Mtaala mpya wa elimu, walimu jiandaeni kurudi shule

Mtaala mpya wa elimu, walimu jiandaeni kurudi shule

Huu mtaala ni mzuuri lakin siyo sanaa Sasa hapa kwenye utekelezaji ni zero kwanz mm naona ni siasa tuu unawezaje kusema darasa la kwanz mpka form four Huku hujaboresha miundombinu mfano kata Moja Ina shule za msingi 6 mpka 5 Alfu shule ya secondary ipo Moja kata nzima ndo ihudumie shule 6 za msingi,,,, Alfu hiyo shule Moja ya secondary unakuta Ina changamoto ya Madarasa Yani wanafunz hawatoshelezi kweny Madarasa,, imagine watoto waunganishe kutoka la kwanza mpka secondary kama hatuendo kutengeneza zero nyingi kwa sabab ya changamoto za miundo mbinu kama vyoo, maji pamoja na mazingira kwa ujumla Kuna baadhi ya wanafunzi wapo mbali na shule ya sekondari watahitaji waishi bwenini Ili Kuwa karibu na shule,, na masomo ya secondary siyo kama msingi inahitaji mtot ajipange vizuri kimazingira.
Kwangu mm sion huu mtaala kama utaleta faida kama wanataka faida waboreshe miundo mbinu kama kujenga Madarasa kutengeneza mazingira Bora.

Tusifurahie mtaala huu mzuri tifikirie upande wa pili mfano kwenye mtaala huo nimeona wanasema mason ya tehema (technology) yatakuwa kipaumbele je vitendea kazi vipo kama walimu wa kufundisha hayo masomo lakini pia hizo computer 🖥️ zipo kwa ajili ya kujifunza kwa upande wa practically,, na hizo computer zitahitaji kuendeshwa kwa umeme, mfano Huku kwetu shule Ina zaidi ya miaka 40 lakin Haina umeme so hapo serikari imejipanga kivip au ni siasa tuu

Kwenye kusema hapo walimu sjui wa shule msingi wakafanye mitihani ya form six hicho kitu kigum coz Kuna baadhi sifa za kufanya mtihani wa form six mfano Kuna shule Moja Kuna mwalimu ana certificate lakin kwenye cheti chake ana four ya 28 Yani Hawa ndo wale walokua wakihitim Kipindi JK maana hat zile credit za kwenda advance Hana Sasa huyo umrudishe tena form six kumferisha tuu

Kiufupi huu mtaala upo vizur lakin bila kuboresha miundombinu huu mtaala hauna faida yeyote na wanafunzi wanaweza hitimu lakin wasiambulie kitu
me naona hizo shule za msingi ndo wanafunzi wataunganisha hapo hapo na masomo ya sekondari kidato cha nne ndo maana walimu wanaotakiwa kufundisha ni wa digri na masters
 
Wametoka kuajiri walimu juz juz hapa.. walizingatia hizo sifa maana najua kbs hii project ilikuw tyr documented au hawakufanya forecasting vzr?

Ningependa zaidi walimu wawe na masters kbs pia mishahara iongezwe.

Hii nchi ina walimu vilaza wengi warudi shule.
walimu wa masters hawezi kujituma kama walimu wa diploma na digri wao muda mwingi mikoni mfukoni tu ndo maana makampuni mengi yaliyofanikiwa watenda kazi wazuri ni ma-technicians na artisans
 
Hazina walimu wenye Diploma lazima uwe na University degree ns teaching licence

Wao degree huita University Diploma

Mtu wa nje ukitaka kufundisha Scandinavian schools lazima ujue lugha yao na uwe na digrii ya education kwenye masomo husika

Bila degree hufundishi hata chekechea
Na bila shaka walimu wanalipwa huko Scandinavia.

Unaleta sera mpya, mtaala mpya, leseni za kufundisha, bodi ya walimu ila unashindwa boresha

Hali za walimu kwa kuwapa mishahara yenye hadhi sawa na kada zingine.

