Mtaalam wa kilimo na ufugaji Morogoro

Mtaalam wa kilimo na ufugaji Morogoro

2018

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2018
Posts
546
Reaction score
779
Habari zenu wakuu, Mimi ni mtaalam wa kilimo na ufugaji nimeupata ujuzi huu kutoka katika chuo kikuu cha kilimo cha Sokoine Morogoro.

Natafuta mtu ambaye anatamani kuwekeza katika kilimo cha kisasa,lakini hajui pa kuanzia.

Mimi binafsi natamani kuwekeza katika kilimo cha kisasa na ufugaji maana utaalam na uzoefu ninao wa kutosha ila nimekosa mtaji na eneo la kufanya shughuli hizo,hivyo basi nakaribisha mtu yeyote ambaye yupo committed kuwekeza katika kazi hii yenye manufaa makubwa ndani ya muda mfupi.

Kilimo cha mboga mboga,matango,karoti, vitunguu,nyanya,viazi,nyanya chungu ni kilimo chenye faida kubwa ndani ya miezi michache,pia ufugaji wa kuku,bata,sungura vyote hivyo vitarudisha hela yako mapema endapo utazingatia kanuni bora za kilimo na ufugaji wa kitaalamu.

Hivyo kama kuna mtu yupo Mbeya anataka tufanye kazi hii nipo tayari kufanya nae kazi

Nipate kwa 0755340150
Nipo Mbeya mjini
Karibu!

images.jpg
 
Habari zenu wakuu, Mimi ni mtaalam wa kilimo na ufugaji nimeupata ujuzi huu kutoka katika chuo kikuu cha kilimo cha Sokoine Morogoro.

Natafuta mtu ambaye anatamani kuwekeza katika kilimo cha kisasa,lakini hajui pa kuanzia.

Mimi binafsi natamani kuwekeza katika kilimo cha kisasa na ufugaji maana utaalam na uzoefu ninao wa kutosha ila nimekosa mtaji na eneo la kufanya shughuli hizo,hivyo basi nakaribisha mtu yeyote ambaye yupo committed kuwekeza katika kazi hii yenye manufaa makubwa ndani ya muda mfupi.

Kilimo cha mboga mboga,matango,karoti, vitunguu,nyanya,viazi,nyanya chungu ni kilimo chenye faida kubwa ndani ya miezi michache,pia ufugaji wa kuku,bata,sungura vyote hivyo vitarudisha hela yako mapema endapo utazingatia kanuni bora za kilimo na ufugaji wa kitaalamu.

Hivyo kama kuna mtu yupo Morogoro anataka tufanye kazi hii nipo tayari kufanya nae kazi

Nipate kwa 0778464016
Nipo Morogoro mjini
Karibu!

View attachment 1957464
Huna mtaji na ujuzi na uzoefu unao ? ? wasomi mnatuangusha ! ! kwani mtaji ni nini ? huo ujuzi tayari ni mtaji mkubwa ! ! JIbu hapo tayari wewe sio mjasriamali(wewe ni wa kutumwa na wajasriamali yaani ni mfanyakazi kwa asili) kwa maana hiyo hata ungepewa hicho unachokihitaji ni ngumu sana kufaulu, kama mpaka sasa huoni namna yeyote ya kuanza nakushauri endelea kutafuta ajira..

Msilazimishe mambo kwa gharama za wenzenu, Naomba unisamehe mkuu kama nitakuudhi.
ila lengo langu nikustue hiyo akili yako usiendelee kusubiri mtu na pesa zake azilete uzile.

Kama wewe mwenyewe hujui pa kuanzia then unamtafuta mwenzio asiyejua pa kuanzia yaani vipofu wawili waongozane mtafika kweli ? ?

Naomba MASWALI KUTOKA KWAKO kwa lugha ya kistaarabu
 
Mimi nina eneo zuri huko Turiani na ninapenda sana kuwekeza kwenye kilimo BUT tatizo kuu ni mifugo, wamang'ati na wamasai wamekuwa ni kikwazo kikubwa sana kwa ufugaji wao wa holela. Nishawishi ni kwa namna gani wewe utakabiliana na hii changamoto??
 
Sorry mkuu eneo la ukubwa gani ?
 
Ingekuwa Pwani ningekupa ekari 10 or 20 uzitumie bure kwa muda wa hata 5 years.Nina imani ndani ya muda huo utakuwa na eneo lako tayari.Maji na umeme ni vya kuvuta tu maana vipo jirani na barabara ni nzuri
 
Naomba kuja inbox mkuu
 
Ingekuwa Pwani ningekupa ekari 10 or 20 uzitumie bure kwa muda wa hata 5 years.Nina imani ndani ya muda huo utakuwa na eneo lako tayari.Maji na umeme ni vya kuvuta tu maana vipo jirani na barabara ni nzuri
Naomba kuja inbox mkuu
 
Huna mtaji na ujuzi na uzoefu unao ? ? wasomi mnatuangusha ! ! kwani mtaji ni nini ? huo ujuzi tayari ni mtaji mkubwa ! ! JIbu hapo tayari wewe sio mjasriamali(wewe ni wa kutumwa na wajasriamali yaani ni mfanyakazi kwa asili) kwa maana hiyo hata ungepewa hicho unachokihitaji ni ngumu sana kufaulu, kama mpaka sasa huoni namna yeyote ya kuanza nakushauri endelea kutafuta ajira..

