Mkuu naona kama unakwepa kwepa kujibu au kuchangia chochote cha faizafoxy why au ndo mfungo unakataza ok basi naomba utupe hyo ya maasi aliyouliza mkuuMaalim Mohamed Said,
Tafadhali tupe darsa kuhusu hayo maasi ya tarehe 20, nnadhani vijana wengi humu hawajapatapo hata kuyasikia.
Kambaresharubu,
Sikuwa najua kuwa Mtaa wa Pemba ulipewa jina la Mwalimu
Sakina.
Ahsante sana kwa taarifa hii.
Capt Tamar,Jomo kenyata ndiye anayetambulika kama aliyefanikisha uhuru wa kenya,Tanzania ni nyerere! Japo hawakuwa. Peke yao ila hao ndio main character!! Kwa sababu kimsingi karibu kila mwananchi mtanzania wa wakati huo Ali play some part kuupigania uhuru!! Na hata kwenye hiyo mnayoita kuwa ni Historia iliyopotoshwa majina ya hao wazee wenu waislam yapo mengi tu!! Ila hilo jina moja kubwa la (khafir)ndilo mmeligeuzia silaha zenu baada ya mkoloni kuondoka!! Uhuru wenyewe mmeupata bure tu lakini kelele nyiiiiiingi!! Hao kina kiyate waliwahi hata kumchapa mkoloni bakora moja? Au walimwondoa mkoloni kwa zogo na bao? Nyerere ndiye aliyekuwa msomi miongoni mwao,na Ndiyo maana hao Wazee wenu walimpa heshima yote aliyoistahili,kwa sababu walijua vita ile haikuwa ya bakora na mikuki!! Bali akili,na mwenye akili alikuwepo,na alitumika ili kufikia lengo,na lengo lilifikiwa!! Kizuri zaidi wazee wenu waliendelea kumheshimu kijana wao hata baada ya uhuru!! Kwa sababu waliitambua kazi kubwa aliyoifanya kijana wao huyo! Japo hakuwa mwislam.
"Sifuatilii sana hoja zako ila chache nilizofuatilia ....."Sifuatilia sana hoja zako ila chache nilizofuatilia lazima kuwe na chembechembe za dini ndani yake........ila shukrani kwa taarifa, natumai wahusika watabadili hilo jina.
Magari7,Mzee, naomba kujua kuhusu hio mizinga aliyoisema faizafoxy
Halafu utakuja mijitu imezaliwa 1990 hapa inaanza kupinga utadhan walikuwepo miaka ya 1960.Dar ndiyo kilikuwa kitovu Cha kupigania uhuru na siyo kagera au songea. Mzee Mohammed Said Yuko sahihi. Historia inakawaida ya kupotoshwa Sana na ndiyo maana mwenye akili shuleni hushauriwa kusoma science na siyo art
Sent using Jamii Forums mobile app
Boniphace...Mwalimu Nyerere ndiye aliyeleta Uhuru wa Tanganyika.
Mkuu naomba unitumie picha ya Omary Londo kama unayoBoniphace...
Hakuna anaeweza kudogosha historia ya Mwalimu Nyerere katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.
Mjadala hajapatapo kuwa katika hili.
Mjadala siku zote umekuwa katika historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika.
Iweje iandikwe historia ya TANU Abdul Sykes jina lake lisiwepo?
Naamini unaijua historia ya Sykes katika siasa za kikoloni Tanganyika.
Naamini unajua historia ya Sheikh Hassan bin Ameir katika TANU.
Haya majina hayakuwapo pamoja na jina la Nyerere katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.
View attachment 1295297
Kushoto Iddi Faiz Mafungo Mwekahazina wa TANU na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika, Sheikh Mohamed Ramia, Julius Nyerere, Saadan Abdu Kandoro na Haruna Taratibu, Dodoma train station 1955
Haya ni machache lakini wazalendo wengi historia iliwasahau.
Ubarikiwe sana SheikhView attachment 1295485
Aliyekaa mbele anatabasamu ni Omari Londo na nyuma yake ni Abdallah
Kassim Hanga na juu ya jukwaa ni Julius Nyerere
Vitabu bei gani?Ukweli ni kuwa Mtaa wa Mshute Kiyate haupo kwa sababu wahusika wamekataa kubadili kibao cha jina sasa yapata zaidi ya miaka 20.
Kitwana Kondo alipokuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam ndiye aliyefanya mabadiliko ya majina ya mitaa kuwaenzi wazalendo waliopigania uhuru wa Tanganyika kwa kuipa majna yao ile mitaa waliokuwa wakiishi.
Hivyo ndivyo Mtaa wa Kipata ujabadilishwa na kuitwa Mtaa wa Kleist Sykes, Mtaa wa Somali ukaitwa Omari Londo, Mtaa wa Aggrey ukaitwa Max Mbwana, Pugu Road ikaitwa Barabara ya Mwalimu Nyerere, Bi. Tatu binti Mzee akapata mtaa Ilala na Mtaa wa Tandamti ukabadilishwa jina na kuitwa Mtaa wa Mshume Kiyate.
Lakini palizuka malalamiko kuwa kilichomsukuka Kitwana Kondo kubadili majina ni hisia za udini. Hii ni baada ya kuonekana wazalendo wengi waliopewa majina ya mitaa ni Waislam.
Magazeti yakahoji ni michango gani wazalendo hawa walitoa? Kitwana Kondo katika mahojiano aliyofanya na marehemu Sarah Dumba wa Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) alijibu kwa kusema, ''Ikiwa hamjui michango ya watu hawa ulizeni mtaelezwa.''
Kushoto: Mwinjuma Mwinyikambi, Max Mbwana Julius Nyerere
na Mshume Kiyate Uchaguzi Mkuu wa 1962
Mtaa wa Mshume Kiyate katika mihangaiko ya kutafuta rizki nyakati za
mchana wakati wa kutafuta rizki
Mtaa wa Mshume Kiyate karibu na Soko la Kariakoo kama unavyoonekana
hivi sasa