mwitakesowani,
tatizo la kukosa usingizi hasa ni tatizo la kisaikolojia zaidi, iwapo hajuna dawa zilizotumika kabla ya tatizo. Hii kitaalamu huitwa insomnia.
Kukosa usingizi hutegemea,
1. Je, shida ni kushindwa kuanzisha/kulala?
2. Je, shida ni kushindwa kuendeleza usingizi mara uamkapo?
3. Je shida ni kuamka mapema ("usingizi kupaa")?
Kuna vitu vinavyoweza kusababisha tatizo hili, baadhi ni msongo wa mawazo, kutumia baadhi ya dawa, kubadilisha mfumo wa upumzikaji (kulala), vileo n.k.
Kwa kuonana na mtaalamu wa saikolojia, huweza kubainisha tatizo hasa kwa kutegemea maelezo yako.