Mtaala mpya wa elimu, walimu jiandaeni kurudi shule

me naona hizo shule za msingi ndo wanafunzi wataunganisha hapo hapo na masomo ya sekondari kidato cha nne ndo maana walimu wanaotakiwa kufundisha ni wa digri na masters
 
walimu wa masters hawezi kujituma kama walimu wa diploma na digri wao muda mwingi mikoni mfukoni tu ndo maana makampuni mengi yaliyofanikiwa watenda kazi wazuri ni ma-technicians na artisans
 
Na bila shaka walimu wanalipwa huko Scandinavia.

Unaleta sera mpya, mtaala mpya, leseni za kufundisha, bodi ya walimu ila unashindwa boresha

Hali za walimu kwa kuwapa mishahara yenye hadhi sawa na kada zingine.

Posho ya kufundishia.

Halafu unataka matokeo makubwa big NOO

Mwalimu wa degree unamlipa laki 7 halafu unataka impact chanya.

Ukiwauliza wanasema walimu wapo wengi sana hawawezi lipwa wote eti serikali itafilishika lakini hao hao Kila mwaka utasikia bungeni

Tamisenga Wanaomba wapewe bilioni 100.5 za kununua magari ya wakuu wa wilaya Kila mwaka.

Wanaomba bilioni 50 za matumizi mengine ambayo hayajulikana (Hela zinaenda mifukoni)

Kila wizara inaomba billion kadhaa za magari, matumizi mengine, chai za vikao yaani nonsense tupu.

Ukitaka uinue sekta ya elimu inua Kila kitu sio unafanya hiki unaacha.

Tuache siasa kwenye ya mambo ya msingi especially ELIMU YETU.
 
Ili kuzivutia hizo div 1 na 2 waongezea maslahi mapana katika Fani ualimu.

1. Wapandishe mishahara yenye hadhi.

2. Walete posho za kufundisha pamoja na posho ya makazi kwa walimu wanaokaa mbali na shule.

3.Lete daraja la mshahara kwa level za masters na PhD kwa walimu Ili kuwapa motisha ya kujiendeleza na hatimaye kuwa na walimu wasomi zaidi.

Pia walimu wapya wote mwisho div 3 kwa o level na div 3 kwa form $ix at least kwa kuanzia then iwe mwisho div 2 kwa level zote.

Haya mambo hivi hivi lazima tujidhatiti kweli kweli.

Kuleta mtaala mpya na sera mpya bila maslahi Bora ni sawa kunywa uji bila andazi utaishi kupiga miluzi tu.
 
Mwalimu wa Diploma anakuaje deep helezea hapo kwanza

Anasoma miaka 2 tu Chuo wakati wa degree miaka 3 plus form six yake.

Naomba nikuambie katika ualimu kinachofundishwa chuoni ni pedagogy skills mostly na few courses kwa teaching subjects.

Pedagogy skills wanasomea wote.(dipl na degree)

Management skills wanasomea wote

Teaching subjects courses na methodology wanasomea wote.

So hoja Yako ya mwalimu wa Diploma Yuko deep Haina mashiko mkuu(kwa heshima zote)

Labda nipe point zingine nitakuelewa.
 
me naona hizo shule za msingi ndo wanafunzi wataunganisha hapo hapo na masomo ya sekondari kidato cha nne ndo maana walimu wanaotakiwa kufundisha ni wa digri na masters
Ebu fikiria tena je Vitabu vipo vya kufundishia Madarasa je? Walimu yani mwalimu afundishe la kwanza au la tano tena aende afundishe form three hicho kitu kinawezekana haya Leo tunaona shule msingi nying wanafunzi hawana madawati weng wao wanakaa chin je hilo utapambana nalo vipi? Kama umesoma secondary nafikiri unajua jinsi gani masom ya secondary yalivyo yanahitaji mazingira Bora Ili mwanafunzi afaulu siyo kwa mazingira mabovu tu ufikiri utatengeneza ufauli mzuri hicho kitu hakiwezekani
Waboreshe miundo mbinu kwanza ndo mengine yafuate
 
wataboresha wanasema wamejipanga
 
Ni kama unataka mambo yabaki vile vile kama zamani lakini hayana tena impact kwa Sasa Hali halisi ilivyo.

Unataka watu waliofeli ndio wabaki kufundisha huko mashuleni.

