Mtaalamu wa mafuta na gesi Tanzania afanikiwa kuzalisha gesi kutoka kwenye kitalu chake mwenyewe na kuandika andiko linaloelezea kile alichokifanya

Mtaalamu wa mafuta na gesi Tanzania afanikiwa kuzalisha gesi kutoka kwenye kitalu chake mwenyewe na kuandika andiko linaloelezea kile alichokifanya

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
7,899
Reaction score
10,415
Mtaalamu wa mafuta na gesi Tanzania, bwana Elia Wilinasi ameitendea haki field yake ya mafuta na gesi baada ya kuzalisha gesi kutoka kwenye kitalu chake mwenyewe na kufanikiwa kuandika andiko zima ya kile alichokifanya.

Katika project hiyo ameshirikiana na wachina wawili wanaoishi China, msudani mmoja anayeishi Dubai, mkongo mmoja na Mnaijeria mmoja.

Screenshot_20231229_114545_LinkedIn.jpg
 
Hayo ndio tunayoyataka na JF yanapigiwa kelele kila siku kuhoji usomu wa mtanzania na mwafrika.
Wasomo watatue matatizo sio wageni tu. Kushirikana sio mbaya hata China, Marekani inashirikiana ma mataifa mengine.
Wasomi wa kada nyingine waige hasa kwenye madini almasi dhahabu nk.
Kuna mgodi mmoja wa dhahabu niliwahi sikia ktk TV jamaa wakieleza walivyowekeza.
Tuone kwenye sekta mbalimbali kama uvuvi, kilimo , misitu, madawa nk

Tanzania inaweza kuuga umasikini.
 
serikali hapo imelala usingizi wa pono, badala wamsaidia afanye kitu kikubwa kitakachoisaidia nchi, wamemtosa, kwasababu yeye sio muwekezaji wa nchi za nje atakayewapatia ten percent. viongozi wetu hawana uchungu na hii nchi. tena awe makini na usalama wake, wabaya wanaweza kumwondoa.
 
Hayo ndio tunayoyataka na JF yanapigiwa kelele kila siku kuhoji usomu wa mtanzania na mwafrika.
Wasomo watatue matatizo sio wageni tu. Kushirikana sio mbaya hata China, Marekani inashirikiana ma mataifa mengine.
Wasomi wa kada nyingine waige hasa kwenye madini almasi dhahabu nk.
Kuna mgodi mmoja wa dhahabu niliwahi sikia ktk TV jamaa wakieleza walivyowekeza.
Tuone kwenye sekta mbalimbali kama uvuvi, kilimo , misitu, madawa nk

Tanzania inaweza kuuga umasikini.
Ni kweli mkuu, kama wazawa wakipewa nafasi ya kutumia akili zao vizuri hakika wanaweza kuvumbua vitu vingi tu.
 
Back
Top Bottom