KERO Mtaa wa Swahili - Kariakoo unatia aibu Taifa kwa wageni

KERO Mtaa wa Swahili - Kariakoo unatia aibu Taifa kwa wageni

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kariakoo ni kitovu cha biashara na panaingiza fedha nyingi sana lakini ni eneo ambalo ni limesahaulika na watu wa manispaa au serikali za mitaa wanachojua ni kukusanya service levy tu.

Mfano, mtaa mmoja wa Sikukuu una matope, chemba zinatiririsha maji machafu, mtaa unanuka na kibaya zaidi ni mtaa ambao unaunganisha barabara ya Uhuru na Soko Kuu.

Nimetumia mtaa mmoja kama mfano tu. Pia ni maajabu barabara nyingi za Kariakoo zimekuwa tope na vumbi. Kiangazi zinajengwa kwa lami lakini baada ya miaka miwili au mitatu zimeisha utadhani yanapita malori.

Mamlaka chukueni hatua, tunaaibika kwa wageni
 
Back
Top Bottom