Posho ya kufundishia.

Halafu unataka matokeo makubwa big NOO

Mwalimu wa degree unamlipa laki 7 halafu unataka impact chanya.

Ukiwauliza wanasema walimu wapo wengi sana hawawezi lipwa wote eti serikali itafilishika lakini hao hao Kila mwaka utasikia bungeni

Tamisenga Wanaomba wapewe bilioni 100.5 za kununua magari ya wakuu wa wilaya Kila mwaka.

Wanaomba bilioni 50 za matumizi mengine ambayo hayajulikana (Hela zinaenda mifukoni)

Kila wizara inaomba billion kadhaa za magari, matumizi mengine, chai za vikao yaani nonsense tupu.

Ukitaka uinue sekta ya elimu inua Kila kitu sio unafanya hiki unaacha.

Tuache siasa kwenye ya mambo ya msingi especially ELIMU YETU.
 
Uko sahihi kabisa, wakati niko SUA miaka ya nyuma, wale waliokuwa vipanga na kumaliza chuo na GPA kali ndiyo walikuwa wanabakishwa chuoni na baadae wanaendelea Masters na kuwa assistant lecturers. Shida ya huku ualimu wa primary na sekondari ni maslahi duni, kiasi kwamba sidhani kama wenye Div 1 na 2 watakubali kwenda ualimu.
Ili kuzivutia hizo div 1 na 2 waongezea maslahi mapana katika Fani ualimu.

1. Wapandishe mishahara yenye hadhi.

2. Walete posho za kufundisha pamoja na posho ya makazi kwa walimu wanaokaa mbali na shule.

3.Lete daraja la mshahara kwa level za masters na PhD kwa walimu Ili kuwapa motisha ya kujiendeleza na hatimaye kuwa na walimu wasomi zaidi.

Pia walimu wapya wote mwisho div 3 kwa o level na div 3 kwa form $ix at least kwa kuanzia then iwe mwisho div 2 kwa level zote.

Haya mambo hivi hivi lazima tujidhatiti kweli kweli.

Kuleta mtaala mpya na sera mpya bila maslahi Bora ni sawa kunywa uji bila andazi utaishi kupiga miluzi tu.
 
Sikubaliani na wewe. Walimu wa diploma kwa o level wanafaa sana, na huwa wako deep kuliko hao wa University. Ufaulu Private huchangiwa na mambo mengi. Mfano huchagua wanafunzi wazuri tu huku sekondari za umma zikihamishiwa darasa la saba zima bila mchujo wa maana.

Pia, wana miundombinu ya kutosha na hata teacher to student ratio si kubwa kivile. Kama hujui miaka ya nyuma (2000 kurudi nyuma, o level zote zilikuwa na walimu wa diploma tu, lakini ufaulu ulikuwa mzuri kuliko hizo private. Sababu, sekondari zilikuwa chache sana na hivyo mchujo wa maana.
Mwalimu wa Diploma anakuaje deep helezea hapo kwanza

Anasoma miaka 2 tu Chuo wakati wa degree miaka 3 plus form six yake.

Naomba nikuambie katika ualimu kinachofundishwa chuoni ni pedagogy skills mostly na few courses kwa teaching subjects.

Pedagogy skills wanasomea wote.(dipl na degree)

Management skills wanasomea wote

Teaching subjects courses na methodology wanasomea wote.

