Mtaala mpya wa elimu, walimu jiandaeni kurudi shule

Mbona wa diploma husoma form six pia.
 
Tuko pamoja, ila lazima ujue unataka elimu ya Nini kwa watu gani. Siyo ku copy copy kutoka Ulaya. Haingii akili eti mtu aliesoma BA/BSC with education ukampeleka primary akafundishe darasa la kwanza, pili, tatu au nne. Hayo ni matumizi mabaya ya rasilimali watu na uharibifu wa elimu.

Km watu wanataka kuinua Elimu dawa ni moja tu, ni kuchukuwa waliofaulu vizuri O-LEVEL na A-Level (daraja la 1&2). Hapo utaona utofauti wa mtu aliyemaliza form 6 na kwenda Diploma ya Ualimu na kuwa Mwalim na yule aliepata daraja la 3 tena lamwisho na kwenda form 6 kisha Diploma. Hao watakuwa Walimu 2 tofauti kabisa. Siyo tu kufika chuo kikuu.Hujiulizi kwa nini vyuo vya kati na primary na sekondari hakuna mambo ya GPA ili kuajiliwa? Ukipata jibu ulete hapa. Kuna levels ktk Elimu ya Tanzania inachukuluwa easy na ya kawaida sn, hatiliwi mkazo Wala maanani.

Madarasa mengi kichwani siyo determinant factor ya mtu kuwa na uelewa mkubwa wa mambo ingawa madarasa hayo mengi ni kiashiria Cha mtu kusoma sana na kuwa na uelewa mkubwa. But vice versa is true.

Km na wewe bado unaamini kuwa na Degree ndiyo usomi umepotea. Rejea kwenye mchango wangu wa jana ktk bandiko hili. Ni kweli tunahitaji Walimu waliosoma sana lakini wawe ni wale walioonesha wazi tangu Msingi kwamba ni wazuri kichwani siyo kwa kubahatisha ktk mtihani mmoja wa mwisho.

Labda nikuulize tu. Hivi hukuwahi kuona mtu darasani akiwa wa kawaida lakini kwenye mtihani wa mwisho akawazidi wengi tu waliokuwa vipanga darasani.

Kwani mikataba mibovu ya Nchi hii ambayo inapigiwa kelele na Wananchi unadhani ilisainiwa na watu mbumbumbu, si hao hao wasomi wenye madarasa mengi kichwani lakini no impact.

Km hutaki kuelewa huwezi kuelewa ninachomasnisha

Nimemaliza.
 
Na hili mkalitizame upya
 
Nakumbuka enzi ya UPE, walitakiwa wawe na cheti cha kidato cha nne. Sikumbuki walioshindwa walifanywaje!!
 
Hio ndio mistake kubwa wamefanya wanaongeza idadi nyingine ya walimu wenye certificate wakati wanataka kuachana na huo mfumo.

Hilo ni tatizo . Sijui wamejipangaje!?
Nahisi wanatengeneza Mazingira ya upigaji
 
walimu wa masters hawezi kujituma kama walimu wa diploma na digri wao muda mwingi mikoni mfukoni tu ndo maana makampuni mengi yaliyofanikiwa watenda kazi wazuri ni ma-technicians na artisans
Hapo unaongelea utendaji kazi wa kada za ufundi ni tofauti na Ualimu.

kwa kada zinazohitaji ufundi mtu kuanzia Degree mpk ngazi za juu haendi kufanya kwa vitendo bali anaenda kusimamia tu mara nyingi ni hivyo ila hawa wa kada za chini ndio watendaji wakuu, fatilia hata shughuli za ujenzi hasa barabara.
 
Nakumbuka enzi ya UPE, walitakiwa wawe na cheti cha kidato cha nne. Sikumbuki walioshindwa walifanywaje!!
Hapo ilikuwa ni baada ya kufundisha kwa mafanikio makubwa ila baadae wakaja wanasiasa km sasa wakalazimisha wajiendeleze. Si unajua Tz Kila anae shika mpini anakuwa na yake.
 
Serikal igharamie hzo cost za walimu kwenda soma, ila wakisema mtu akajisomeshe tena kwa mshahara ambao mtu kajaa madeni telee asee itakuwa mazingaombwe.....

Nakumbuka zamani mwajiri alikuwa akimgharamia mtumishi wake katika masomo.

Ila yote kwa yote pamoja na mabadiliko ayo ya mtaala wasisahau maslahi ya hao walimu, leo ukiulza vijana wanataka kufanya kaz wap mtu atakutajia TRA, Bandarin, airport n.k lkn hautosikia mtu akisema ataka akasomee ualim cz wanajua kuwa maslah ya ualim n duni,
 
Inabidi ule upuuzi wa mtu akipata daraja la nne anakimbilia kusoma ualimu ufike mwisho kabisa, kwa sababu haiwezekani 4 itengeneze 1 haiwezekani kabisa
 
Vyema.
Ngoja tuone.
 
Km kuna ukweli vile.
 
Leo tumelijadili hili,mishahara ina viraka sana,hao wakujisomesha itakuaje,na je wasiposoma muafaka utakua ni upi,any way,tuendelee kuvuta mtori nyama tutazikuta chini
 
Unaongea usilolijua ww ..

Private schools never prefer graduates employee...

Nenda kesho private yeyote utakuta vijana form six...fresh kabisa wanapiga kazi..

Private shida yao content bas...
You are right, in private schools the graduates are needed only during the registration of a school. After that it is form six leavers who are cheaper and more efficient at work.
 
Elimu ya Tz mnawapa wanasiasa wasiojitambua that way watu hupeleka watoto wao kusoma nje

Yaani kila kichaa akipata uwaziri anakuja na Ajenda na sera Mpya kuhusu Elimu yetu ...ujinga mtupu
Yakupasa uutazame mchakato wenyewe na usitazame mtu.....
 
Umeisoma sera? Yote hayo yameshughulikiwa.
Watasambaza computer na walimu wake?
Watasambaza science kit na laboratory equipments.?
Watapeleka walimu wa S/Kazi wakafunfundishe kwa halisi?
Watasambaza internet mashuleni ?Watabomia majengo ya zamani na kujenga kama yale ya covid 19.
Wataongezea kipato cha mwalimu na kumupa posho.
Hawa hawa viongizi wa TZ. Aisee nitahamia malawi.
Mkuu sera gazijaanza kubadilishwa leo, nakwambia ni mbwembwe za kila utawala.
Sera ilopo tu imeshindwa kutekelezwa kwa vitendo vipi mpya?
 
Sawa lakini lazima tuanzie somewhere, na pa kuanzia ni SERA na MITAALA then hayo mengine yatafuata mkuu...
Sera zilizopo hazijawahi leta tija, zina avrg implementation, binafsi sitegemei makubwa maana viongizi wetu hawana hamu ya ukweli to transform our education and life. We have mediocre leaders, hatuna exceptional leaders wanaoweza kutuvusha ktk mkwamo wa mtu mweusi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…