Mtaalamu wa maswala ya usingizi

Mtaalamu wa maswala ya usingizi

Mwitakesowani

Member
Joined
Jul 24, 2012
Posts
94
Reaction score
29
Habari wanajamii forum wenzangu....

Kwa yeyote anayefahamu dokta au mtaalamu yoyote anayehusika na maswala ya usingizi naomba anijuze hapa niweze kumuona. Kifupi nakosa usingizi kwa muda mrefu hivyo nataka niende hospital kwa tiba.. Asanteni kwa maoni na ushauri
 
Nakushauri uende hospitalini kwanza na tatizo likiendelea kuwepo urudi hapa
 
Fanya mazoezi. Kwa mfano fanya jogging ya kati ya nusu saa mpaka saa nzima. Usipolala rudi hapa uripoti!
 
Mwitakesowani,

Tatizo la kukosa usingizi hasa ni tatizo la kisaikolojia zaidi, iwapo hajuna dawa zilizotumika kabla ya tatizo. Hii kitaalamu huitwa Insomnia.

Kukosa usingizi hutegemea,
1. Je, shida ni kushindwa kuanzisha/kulala?
2. Je, shida ni kushindwa kuendeleza usingizi mara uamkapo?
3. Je shida ni kuamka mapema ("usingizi kupaa")?

Kuna vitu vinavyoweza kusababisha tatizo hili, baadhi ni msongo wa mawazo, kutumia baadhi ya dawa, kubadilisha mfumo wa upumzikaji (kulala), vileo n.k.

Kwa kuonana na mtaalamu wa saikolojia, huweza kubainisha tatizo hasa kwa kutegemea maelezo yako.
 
Last edited by a moderator:
mwitakesowani,

tatizo la kukosa usingizi hasa ni tatizo la kisaikolojia zaidi, iwapo hajuna dawa zilizotumika kabla ya tatizo. Hii kitaalamu huitwa insomnia.

Kukosa usingizi hutegemea,
1. Je, shida ni kushindwa kuanzisha/kulala?
2. Je, shida ni kushindwa kuendeleza usingizi mara uamkapo?
3. Je shida ni kuamka mapema ("usingizi kupaa")?

Kuna vitu vinavyoweza kusababisha tatizo hili, baadhi ni msongo wa mawazo, kutumia baadhi ya dawa, kubadilisha mfumo wa upumzikaji (kulala), vileo n.k.

Kwa kuonana na mtaalamu wa saikolojia, huweza kubainisha tatizo hasa kwa kutegemea maelezo yako.

asante kwa ushauri mzuri ndugu, je kwa hapa dar ni wapi naweza kuonana na mwanasaikolojia i believe nitapona
 
jaribu kuweka mazingira ya kulala vzur ambayo ni
1.hakikisha sehemu ya kulala iwe sehemu ya kulala tu.usifanye kazi sehemu ya kulala.
2.hakikisha kwamba joto la bedroom liko chini au hakikisha mwili uko ktk joto la chini kwa kuoga ucku kabla ujalala
3.ondoa vitu vinavyokusumbua kulala vizuri mf. Redio,tv,cm chochote ambacho kitakufanya uwaze hicho badala ya kuwaza kulala
4.light intensity inatakawi kupunguzwa.saa ya kulala inatakiwa kuwe giza.extinguish all kind of lights b4 sleepin
 
asante kwa ushauri mzuri ndugu, je kwa hapa dar ni wapi naweza kuonana na mwanasaikolojia i believe nitapona

Hapa Muhimbili kuna kitengo/idara hiyo, unaweza kuonana nao..pia kuna clinic binafsi, mf. kule Kijitonyamana, Mikocheni na Masaki. Lakini wengi wa wanasaikoloia hao ni wale wale wa MNH, kuepuka gharama nashauri uje Muhimbili.
 
Back
Top Bottom