Ukweli ni kuwa Mtaa wa
Mshute Kiyate haupo kwa sababu wahusika wamekataa kubadili kibao cha jina sasa yapata zaidi ya miaka 20.
Kitwana Kondo alipokuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam ndiye aliyefanya mabadiliko ya majina ya mitaa kuwaenzi wazalendo waliopigania uhuru wa Tanganyika kwa kuipa majna yao ile mitaa waliokuwa wakiishi.
Hivyo ndivyo Mtaa wa Kipata ujabadilishwa na kuitwa
Mtaa wa Kleist Sykes, Mtaa wa Somali ukaitwa
Omari Londo, Mtaa wa Aggrey ukaitwa
Max Mbwana, Pugu Road ikaitwa Barabara ya
Mwalimu Nyerere, Bi. Tatu binti Mzee akapata mtaa Ilala na Mtaa wa Tandamti ukabadilishwa jina na kuitwa Mtaa wa
Mshume Kiyate.
Lakini palizuka malalamiko kuwa kilichomsukuka
Kitwana Kondo kubadili majina ni hisia za udini. Hii ni baada ya kuonekana wazalendo wengi waliopewa majina ya mitaa ni Waislam.
Magazeti yakahoji ni michango gani wazalendo hawa walitoa?
Kitwana Kondo katika mahojiano aliyofanya na marehemu
Sarah Dumba wa Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) alijibu kwa kusema, ''Ikiwa hamjui michango ya watu hawa ulizeni mtaelezwa.''
Kushoto:
Mwinjuma Mwinyikambi, Max Mbwana Julius Nyerere
na
Mshume Kiyate Uchaguzi Mkuu wa 1962
Mtaa wa
Mshume Kiyate katika mihangaiko ya kutafuta rizki nyakati za
mchana wakati wa kutafuta rizki
Mtaa wa
Mshume Kiyate karibu na Soko la Kariakoo kama unavyoonekana
hivi sasa