KERO Responded Mtaa wa Malabi - Tabora tunateseka na umeme, unakatika Siku 5 kati ya 7 za wiki

KERO Responded Mtaa wa Malabi - Tabora tunateseka na umeme, unakatika Siku 5 kati ya 7 za wiki

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Natokea Tabora Manispaa, Kata ya Mpera, Mtaa wa Malabi.. Tumekuwa na shida ya umeme ya muda mrefu ambayo haipatiwi ufumbuzi.

WhatsApp Image 2026-05-04 at 15.37.18.jpeg

WhatsApp Image 2026-05-04 at 15.37.17 (2).jpeg

WhatsApp Image 2026-05-04 at 15.37.17 (1).jpeg
Ndani ya siku 7 za week kuna siku 4 hadi 5 lazima tuwe hatuna umeme, tumejaribu kuwasiliana na Huduma kwa Wateja TANESCO mambo yanakuwa yaleyale tu.

Soma Pia: Wiki ya pili Sasa Jimbo la Kivule Mtaa wa Bombambili umeme unakatwa kila siku asubuhi na kurudishwa saa nane usiku

Tumejenga apartments huo mtaa kujikwamua na hali ya maisha lakini kinachotuumiza zaidi ni kuwa wapangaji mara kwa mara wameku wakihama na kuleta usumbufu.

Mtaa wetu upo takribani Kilometa 2 kutoka Makao Mkauu ya TANESCO, kuna kiongozi wetu alifuatilia TANESCO akajibiwa kuwa kuna umeme mdogo (low voltage) lakini hali hiyo idumu kwa zaidi ya miaka mitatu?
WhatsApp Image 2026-05-04 at 15.37.18 (1).jpeg

MAJIBU YA TANESCO 👇🏽
 
Natokea Tabora Manispaa, Kata ya Mpera, Mtaa wa Malabi.. Tumekuwa na shida ya umeme ya muda mrefu ambayo haipatiwi ufumbuzi.

Ndani ya siku 7 za week kuna siku 4 hadi 5 lazima tuwe hatuna umeme, tumejaribu kuwasiliana na Huduma kwa Wateja TANESCO mambo yanakuwa yaleyale tu.

Soma Pia: Wiki ya pili Sasa Jimbo la Kivule Mtaa wa Bombambili umeme unakatwa kila siku asubuhi na kurudishwa saa nane usiku

Tumejenga apartments huo mtaa kujikwamua na hali ya maisha lakini kinachotuumiza zaidi ni kuwa wapangaji mara kwa mara wameku wakihama na kuleta usumbufu.

Mtaa wetu upo takribani Kilometa 2 kutoka Makao Mkauu ya TANESCO, kuna kiongozi wetu alifuatilia TANESCO akajibiwa kuwa kuna umeme mdogo (low voltage) lakini hali hiyo idumu kwa zaidi ya miaka mitatu?
Habari, ndugu mteja.

Kwanza, tunaomba radhi kwa kuchelewa kukujibu. Tulipata changamoto ya muda kwenye akaunti yetu, lakini kwa sasa tatizo hilo limetatuliwa.

Pole sana kwa changamoto ya umeme uliyoipitia. Ingawa muda umepita tangu ulipotutumia ujumbe wako, tunaomba nafasi ya kufanya ufuatiliaji wa hali ya huduma katika eneo lako ili kubaini kilichosababisha changamoto hiyo na hali ilivyo kwa sasa.

Tunaomba uvumilivu wako kwa muda mfupi wakati tunakamilisha ufuatiliaji huo. Tutakurejea mara tu tutakapopata mrejesho kamili.

Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza na tunakushukuru kwa uvumilivu na ushirikiano wako.

Asante. ^FL
 
Habari, Ndugu Mteja.

Tunashukuru kwa uvumilivu wako. Tumefanya ufuatiliaji kuhusu suala lako na kubaini kuwa kwa sasa mita ya Malabi ilishafanyiwa kazi, na hakuna changamoto iliyoripotiwa kwa wakati huu.

Hata hivyo, ikiwa bado unaendelea kukutana na changamoto yoyote, tafadhali tujulishe ili tuweze kufanya ufuatiliaji wa kina zaidi na kuchukua hatua stahiki.

Tunaomba tena radhi kwa kuchelewa kukupatia mrejesho. Kwa sasa, akaunti yetu iko katika hali nzuri, hivyo endapo utakuwa na changamoto yoyote kuhusu huduma zetu au una maoni, usisite kuwasiliana nasi kupitia ukurasa huu au kupiga simu kupitia namba yetu ya huduma kwa wateja "180," bila malipo.

Asante kwa uvumilivu na ushirikiano wako. Karibu sana! ^FL
 
Back
Top Bottom