Mabadiliko haya ya Sasa kwa walimu na kiwango Cha taaluma zao ni step stone kuelekea kupandisha hadhi ya elimu yetu kiubora na maslahi ya walimu.

Achana na fikra za zamani sijui ilikuwa vipi au vile wote tumesoma huko zamani ila kwa mahitaji ya Sasa ya Dunia na mwamkonwa mabadiliko ya sayansi na teknolojia tunahitaji walimu wasomi kwa level zote.

Hii itawasaidia hata waajiri wao waone aibu wawalipe vizuri kama kada zingine.
 
Sio lazima walimo wote wa diploma waomdoke kwenda masomoni wakiiacha shule Haina walimu

Dunia imebadilika sana mkuu siku hizi.

Kuna vyuo vinatoa shahada za elimu katika njia huria na masafa( Open and distance learning)

Una Chuo kikuu huria(OUT) taasisi ya elimu ya watu wazima (IAE) huko watoa degree za

Bachelor of education
Bachelor of science
Bachelor of arts with education.

Wanaweza jiendeleza huko na wakafikia lengo.

Tena nimesikia serikali imeanza ukarabati wa teachers resources centers (maarufu kama Clasta). Ili kuwapa walimu mazingira mazuri ya kujiendeleza wakiwa ndani ya vituo vya kazi bila kuathiri ufundishaji na ujifunzaji mashuleni.

So Kila kitu kinawezakana jambo la kwanza kabisa ni attitude Yako na ya yule. Unajiset vipi kukabiliana na changes.
 
Ila kumbuka Kuna diploma ya primary na diploma ya secondary education
Usichanganye madesa
Kuna kitu kinaitwa elimumsingi maana yake ni elimu kuanzisha Darasa la kwanza hadi kidato Cha sita.

Walimu wote wa sekondari regardless kasomea SoMo Gani anaweza fundisha shule ya msingi maana na pedagogy skills na others skills which makes him/her a teacher.

Japo walimu wa shulengi hasa wenye certificate hawawezi fundisha sekondari kutokana level yao ya elimu
 
Hio ndio mistake kubwa wamefanya wanaongeza idadi nyingine ya walimu wenye certificate wakati wanataka kuachana na huo mfumo.

Hilo ni tatizo . Sijui wamejipangaje!?
 
Hio ndio mistake kubwa wamefanya wanaongeza idadi nyingine ya walimu wenye certificate wakati wanataka kuachana na huo mfumo.

Hilo ni tatizo . Sijui wamejipangaje!?
 
walimu wa masters hawezi kujituma kama walimu wa diploma na digri wao muda mwingi mikoni mfukoni tu ndo maana makampuni mengi yaliyofanikiwa watenda kazi wazuri ni ma-technicians na artisans
Tatizo linakuja ni pale mwalimu mwenye masters unapomlipa sawia na mwalimu mwenye cheti

Mwalimu huyo mwenye masters kafanya bidii kujiendeleza wakati huo huo anafundisha

Humpia rewards kulingana na kiwango chake Cha elimu alichofikia unamlipa sawa sawa na mwenye certificate.

Motisha atapata wapi ya kufundisha

Hao wenye cheti wanafundisha sana sababu ya woga tu Wala sio kwamba wanaipenda sana kazi yao maana nao msoto uko pale pale.

Ndio maana nasema kuwe daraja la mshahara kwa walimu wenye masters akileta masters yake apewe daraja jipya instantly bila longo longo na kuzushana.

Hii pia italeta motisha kwa wenye vyeti tu wakajiendeleze hatimaye shule zinajaa walimu wenye masters wasomi wenye maarifa ya kutosha na kutoa elimu Bora zaidi.

Tuachane na mawazo ya kizamani
 
Mwalimu wa Diploma anakuaje deep helezea hapo kwanza

Anasoma miaka 2 tu Chuo wakati wa degree miaka 3 plus form six yake.
Kifupi mwalimu mwenye Diploma hawezi jioinganisha na mwenye digrii hata siku.moja yuko chini sana wa Diploma sababu vyuoni wanakosomea Diploma za ualimu ,walimu wanaowafundisha hizo diploma ni wenye digrii

Sasa huyo mwalimu wake akienda kufundisha sekondari kusema eti wa Diploma atamzidi uwezo wa kufundisha sio Kweli Degree na Diploma ,degree iko juu zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…