Mtaa wa Muhidin Mfaume Kimario Kinondoni Moscow

Mtaa wa Muhidin Mfaume Kimario Kinondoni Moscow

Duh, huyu mrombo nani alimsilimisha?

Wachaga waislam wanapatikana:
-Masama ukanda wa kwa Sadala
-Lyamungo ambapo ni mpakani mwa Kibosho na Machame.
Upo very sensitive na mambo ya kiimani
 
Mshangao wa kwanza ni kuwa Kimario kumbe alikuwa Islam, okay.

Kweli nilisikia miaka ile kuwa jeshi letu lililemewa sana huko kwa nduli, japo ilikuwa siri kuu.

Kuhusu hilo alilokuambia kuwa anaandika historia yake hebu jaribu kufuatilia yawezekana makaratasi yakawepo.

Itakuwa nzuri kwenye makumbusho ya Taifa au hata hapa jf tu.
Kitabu kulizuiwa kwa sababu maalum

aliundiwa zengwe la kuchafuliwa akiwa Mkuu wa CDA Dodoma

Mkapa akagundua fitna ile akampa Nishani ya juu kabisa kwa utumishi uliotukuka

alikuwa hapendi unafiki

kuna Viongozi walikuwa wanamchimba chimba sana kwa fitna …akakutana nao Airport wakati wanamkaribisha Baba wa Taifa Mwl Nyerere Dodoma…alimshika Mkono Baba wa Taifa akiwa ame lineup akamvuta Mstaafu Nyerere nje ya mstari kwa mkono wa kushoto a yule Mh.kwa Mkono wa kulia akamuuliza …

Kimario alisoma Israel akitumia hati ya kusafiria ya Ghana
 
..Ni Meja Jenerali Muhidin Mfaume Kimario.

..Jina la kivita anaitwa " Kamanda Mbogo. "

..Kimario ndiye kamanda aliyeongoza mapigano ya Sembabule au the battle of Sembabule.

..Majeshi ya Tanzania yalikuwa ktk wakati mgumu sana.

..Hapo Sembabule kulikuwa karibu na yalipo makambi ya Tiger Regiment ya Uganda.

..Kulitokea mapigano makali kati ya vijana wetu wa Jwtz [ brigade # 205] na majeshi ya Amin.

..Vijana wetu wa Jwtz walikuwa ktk hatari ya kushindwa mapigano hayo, na wajuzi wa mambo ya kivita wanasema Tanzania angepigwa Sembabule, basi angeshindwa vita.

..Hali ktk uwanja wa mapambano ilikuwa tete mno kiasi cha kulazimisha Mkuu wa Jwtz, na kamanda wa divishen kutembelea uwanja wa mapambano kuhakiki kinachoendelea.

..Kutokana na askari wetu kukwama ilibidi aitwe Brigedia Muhidin Kimario kuongoza mapambano ya kuwakwamua vijana wetu. Kimario aliifanya kazi hiyo kwa weledi mkubwa na ushindi ukapatikana.

Kuna mzee jirani yetu kipindi nakaa huko vituka alikuwa hasikii vizuri nikauliza naambiwa lile kombora lilidondosha ndege huko uganda kipindi hicho ni huyo mzee aliidungua mpaka sasa ana ugonjwa wa kutokusikia
 
Mie nilijua Chang'ombe quaters waliishi civil servants, kumbe hata wanajeshi walikuwemo?

Anyway, nilikuwa bado mdogo sana kuyajua mengi.
Ni kweli, wanajeshi wengi tu waliishi Chang'ombe Govt houses miaka ya zamani, hasa senior officers!
Sisi tumekaa hspo toka 1967.
 
Back
Top Bottom