Mtaalamu wa mchezo wa bao msaada

Mtaalamu wa mchezo wa bao msaada

YphNet

Member
Joined
Sep 3, 2022
Posts
63
Reaction score
107
Naomba mnisaidie kipengele cha kutakata katika bao la kete. Shida yangu ni kujua kipengele cha kutakata katika hatua ya kwanza ya mchezo wa bao. Je ikiwa unatakata ukatua kwenye jumba ni lazima kulala au unaruhusiwa kuzoa jumba na kuendelea kutakata ukipenda?

Mi si mchezaji wa bao lakini kuna app /Android game nimelitengeneza ambalo binadamu anacheza vs AI. Kwa sasa linatumia sheria ya uhuru wa "kulala" kwenye jumba au ukitaka unazoa jumba na kuendelea kutakata. Tazama hiyo picha, mfano nataka kutakata kuanzia chumba chenye kete mbili kuelekea kwenye jumba.

So, hapo nataka sheria ambayo inatumika sana (na wengi) ili nikipata muda nibadilishe sheria iliyopo. App bado inamapungufu mengi kwakuwa mchezo wenyewe huu unasheria nyingi na zinachanganya na kila sehemu wanakanuni zao, so napata changamoto katika kuliboresha.
Link ya Playstore.

Nime-attach PDF linaloelezea jinsi ya kutumia BaoTz app na jinsi ya kucheza special bao type (Bao toto type) kwenye hiyo BaoTz app.

UPDATE: Version 2.2.0, Sasa app ya BaoTz inafuata sheria ya kuto kula jumba wakati wa kutakata tofauti na awali ambapo unauhuru wa kula jumba au la. Sheria hii ya sasa ndiyo inatumiwa na wengi. Samahani kwa usumbufu wowote kutokana na mabadiliko haya.
 
Attachments

  • namu.png
    namu.png
    9.6 KB · Views: 5
  • BaoTzGuide.pdf
    BaoTzGuide.pdf
    514.1 KB · Views: 18
Ngoja nikipata nafasi nitafuatilia ulivyootengeneza huo mfumo wako, kisha nitakuchangia maoni juu ya hilo maana mimi ni mdau wa mchezo wa bao
 
Poa
 
Naomba mnisaidie kipengele cha kutakata katika bao la kete. Shida yangu ni kujua kipengele cha kutakata katika hatua ya kwanza ya mchezo wa bao. Je ikiwa unatakata ukatua kwenye jumba ni lazima kulala au unaruhusiwa kuzoa jumba na kuendelea kutakata ukipenda?

Mi si mchezaji wa bao lakini kuna app /Android game nimelitengeneza ambalo binadamu anacheza vs AI. Kwa sasa linatumia sheria ya uhuru wa "kulala" kwenye jumba au ukitaka unazoa jumba na kuendelea kutakata. Tazama hiyo picha, mfano nataka kutakata kuanzia chumba chenye kete mbili kuelekea kwenye jumba.

So, hapo nataka sheria ambayo inatumika sana (na wengi) ili nikipata muda nibadilishe sheria iliyopo. App bado inamapungufu mengi kwakuwa mchezo wenyewe huu unasheria nyingi na zinachanganya na kila sehemu wanakanuni zao, so napata changamoto katika kuliboresha.
Link ya Playstore.
Inakupasa utembelee kwenye vilabu vya mchezo wa bao, zamani pale magomeni mapipa kulikuwa na klabu.Sijui kama ipo...pia pita katika matawi ya CCM mitaani huwa hawakosi wazee wanaocheza hii michezo ya bao na draft. Wao watakufafanulia sheria zote muhimu za mchezo huo,hivyo utajua wapi urekebishe app yako
 
Shukran
 
Naomba mnisaidie kipengele cha kutakata katika bao la kete. Shida yangu ni kujua kipengele cha kutakata katika hatua ya kwanza ya mchezo wa bao. Je ikiwa unatakata ukatua kwenye jumba ni lazima kulala au unaruhusiwa kuzoa jumba na kuendelea kutakata ukipenda?

Mi si mchezaji wa bao lakini kuna app /Android game nimelitengeneza ambalo binadamu anacheza vs AI. Kwa sasa linatumia sheria ya uhuru wa "kulala" kwenye jumba au ukitaka unazoa jumba na kuendelea kutakata. Tazama hiyo picha, mfano nataka kutakata kuanzia chumba chenye kete mbili kuelekea kwenye jumba.

So, hapo nataka sheria ambayo inatumika sana (na wengi) ili nikipata muda nibadilishe sheria iliyopo. App bado inamapungufu mengi kwakuwa mchezo wenyewe huu unasheria nyingi na zinachanganya na kila sehemu wanakanuni zao, so napata changamoto katika kuliboresha.
Link ya Playstore.
Kwa upande wa kusini mwa tanzania hauruhusiwi kuondoka na jumba kama utatakata. Pia kuna game nyingine nacheza hapa ya bao ninayo, unakuta kwamba akitaka anafikia kula au kusafiri ambapo pia ni nje ya sheria. Nyingine jaribu kufika vijiweni wanapocheza bao hilo kila zoeana na wazee wa hapo waambie project yako watakufundisha vitu vingi mpaka baadhi ya michezo hatari ya AI.
Nashauri tu

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Poa poa. Nitajaribu kufuata mfumo huo, nikipata muda, kwani mwenyewe ni wa huko pia south 🙂 . Kwenye app yangu pia intentionally nimeweka aina ya ziada inaitwa bao toto, inasheria rahisi zaidi, na wala ukila hubadili mwelekeo na unaweza kuanza chumba chochote chenye kete zaidi ya moja. Hata mtoto mdogo anaweza ielewa but still ina hesabu nyingi pia.
 
Back
Top Bottom