So hoja Yako ya mwalimu wa Diploma Yuko deep Haina mashiko mkuu(kwa heshima zote)

Labda nipe point zingine nitakuelewa.
 
me naona hizo shule za msingi ndo wanafunzi wataunganisha hapo hapo na masomo ya sekondari kidato cha nne ndo maana walimu wanaotakiwa kufundisha ni wa digri na masters
Ebu fikiria tena je Vitabu vipo vya kufundishia Madarasa je? Walimu yani mwalimu afundishe la kwanza au la tano tena aende afundishe form three hicho kitu kinawezekana haya Leo tunaona shule msingi nying wanafunzi hawana madawati weng wao wanakaa chin je hilo utapambana nalo vipi? Kama umesoma secondary nafikiri unajua jinsi gani masom ya secondary yalivyo yanahitaji mazingira Bora Ili mwanafunzi afaulu siyo kwa mazingira mabovu tu ufikiri utatengeneza ufauli mzuri hicho kitu hakiwezekani
Waboreshe miundo mbinu kwanza ndo mengine yafuate
 
Ebu fikiria tena je Vitabu vipo vya kufundishia Madarasa je? Walimu yani mwalimu afundishe la kwanza au la tano tena aende afundishe form three hicho kitu kinawezekana haya Leo tunaona shule msingi nying wanafunzi hawana madawati weng wao wanakaa chin je hilo utapambana nalo vipi? Kama umesoma secondary nafikiri unajua jinsi gani masom ya secondary yalivyo yanahitaji mazingira Bora Ili mwanafunzi afaulu siyo kwa mazingira mabovu tu ufikiri utatengeneza ufauli mzuri hicho kitu hakiwezekani
Waboreshe miundo mbinu kwanza ndo mengine yafuate
wataboresha wanasema wamejipanga
 
Hizi Elimu za vyuo vikuu wanazitukuza tu % kubwa hazina impact na wanaozisoma wenyewe % kubwa ni weupe kabisa kichwani. Nadhani waliomaliza vyuo vikuu mtanisapoti kwa hili. Huko vyuoni kuna mengi ya kuboresha. Km mtu anamaliza chuo kikuu lakini ni mweupe kichwani inakuwa haina maana. Hata lugha tu ya Kiingereza ambayo ndiyo lugha ya kufundishia na kujifunzia unakuta mhitimu hawezi hata kutengeneza sentence moja. Wakati nipo chuo kikuu nimeshuhudia wanachuo wanashindwa kabisa ku-present assignments wanazopewa. Wakati wa presentation mtu ana tetemeka mwili mzima utadhani kuku wa kideli, lakini mwisho wa sku anapitia mgongo wa wenzake ktk course work na kuhitimu. Na huyo eti ndiyo tunataka awafundishe watoto wetu kisa kamaliza Diploma au Degree na GPA kubwa.

Mimi nadhani tulitakuwa tuanze na watoa hizo degree. Tatizo lililoko huko vyuoni kwa sasa limetokana na serikali kuthamini matokeo ya kwenye makaratasi(ufaulu wa vyeti) kuliko uhalisia wa mtu kichwani. Mfano eti ili uwe lecturer sharti uwe na 3.5 na kuendelea undergraduate wakati mtu anakuwa na 4.0 lakini reasoning yake na presentation of ideas are poor. Bora tungeimarisha huko kwanza kuondoa Walimu wa vyuo vikuu wenye GPA kubwa lakini kichwani wanatia mashaka na pia kudhibiti utoaji wa degree za ujanja ujanja(nimewahi kuskia vijana wakiziita degree za vyupi, sjui ni degree gani hizo).

Na niseme tu kuwa hata mambo wanayosoma kwa sasa huko vyuo vikuu wanaenda kutumia robo tu ktk ufundishaji hasa O-level. Enzi zetu Mwalimu wa degree alikuwa anafundisha A-level tu, sio km sasa eti wanafundishwa hadi Msingi. Are we serious. Sisi tumefundishwa na Walimu wa UPE na waliomaliza Elimu ya mkoloni darasa la 4 tukiwa shule ya Msingi, Walimu wa Diploma kwa O-level, na wa Degree kwa A-level na walikuwa wazuri sana hata kuliko wa sasa. Kwa nini hatujiulizi hilo na kujiuliza tulikosea wapi hadi baadae tukapata Walimu wenye uwezo hafifu.

