrundikano wa taka.

Tunachofahamu ni kwamba kumekuwa na mgogoro kati ya Manispaa ya Shinyanga na kampuni binafsi iliyokuwa ikihusika na ukusanyaji wa taka. Tunaambiwa kampuni hiyo imesimamisha huduma kwa sababu haijalipwa fedha za kuendesha shughuli hizo, ikiwemo gharama za mafuta. Jina la kampuni bado ninalifuatilia ili nilipate.

Kutokana na hali hiyo, taka zimejaa maeneo mengi ya mji, hasa katika Soko la Kambarage. Hapa kwetu taka hazijazolewa kwa zaidi ya wiki tatu, jambo ambalo limesababisha harufu kali, kuongezeka kwa nzi na kuhatarisha afya za wananchi pamoja na wafanyabiashara.

Cha kusikitisha zaidi ni kwamba tatizo hili si la leo. Kwa muda mrefu soko letu halijawahi kuwa na eneo rasmi la kutupia taka. Uchafu wa soko umekuwa ukitupwa katikati ya makazi ya watu, karibu na biashara na hata ofisi mbalimbali. Licha ya wananchi kulalamika mara kadhaa, bado tatizo halijapatiwa ufumbuzi wa kudumu.

Awali taka zilikuwa zikitupwa upande mwingine wa soko, lakini baada ya mgogoro huo zikaanza kumwagwa katika eneo lililo mbele ya makazi ya wananchi na katikati ya barabara. Wakati wanahamishia taka hapo tuliambiwa kutakuwa na watu maalumu wa kuziondoa mara kwa mara, lakini hali imekuwa tofauti kabisa.

Kwa kawaida gari la kuzolea taka lilikuwa likifika angalau mara moja kwa wiki, lakini sasa zimepita zaidi ya wiki tatu bila taka hizo kuondolewa. Tunaendelea kuishi na kufanya biashara karibu na mlundikano wa taka, hali ambayo ni hatari kwa afya na mazingira.

Ninaomba Manispaa ya Shinyanga na mamlaka zote husika ziingilie kati haraka kutatua mgogoro uliopo na kuhakikisha huduma ya ukusanyaji wa taka inarejea kama kawaida. Pia tunaomba kupatikane suluhisho la kudumu kwa kuweka eneo rasmi la kutupia taka ili wananchi tusiendelee kuishi katika mazingira haya yasiyofaa.
 
Screenshot_20260514-220817~2.png
 
Back
Top Bottom