Hbr Dr.
Madaktari wetu huwa hawana muda wa kuongea na mgonjwa na kudadisi kwa kina. Nilikuwa na tatizo la kusumbuliwa na malaria kwa karibu miaka kumi mfululizo, miaka hii miwili ukiwamo huu ndio siumwi sana. Sambamba na hill tangu 2002 ninasumbuliwa na Tumbo. Nilipima b/meal pale MMC mwaka huo, wakaona D-Cup is ulcerated. Nikatumia H/Kit. Hakukuwa na nafuu. 2004 Nikafamya endoscopy Serian Hospital Arusha, Dr. hakuona ulcers ila kulikuwa na inflamation sana tumboni. 2010 nikafanya tena endoscopy kwenye Private Hospita., Dr. Akasema kuna vidonda vingine vinaanza vingine vinapona akanipa dawa pamoja na sindano ya kwenye mshipa tatizo halikuisha. 2016 nikafanya tena endoscopy MNH, Dr. hakuona vidonda Ila Tumboni kuna inflammation sana. Kwa sababu ya kuwa na gesi nyingi sehemu ya chini ya kitovu pamoja na kukosa choo kwa hata siku tatu ameshauri afanye colonalscpy, hiki kipimo bado hajakifanya. Ameniambia nifanye Kipimo kingine urea breath test, nimetafuta hospitali zote DSM nzima hakuna hocho kipimo.
Tatizo nikipewa Yale madawa ya kuondoa gesi Mara nyingi yananisabisha kukosa choo. Pia nialiwahi kufanya kipimo cha Hpyroli majibu hayakuweza kuthibitisha uwe.
Aidha ninapata maimivu ya kiuno na chini ya kiunko mpaka kwenye matako. Mgongo mabega nayo yanauma. Nikirudi nyumbani huwa nalala kifudifudi kwa muda wa kama nusu saa mpaka saa moja ili kutoa gesi.
kwa wadudu hao. Hii ni historia kwa kifupi.
Naomba ushauri na mwongozo na sehemu sahihi ya kupata tiba.