Hivyo, tulitakiwa kupata majibu ya wapi tulipotoka, tumefikaje hapa, na tutaendaj huko mbele bila kubadilisha mtaala kwa kasi ya 4G na kuwabana Walimu kuwa na Elimu kubwa wakati application yake ktk kazi zao hata robo haifiki. Kuendelea kuthamini Elimu kubwa na GPA kubwa ni kujitekenya na kucheka wenyewe.

Sioni ulazimana wa Walimu wa shule ya Msingi kuwa na Diploma na Sekondarikuwa na degree kwa kuzingatia hayo niliyosema hapo juu. Wapo watakaonipinga lakini huo ndiyo ukweli. Kuna Walimu kibao tu Wana Elimu ya cheti au stashahda lakini wako makini na wanajuwa kuliko hao wa degree.

Km wingi wa madarasa kichwani ni utambulisho kwa mtu kuwa amesoma sana na kujua mengi mbona serikalini Elimu ya Uzamili ( Masters) kwa Walimu haitambuliki wala siyo ya lazima. Yani ukiwa nayo ni sawa na pambo tu haitakuongezea chochote ktk career yako ya Ualimu? Maanake ni kuwa mtu wa Masters kwa career ya Ualimu hana jipya tofauti na undergraduate. Na huo pia unabakia kuwa ukweli.

Nimemaliza, wale milozaliwa kwa ajili ya kupingapinga bila hoja madhubuti kazi kwenu.
Ni kama unataka mambo yabaki vile vile kama zamani lakini hayana tena impact kwa Sasa Hali halisi ilivyo.

Unataka watu waliofeli ndio wabaki kufundisha huko mashuleni.

Mabadiliko haya ya Sasa kwa walimu na kiwango Cha taaluma zao ni step stone kuelekea kupandisha hadhi ya elimu yetu kiubora na maslahi ya walimu.

Achana na fikra za zamani sijui ilikuwa vipi au vile wote tumesoma huko zamani ila kwa mahitaji ya Sasa ya Dunia na mwamkonwa mabadiliko ya sayansi na teknolojia tunahitaji walimu wasomi kwa level zote.

Hii itawasaidia hata waajiri wao waone aibu wawalipe vizuri kama kada zingine.
 
Kabisa mkuu,
Sikufanya utafiti ila mdo

Kabisa mkuu,
Sikufanya utafiti ila nilimuuliza mdogo wangu ni Mwl.
Majibu yalikuwa hivi;

Shuleni kwao kuna walimu 17,kati yao mathematics ni 3,Physics 2, chemistry ni 3(HM) ndani, Biology ni 4(HM)ndani. Kati ya hao degree holder ni 2 kwa maana ya mathematics and ICT, Chemistry and biology (HM). Waliosalia (physics and mathematics ni 1),(Chemistry and biology ni 2),(mathematics and geography ni 1) na (physics and biology ni 1) hawa wote ni diploma holder. Hapo ni shule moja,waende masomoni kwa wakati mmoja?

Hili suala Linahitaji maandalizi ya muda mrefu ili kuto athiri ufundishaji na ujifunzaji shuleni.
Mdogo wangu ndo huyo wa physics and mathematics lkn anasema hana muda wa kupoteza kwenda kupiga book upya,yuko tayari kwenda msingi ama achote mpunga Bank ajiengue akasomee pharmacy baadae afungue pharmacy kuliko elimuni huko kutishiana kwingi.
Sio lazima walimo wote wa diploma waomdoke kwenda masomoni wakiiacha shule Haina walimu

Dunia imebadilika sana mkuu siku hizi.

Kuna vyuo vinatoa shahada za elimu katika njia huria na masafa( Open and distance learning)

Una Chuo kikuu huria(OUT) taasisi ya elimu ya watu wazima (IAE) huko watoa degree za

Bachelor of education
Bachelor of science
Bachelor of arts with education.

Wanaweza jiendeleza huko na wakafikia lengo.