Msilazimishe mambo kwa gharama za wenzenu, Naomba unisamehe mkuu kama nitakuudhi.
ila lengo langu nikustue hiyo akili yako usiendelee kusubiri mtu na pesa zake azilete uzile.

Kama wewe mwenyewe hujui pa kuanzia then unamtafuta mwenzio asiyejua pa kuanzia yaani vipofu wawili waongozane mtafika kweli ? ?

Naomba MASWALI KUTOKA KWAKO kwa lugha ya kistaarabu
Unataka nivamie tuu shamba la mtu nianze kulima?nilimie meno au kucha?nipande kokoto? Ntamwagiliaje hio mimea? Mkuu sina pesa yoyote ya kuanzia? Sio kwamba akili haipo na commitment ya kutosha ila huwezi anza tuu bila resources
 
Shukran sana POLE SANA nimekuelewa kwa majibu yako
 
Ingekuwa Pwani ningekupa ekari 10 or 20 uzitumie bure kwa muda wa hata 5 years.Nina imani ndani ya muda huo utakuwa na eneo lako tayari.Maji na umeme ni vya kuvuta tu maana vipo jirani na barabara ni nzuri
Mkuu mtu akitaka kukodi inakuwa je?
 
Unataka nivamie tuu shamba la mtu nianze kulima?nilimie meno au kucha?nipande kokoto? Ntamwagiliaje hio mimea? Mkuu sina pesa yoyote ya kuanzia? Sio kwamba akili haipo na commitment ya kutosha ila huwezi anza tuu bila resources
Haya majibu sio mazuri hata kidogo. Amekuambia kistaarabu lakini ulivyojibu umetoa mashaka.

Mtu kama wewe ungenifaa Sana ila tatizo watu uaminifu imekuwa shida.

Ongea na jamaa kama atakupa hizo heka 20 au kumi nitafute tuangalie nini cha kugamya. Soko la mboga , boga ninalo shida ni mtu wa kusimamia na eneo ambalo liko karibu na Dar es salaam
 
Mkuu mtu akitaka kukodi inakuwa je?

Inawezekana lakini kwa kuanzia naona sii vizuri kukodisha hasa kwa mtu anayeanza!Naona ni vizuri kumsaidia mtu kwa kile unachoweza.Pia kuliko pori likae tu bure ni afadhali umpe mtu atumie bure.
By the way nimeshafyeka na kung'oa visiki kama ekari 10
 
Safi sana. Shamba liko PWANI sehemu gani mkuu na hayo maji uliosema ya kuvuta ni mto ama dawasa?
 
Haya majibu sio mazuri hata kidogo. Amekuambia kistaarabu lakini ulivyojibu umetoa mashaka.

Mtu kama wewe ungenifaa Sana ila tatizo watu uaminifu imekuwa shida.

Ongea na jamaa kama atakupa hizo heka 20 au kumi nitafute tuangalie nini cha kugamya. Soko la mboga , boga ninalo shida ni mtu wa kusimamia na eneo ambalo liko karibu na Dar es salaam
Usimamizi wa namna gani mkuu? Fafanua kidogo hapa
 
Haya majibu sio mazuri hata kidogo. Amekuambia kistaarabu lakini ulivyojibu umetoa mashaka.

Mtu kama wewe ungenifaa Sana ila tatizo watu uaminifu imekuwa shida.

Ongea na jamaa kama atakupa hizo heka 20 au kumi nitafute tuangalie nini cha kugamya. Soko la mboga , boga ninalo shida ni mtu wa kusimamia na eneo ambalo liko karibu na Dar es salaam
Hata jamaa alivyomjibu hakumjibu vizuri,binafsi naona kamjibu vizuri that is why jamaa kagundua kakosea,unajua ukiwa mtu wa theory huwezi jua huko field mambo yalivyo magumu.Mtu akisema hana mtaji,neno mtaji ni pana haimanishi hajui cha kufanya au hana elimu.
Unajua mtu ambaye hajawahi kupata shida anashauri kiurahisirahisi tu,lakini in reality unapo enda kwenye utekelezaji mambo ni tofauti sana.
 
Kuna ukweli kwa unacho kisema Ila kama unahitaji msaada lazima ujishushe
 
Back
Top Bottom