Mtaalamu na wadaua wengine habarini za asubuhi?
Tunamshukuru Mungu kwa kutuamsha salama. Mimi ni mfugaji wa ng'ombe wa kienyeji katika wilaya ya kibondo mkoani Kigoma.
Nina maswali matatu kwa mtaalamu wetu:
1. Huku kigoma kuna ugonjwa common sana kwa ng'ombe kwa kisukuma tunauita "LUHAHA" na nadhani ni MAPAFU na dalili zake ni kukohoa kwa ng'ombe, manyoya kusimama kuonyesha dalili kuwa anahisi baridi, kutoa udenda na makamasi.
Tumekuwa tukitumia dawa aina ya Tylocin na OTC 10 au 20%, zinapona lakini hawaishi kuugua kwenye zizi. Naomba kujua Je kuna chanjo ya ugonjwa huu? Na kama hakuna, ni dawa gani nzuri zaidi?
2. Naomba kujua Ng'ombe tunapaswa kuwaogesha dawa ya kuua wadudu ( kupe, chawa n.k) mara ngapi kwa mwezi na je ni dawa gani nzuri zaidi? Mimi natumia Paranex na Twiga TRAZ.
3. Updatikanaji wa dawa za mifugo huku mkoani ni ghari sana, Je kwa jijini kama Dar es Salaam bei zina unafuu ili nipate wakala wa kuwa ananitumia mzigo mkubwa kwa bei nafuu?
Asante
Naitwa James J.
Habari za asubuhi Ndugu James.
Kwanza kabisa nikupe pole kwa kuuguliwa mifugo yako. Kwanza kabisa ugonjwa unaowasumbua huko ni Contagious bovine pleuro pneumonia (CBPP) ugonjwa huu husababishwa na bakteria anaeitwa Mycoplasma mycoides, huenezwa kwa njia ya hewa kutoka kwa mfugo mmoja kwenda kwa mwingine na mara nyingi hutokea sana katika jamii zenye mifugo mingi.
Kuhusu tiba ya ugonjwa huu haupo bali unaweza kuzuiwa kwa njia ya chanjo.
Na kama ni kufanya tiba ni kwamba wale ng'ombe wote uliowatibu watapona lakni wataendelea kuwa carrier (Hapa namaanisha ya kuwa wataendelea kueneza ugonjwa huu kwa mifugo mingine ambao hawakuwahi kupata ugonjwa huu), na mara nyingi huwa tunashauri mifugo wote waliougua ugonjwa huu kutoa kundini moja kwa moja ili kuepuka kuenezwa ugonjwa huu kwa mifugo mingine...
Na ikitokea ukashindwa kutoa mifugo hiyo ndio tunakuja na options ya kutibu na dawa ambazo huwa tunatumia ni TYLOSIN 10mg/kg ambapo hupewa kila baada ya masaa 12 kwa siku 3-5 au OTC 20% katika dose ya 10mg/kg kwa siku 3-5..
Hivyo basi kwa case ya ugonjwa kujirudia rudia ni kwamba either;
1. Hao bakteria wamekuwa sugu hivyo kufanya hizo dawa kutokuwa na madhara kwao (bacterial resistance)
2. Dawa ulizokuwa unawapa ng'ombe wako ulikuwa unakosea matumizi ya dose kwa ujumla
Nini kifanyike sasa, kama ni suala la drug resistance ni vyema ukabdili dawa na ukaanza kutumia dawa nyingine kama vile;
1. Amoxicillin 11mg/kg wape kila baada ya masaa 24 kwa siku 3-5
2. Sulphadimethoxine 30mg/kg wape kwa siku 5
3. procaine penicillin G kwa siku 5 mfululizo.
NB. Kumbuka ugonjwa huo hauna tiba bali kinga tu na chanjo ukihitaji zinapatikana tuwasiliane tu.
Kuhusu kuogesha dawa nzuri kwa sasa ni hiyo Paranex maana ndio imepitishwa na wizara kutumika kwa kipindi hichi...
Na kuhusu kuogesha jitahidi kuogesha kila baada ya siku 21 na katika kipindi cha kupe wengi basi ujitahidi kuwaogesha ng'ombe wako kila baada ya siku 14...
Kuhusu dawa kwa huku DAR ni nafuu kidogo, pia tunaweza fanya biashara nakutumia mzigo baada ya kulipia.
Kama kuna maswali zaidi karibu..
Regards.
Dr. MCM