Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
MTAA WA MUHIDIN MFAUME KIMARIO KINONDONI MOSCOW
Leo nikiwa na ndugu yangu mwanahistoria na maktaba inayotembea Hamisi Hababi tumekutana na kibao cha Mtaa wa Kimario Kinondoni Moscow tukaamua kukipiga picha kibao hicho.
Hakika inafurahisha kukuta kumbukumbu kama hizi za wazalendo walioipigania Tanzania katika hali na nyadhifa zao iwe wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika au baadae katika Tanganyika huru.
Muhidin Kimario alifikia ngazi ya Major General katika Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Muhidin Kimario nyumbani kwao Moshi, Mtaa wa Chini kulikuwa na Zawia ya Tariqa Quadirriyya ambayo ipo hadi leo na unaweza kusema inakimbilia miaka 100 sasa.
Nikiwa mtoto mdogo namkumbuka Muhidin Kimario akiwa mwalimu Muslim School Moshi pamoja na walimu wengine ambae ninaemkumbuka ni Mwalimu Badi ambae alikuwa ndiye mwalimu akisomesha Qur'an katika shule hiyo.
Miaka mingi baadae sasa mimi mtu mzima nilikutana na Mwalimu Badi jirani ya Msikiti wa Raidha na nikamkumbuka lakini yeye hakunikumbuka hata kidogo.
Mimi nilikuwa nasoma Stanley Primary School jirani sana na Muslim School na vipindi vya dini shule yetu ingawa ilikuwa ya Walutheri wanafunzi Waislam walikuwa wanaruhusiwa kwenda Muslim School kuhudhuria vipindi vya dini wakisoma darasa moja na wanafunzi wa Muslim School.
Mwalimu wetu wa dini alikuwa Mwalimu Badi.
Picha hiyo hapo chini inamuonyesha Muhidi Kimario akiwa mtoto mdogo hajafika hata miaka 10 amekaa chini ya miguu wa masheikh wake.
Picha nyingine inamuonyesha Muhidin Kimario katika ujana wake na picha ya mwisho akiwa katika mavazi yake ya Brigadier General.
Brigadier Muhidin Kimario alipata kunidokeza kuwa alikuwa anaandika historia ya maisha yake na akasema kuwa ikikamilika angependa In Shaa Allah niitupie jicho.
Hatukuonana tena baada ya siku ile.
Allah amrehemu na amweke mahali pema peponi.