Mtaalamu wa mifugo (Dr. by Veterinarian): Karibuni kwa ushauri, tiba na dawa za mifugo tu

kuku wangu wamezidiwa na mafua na kikohozi mpaka imepelekea kifo cha kuku wanne aina ya saso mpaka sasa,niliwapatia tylodox nkiwa na mix na eggbooster ila sikufanikiwa kutibu chochote zaidi ya tatizo kuzidi,na saivi nimeshauriwa kuwapa otc 50%,cjui itanifaa kwa wale mlio wataalam naombeni msaada wenu please kuku wangi wana miezi 6 saivi,wananitian stress kwa kweli
 
Habari mtaalamu, ebhana mm nna changamoto ya kupata maziwa kwa ngombe wangu. Niwape lishe gani waongeze maziwa
 
Du pole ningepata huu uz mapema. Wake doxcol kwa doz ya kijiko cha chakula kwa maji Lita 10. Pamoja na multivitamin kama farmvita. Yalikua mafua makali eidha yaliambatana na Kuku kuvimba macho, kukoroma n.k ko ilibid ubadili dawa.
 
Siku nyingine ujipatwa na tatizo hili wape doxcol kwa doz ya kijiko cha chakula kwa maji Lita 10. Pamoja na multivitamin kama farmvita. Yalikua mafua makali eidha yaliambatana na Kuku kuvimba macho, kukoroma n.k ko ilibid ubadili dawa.
 
doctor tunakuomba kwenye group letu la ufugaji kuku Ufugaji wa kuku

Naomba msaada wako. Vifaranga wangu wana kuwa na tabia ya kupindisha shingo kama kizunguzungu na anapotaka kula anashindwa kulenga haraka katika kudonoa chakula husika. Unakuta shingo inajigeuza bila mipango yake.

Anapotaka kunywa maji anakuseakosea kuweka shabaha katika chombo husika na kudonoa chombo hadi atakapobahatisha. Ninawafugia vifaranga ndani ya nyumba. Nimeshindwa la kufanya.
 
Mkuu hizo chanjo za bata ndo zipi??
 
Uliwachanja dhidi ya kideri maana dalili ulizosema hapo ni moja wapo ya kideri mkuu..
 
Siku nyingine ujipatwa na tatizo hili wape doxcol kwa doz ya kijiko cha chakula kwa maji Lita 10. Pamoja na multivitamin kama farmvita. Yalikua mafua makali eidha yaliambatana na Kuku kuvimba macho, kukoroma n.k ko ilibid ubadili dawa.
Mafua sugu yaweza kuwa ni infectious bronchitis ni ugonjwa wa virusi ambao kuku wakiupata wanakuwa na mafua ya muda mrefu bila kupona...

Matumizi ya antibiotic si mazuri maana utaingia gharama kubwa ya kuwatibia kuku wako na tatizo likabakia palepale...

Ni vyema sasa nyie wakulima mkaanza kuwachanja kuku wenu dhidi ya infectious bronchitis na mara nyingi chanjo hii inachanjwa sawa na kideri na bei yake ni 15,000 ukinunua hicho kichupa cha chanjo ndani yake utakuta chanjo ya kideri na infectious bronchitis.
 
Ok asante. Maana nmeisoma hyo hepatitis naona ndo imekumba bata wangu maana amekufa shingo kama karudsha nyuma.
Sawa kiongozi jaribu kuwaweka bata wako katika mazingira safi muda wote..
 
Wape madini ya ultramix na chakula cha kutosha. Pia zingatia kutotumia dume ambalo ni ukoo mmoja na majike ili kuepuka inbreeding.
Ukiachana na lishe pia mazingira huchangia mazimwa kushuka chini hashasa ukimtoa ng'ombe katika mazingira ya ubaridi na kumleta katika mazingira ya joto hiyo kadhia lazma ikukute mkuu...

Pia jitahidi kuwapa concentrate wakati wa ukamuaji hakika watajitahidi kutoa maziwa ya kutosha...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…