Tena nimesikia serikali imeanza ukarabati wa teachers resources centers (maarufu kama Clasta). Ili kuwapa walimu mazingira mazuri ya kujiendeleza wakiwa ndani ya vituo vya kazi bila kuathiri ufundishaji na ujifunzaji mashuleni.

So Kila kitu kinawezakana jambo la kwanza kabisa ni attitude Yako na ya yule. Unajiset vipi kukabiliana na changes.
 
Ila kumbuka Kuna diploma ya primary na diploma ya secondary education
Usichanganye madesa
Kuna kitu kinaitwa elimumsingi maana yake ni elimu kuanzisha Darasa la kwanza hadi kidato Cha sita.

Walimu wote wa sekondari regardless kasomea SoMo Gani anaweza fundisha shule ya msingi maana na pedagogy skills na others skills which makes him/her a teacher.

Japo walimu wa shulengi hasa wenye certificate hawawezi fundisha sekondari kutokana level yao ya elimu
 
Wametoka kuajiri walimu juz juz hapa.. walizingatia hizo sifa maana najua kbs hii project ilikuw tyr documented au hawakufanya forecasting vzr?

Ningependa zaidi walimu wawe na masters kbs pia mishahara iongezwe.

Hii nchi ina walimu vilaza wengi warudi shule.
Hio ndio mistake kubwa wamefanya wanaongeza idadi nyingine ya walimu wenye certificate wakati wanataka kuachana na huo mfumo.

Hilo ni tatizo . Sijui wamejipangaje!?
 
Wametoka kuajiri walimu juz juz hapa.. walizingatia hizo sifa maana najua kbs hii project ilikuw tyr documented au hawakufanya forecasting vzr?

Ningependa zaidi walimu wawe na masters kbs pia mishahara iongezwe.

Hii nchi ina walimu vilaza wengi warudi shule.
Hio ndio mistake kubwa wamefanya wanaongeza idadi nyingine ya walimu wenye certificate wakati wanataka kuachana na huo mfumo.

Hilo ni tatizo . Sijui wamejipangaje!?
 
walimu wa masters hawezi kujituma kama walimu wa diploma na digri wao muda mwingi mikoni mfukoni tu ndo maana makampuni mengi yaliyofanikiwa watenda kazi wazuri ni ma-technicians na artisans
Tatizo linakuja ni pale mwalimu mwenye masters unapomlipa sawia na mwalimu mwenye cheti

Mwalimu huyo mwenye masters kafanya bidii kujiendeleza wakati huo huo anafundisha

Humpia rewards kulingana na kiwango chake Cha elimu alichofikia unamlipa sawa sawa na mwenye certificate.

Motisha atapata wapi ya kufundisha

Hao wenye cheti wanafundisha sana sababu ya woga tu Wala sio kwamba wanaipenda sana kazi yao maana nao msoto uko pale pale.

Ndio maana nasema kuwe daraja la mshahara kwa walimu wenye masters akileta masters yake apewe daraja jipya instantly bila longo longo na kuzushana.

Hii pia italeta motisha kwa wenye vyeti tu wakajiendeleze hatimaye shule zinajaa walimu wenye masters wasomi wenye maarifa ya kutosha na kutoa elimu Bora zaidi.

Tuachane na mawazo ya kizamani
 
Mwalimu wa Diploma anakuaje deep helezea hapo kwanza

Anasoma miaka 2 tu Chuo wakati wa degree miaka 3 plus form six yake.
Kifupi mwalimu mwenye Diploma hawezi jioinganisha na mwenye digrii hata siku.moja yuko chini sana wa Diploma sababu vyuoni wanakosomea Diploma za ualimu ,walimu wanaowafundisha hizo diploma ni wenye digrii

Sasa huyo mwalimu wake akienda kufundisha sekondari kusema eti wa Diploma atamzidi uwezo wa kufundisha sio Kweli Degree na Diploma ,degree iko juu zaidi
 
Back
Top Bottom