KERO Responded Mtaa wa Nala - Dodoma tuna umeme mdogo, unakatika kila usiku, kwani Mradi wa JNHPP si umekamilika?

KERO Responded Mtaa wa Nala - Dodoma tuna umeme mdogo, unakatika kila usiku, kwani Mradi wa JNHPP si umekamilika?

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kero kubwa ya kukatika umeme na kuwa gizani ikifika Saa moja usiku, Mtaa wa NALA SHULE YA MSINGI hapa Dodoma, kila tukiuliza majibu ya wahusika ni kwamba umeme mdogo.

Je, huduma tunayolipia sisi kama wateja umeme kukata usiku ni sawa? Tunaomba serikali ichukue hatua maana majibu hayana ufafanuzi wa tatizo kwamba mchakato wa kuweka transforma unaendelea kitu ambacho bado tunapata Kero kubwa sana hasa kukatika umeme usiku.

Kwanini usikatike mchana ukatike usiku tu? Tunaomba TANESCO wajirekebishe kero hii waweke transformer wanalosema, kwani inadaiwa kuwa umeme ni mdogo, kwani si tuliambiwa mradi wa Bwawa la Umeme la Mwalimu Julius Nyerere (JNHPP) umekamilika na kama Nchi tunazalisha umeme kuliko hata ule ambao tunahitaji, sasa haya mambo ya umeme ni mdogo yanatoka wapi?

Wananchi tunateseka jamani.


UFAFANUZI WA TANESCO 👇🏽​
 
Mtu wa kwanza kumsikia analalamikia swala la Umeme Dodoma ama kweli NALA ni kijiji cha Bahi.

Dodoma haijawahi kuwa na shida ya umeme hata wakati kuna mgawo mkali nchini Malawi
 
Kwanini usumbufu wa umeme kukatika hovyo uwe ni mida ya usiku tu?

Magendo?
 
Kero kubwa ya kukatika umeme na kuwa gizani ikifika Saa moja usiku, Mtaa wa NALA SHULE YA MSINGI hapa Dodoma, kila tukiuliza majibu ya wahusika ni kwamba umeme mdogo.

Je, huduma tunayolipia sisi kama wateja umeme kukata usiku ni sawa? Tunaomba serikali ichukue hatua maana majibu hayana ufafanuzi wa tatizo kwamba mchakato wa kuweka transforma unaendelea kitu ambacho bado tunapata Kero kubwa sana hasa kukatika umeme usiku.

Kwanini usikatike mchana ukatike usiku tu? Tunaomba TANESCO wajirekebishe kero hii waweke transformer wanalosema, kwani inadaiwa kuwa umeme ni mdogo, kwani si tuliambiwa mradi wa Bwawa la Umeme la Mwalimu Julius Nyerere (JNHPP) umekamilika na kama Nchi tunazalisha umeme kuliko hata ule ambao tunahitaji, sasa haya mambo ya umeme ni mdogo yanatoka wapi?

Wananchi tunateseka jamani.
Habari, ndugu mteja.

Kwanza, tunaomba radhi kwa kuchelewa kukujibu kuhusu changamoto yako. Akaunti yetu ilikumbwa na changamoto kwa muda, lakini kwa sasa hali imerejea katika kawaida.

Pole sana kwa changamoto uliowasilisha. Licha ya muda kuwa umepita tangu ulipowasilisha taarifa hii, tumeipokea na tunaifanyia ufuatiliaji ili kufahamu hali yake na hatua zinazohitajika.

Tunaomba uvumilivu wako wakati tunakamilisha ufuatiliaji huo na tutakurejea mara tutakapopata mrejesho.

Asante. ^FL
 
Habari, Ndugu Mteja, na tunakushukuru kwa uvumilivu wako.

Tafadhali fahamu kuwa ofisi yetu ya Dodoma tayari imepokea taarifa kuhusu changamoto hii na inaendelea kuifanyia kazi kwa lengo la kuhakikisha suluhisho ni lakudumu.

Tunaomba uendelee kuwa na subira na uvumilivu wakati hatua zinazohitajika zikiendelea kuchukuliwa. Unaweza pia kutufuatilia tena au kutembelea ofisi zetu kwa maelezo na ufuatiliaji zaidi.

Mara maboresho yatakapokamilika, tutatoa taarifa rasmi kuhusu hali ya huduma.

Asante kwa ushirikiano na uvumilivu wako. ^HN
 
Back
Top Bottom