Caroline Patsone
New Member
- Jul 26, 2022
- 3
- 2
Mtaala wa elimu ni mpangilio wa kozi au mafunzo ambao shule,vyuo na taasisi za elimu hutoa na katika muda ulio sahihi mwanafunzi aweze kuhitimu.
Mtaala wa elimu unaotumika katika nchi yetu ya Tanzania ni mtaala ambao unampa Mtanzania maarifa na fikra za kuajiriwa zaidi kuliko kujiajiri wakati huo huo ajira zenyewe ni chache sana kulinganisha na wahitimu waliopo mtaani.Pia unafungia watoto ndani ya boksi katika kufikiri kwao kwa upana sababu inabidi wafikiri vile mfumo wa elimu unawataka wafikiri yaani wanakuwa wamewekewa mipaka wa fikra na vipaji vyao.
Si lazima kila mtoto asome ili aje kuwa Daktari,Rubani,Mwanasheria,Mhandisi wakati maisha yetu ya kila siku yanahitaji watu wa aina tofauti tofauti kama Wapishi,Washonaji,Seremala,Wakulima,Wafanya usafi,Madereva ambao wanaubobeaji ndani yao. Hivyo je kifanyike nini ili kupata watu ambao watakuwa wabobeaji katika sekta mbalimbali ili watumike ndani na nje ya nchi!?
Kwa Mtazamo wangu ninaona kwamba ili mtaala wa elimu ulete matokeo chanya katika nchi yetu basi mtaala uwe kwa namna hii..
Mtoto anapoanza chekechea mpaka darasa la nne asome masomo haya yote ya msingi kulingana na hatua ya darasa alilopo yaani kama wa chekechea anawekewa mada ambazo ni nyepesi na fupi kwake kueleweka. Kiswahili,Kiingereza,Hesabu,Historia,Uraia,Stadi za kazi,Sayansi,Michezo na Elimu ya fedha na masomo yote yafundishwe kwa lugha ya Kiingereza kwa kuandika na vitendo zaidi kwa shule zote za Serikali na Binafsi pia kwasababu Kiingereza ni lugha ya mataifa.Kama ambavyo kwasasa Walimu wengi wenye Shahada na Stashahada wanavyofundisha shule za msingi ni nuru njema kwamba kufundisha kwa lugha ya kiingereza haitokuwa tatizo kadri tunavyoendelea.
Mtoto afikapo darasa la tano apewe uhuru wa kuchagua kwamba anataka kusomea nini ili awe nani katika maisha yake na masomo yapi maalum ayasome ili kutimiza ndoto hizo sababu katika umri huo angalau atakuwa ameshajua anataka kuwa nani kupitia masomo yale ya msingi aliyosoma mpaka darasa la nne.
Mfano anataka kuwa Daktari(Wa mifugo au Binadamu na je anataka kubobea kwenye upande wa moyo, figo, ubongo, damu, mifupa, mishipa, macho, ngozi n.k..Seremala..Mpishi wa kitaifa au mataifa..Rubani..Mhasibu..Mwanasiasa..Mbunifu wa mavazi, viatu, majengo..Fundi kushona..Mhandisi wa barabara,majengo..Mchoraji..Mhunzi..Mwandishi..Mtangazaji..Mwalimu wa masomo fulani..Mwanamziki na kadhalika.Lakini pia katika kila fani kuwe na somo la pembeni la jinsi gani Mtoto ataweza kuingiza kipato na kukizalisha maradufu kupitia kazi hiyo ndani na nje ya nchi. Mpaka kufikia miaka 22 angalau kila kijana awe amehitimu mafunzo ya kile alichosoma na kubobea.
Hii itasaidia kupunguza ongezeko la vijana walio mtaani wakisubiri kuajiriwa kutokana na kile walichomezeshwa kichwani wakiwa shuleni bila ujuzi wowote wa ziada unaowawezesha kujiajiri.Pia itasaidia katika kukuza uchumi wa nchi yetu sababu tutakuwa na vijana wenye ujuzi mbalimbali ambao hata vikianzishwa viwanda, kampuni mbali mbali wabobeaji wa sehemu husika wapo. Au hata vijana wenyewe ambao wamebobea katika sekta fulani wanaweza wakajichanga na kutengeneza kitu chao cha pamoja kama sehemu ya kujiingizia kipato na pia wakaajiri wengine wajao.Hata watu wa nchi za magharibi wakiona ufanisi huo ni rahisi kwao kuja kuwekeza sababu hakuna anaetaka kuwekeza katika watu ambao ana uhakika hawana uzalishaji vitu bora.
Hakuna Kiongozi,Mchungaji,Nabii yeyote atakae weza kututoa katika umaskini kabla ya kutukomboa kifikra.Tutazidi kuchukiana kisiasa, kidini kuvutana na kunyoosheana vidole sababu tuna shughulika na matawi tu na sio mzizi. Rasilimali tunazo nyingi tu za kutosha vizazi na vizazi ila tatizo ni kwamba maarifa ya kuzitumia Rasilimali hizo ndio hatuna. Magari, Simu, Vyombo vya umeme, nguo, viatu na kila kitu tunachonunua kutoka nchi za nje kinaweza tengenezwa Tanzania na hao wa nchi za nje ndio watakao kuja kununua kutoka kwetu kupeleka kwao.
Achana na msemo wa kwamba wazungu wana akili sana kuliko waafrika hapana.Alietuumba ni Mmoja na wala hana Upendeleo, Kama tusingekuwa tishio kwa wazungu basi wasingekuja kututawala na kutuletea mbinu za kutugawanyisha kupitia dini,siasa na elimu ya kibaguzi.
Kila Mtoto ana akili na mwelevu kama atapewa uwanja mpana wa kufikiri na kuchagua ni nini asome na nani awe na sio kulazimishwa kutosha katika mfumo ambao unaweza kuwa na manufaa madogo kwake maishani au kutokuwa na manufaa kabisa na wazazi kutofurahishwa na matokeo hayo kuona kama kama wametupa pesa zao bure na kuzidi kuitia familia umasikini.
Muhimu: Hakuna Mtoto Mjinga ila kuna watoto walioshindwa kutosha kifikra katika mfumo wa elimu waliowekewa.Ukombozi wa kizazi unaanzia katika fikra ya mtoto na si kwenye siasa au dini.

Upvote
5