Mtaalamu wa mifugo (Dr. by Veterinarian): Karibuni kwa ushauri, tiba na dawa za mifugo tu

Retired subiri mpaka mzunguko wa dawa uishe hali itarudi kawaida.Nimeambiwa na mtu hapa yalimkuta.
 
Retired subiri mpaka mzunguko wa dawa uishe hali itarudi kawaida.Nimeambiwa na mtu hapa yalimkuta.
asante kwa kunitia moyo! Leo nimemchoma butalex kuondoa uwezekano wa ECF maana alikuwa anaonyesha kudhoofika zaidi. Baada ya masaa kama 3 hivi akaamka (alikuwa ameanguka anashindwa kuamka), hopefully will resume!
 
Habari za asubuhi Mkuu, kwanza nimeombe samahani kwa kutokujibu kwa wakati hili suala lako la mastitis. Kwa suala lako la mastitis na ng'ombe wa maziwa kupoteza maziwa kwa siku kumi imenishangaza kidogo maana kwa kawaida ng'ombe akiugua mastitis kama alikuwa anatoa maziwa lets say lita 10 kwa siku basi baada ya kuugua ataishia kutoa lita 5 hadi 6 kwa siku na sio kuacha kabisa.

Baada ya kupitia maelezo yako hapo juu, nimeona mtaalamu uliemuita amechoma ng'ombe wako Dexamethasone ambayo hiyo ipo katika kundi la corticosteroid drugs ambapo kiuhalisia hakutakiwa kutumia dawa hii kutibu mastistis narudia tena hakutakiwa kutumia dawa hii kutibu mastitis hii kitu haipo na haitokuja kuwepo katika taaluma hii kutibu mastitis kwa kutumia dexamethasone.

Baada ya huyo kajanja kutumia hiyo dexamethasone ni kwamba ilienda kuingilia mfumo wa uzalishaji maziwa kwa kuzuia hormone inayoitwa ACTH ambayo inahusika na mchakato mzima wa kuinfluence the release of essential hormone ambazo hutumika kuzalisha maziwa. Kisayansi kitendo cha kutumia dexamethasone katika dose ya 40mg inapelekea ng'ombe kutokutoa maziwa kwa takribani siku 4 hadi 5 sasa hapo sijajua huyo kajanja alitumia dose kiasi gani??

Halafu kwenye suala la kutibu mastitis huwa kuna dawa zao maalamu za kuchoma katika kila kuchuchu za ng'ombe ambazo ni Penicillin G ambazo huwa na ujazo wa 10cc, dawa nyingine ambazo husaidia pia ni pamoja na hiyo pen-strep, erythromycin na neomycin ambazo utazitumia kwa siku 3-5 na baada ya hapo mambo yatakuwa safi.

Angalizo, Hakikisha kabla ya kumchoma sindano hizo kiwele chote imekisafisha na maji safi ya uvuguuvugu, umekamua maziwa yote yenye rangi ya unjanounjano hadi pale yatakapokuwa meupe ndio unaruhusiwa kuchoma kwenye chuchu na imani umenieleewa vyema mkuu.

Pia ukitaka kumrudisha ng'ombe wako aendelee kutoa maziwa nenda ukanunue hormone inaitwa oxytocin ni kichupa cha kama 50ml unakuwa unachoma kati ya 5-8ml na ng'ombe ni ndani ya masaa machache utaona ng'ombe anadondosha maziwa mwenyewe ila sasa ningeomba tu uzingatie afya ya wanywaji wa maziwa yako kwa kuruhusu huo mzunguko wa dawa ulizomchoma (withdraw period) umetimia ndio maziwa hayo yaingie sokoni.

Nikutakie siku njema
 
Habari za leo wana jamvi,
Doctor mimi ni mfanyakazi ktk sector binafsi lakini pia mjasiliamali mfugaji ng'ombe wa asili jamii ya ankole na NYABUGESERA ( wana pembe za kati ila miili mikubwa sawa au zaidi ya Ankolle). Nina maswali mawili hapa na ningeomba ushauri na maelekezo ya nini cha kufanya:

1. Kumekuwepo na tatizo la ng'ombe wangu kupata miscarriage mara kwa mara wakiwa na mimba za miezi kati ya sita hadi nane. Kwa ndama wanaozaliwa wakiwa na miezi nane wanakuwa na manyoya na wananyonya japo hawawezi kusimama na hatimaye hufa baada ya wiki kama moja hivi.

2. Naomba kuelewa nini kinasababisha ng'ombe ambaye ana nzao moja au ya pili then apata miscarriage mimba labda ya tatu halafu anakuwa hashiki tena mimba japo anapandwa?

Asante saaana.
 

Habari za saa hizi Mkuu...

Pole sana kwa kuuguliwa na mifugo yako, nafahamu unapitia kipindi kigumu sana kwa sasa kwa kupoteza mifugo yako hasa ndama wadogo baada ya kuzaliwa.

Kutokana na maelezo yako, Mifugo yako wanashambuliwa na ugonjwa unaitwa Brucellosis unaosababishwa na bakteria anaeitwa Brucella abortus, bakteria hushambulia mfumo mzima wa uzazi na hivyo kupelekea ng'ombe alieshika mimba kutoa akiwa na kati ya miezi kuanzia mwezi wa 7

Dalili za ugonjwa huu ni kama ulivyosema hapo juu, ng'ombe hutoa mimba katika miezi tajwa hapo juu, pia akibahatika kuzaa basi huzaa ndama ambae ni dhaifu na hivyo ndama huyo kufa ndani ya kipindi kifupi.

Ugonjwa huu husambaa sana katika shamba maana huambukizwa kwa njia ng'ombe kula nyasi ambazo zimeguswa na majimaji yale ambayo hutoka katika kipindi cha kuzaa na kwa njia ya kupanana baina ya dume na jike maana bakteria hao hupatikana katika shahawa za dume.

Pia ng'ombe husika akitoa mimba mara mbili hadi tatu hupoteza uwezo wa kupata mimba tena kwa sababu kizazi kinakuwa kimeathirika tayari na hakuna uwezo wa kubeba mimba tena.

Njia sahihi ya wewe kujikinga na ugonjwa huo ni kwa kutumia chanjo ambazo zinapatikana aina na brucella strain 19 au 45/20 ili kuwakinga ng'ombe wako..

Pia ukisema utumie antibiotic ni kwamba wataishia kupoa tu lakni wataendelea kusambaza bakteria hao kwa ng'ombe wengine..

Zingatia: Ugonjwa huo ni zoonotic ambayo ina maanisha ya kwamba unaweza kuambukizwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu hivyo hakikisha pale unapomhudumia ng'ombe wako hakikisha unakuwa umevaa vitendea kazi.

Kwa msaada zaidi weka namba yako nitakutafuta incase ukihitaji chanjo na huduma ya kuchanjiwa.
 
Habari za leo Doctor,
Asante saana kwa Ushauri wa kitaalamu.
Habari za muda huu kiongozi.
Asante saana kwa ushauri na mwongozo wa kitaalamu.
Ninayo namba yako inayoishia 65 nitakupigia tuongee zaidi.
Asante
 
Habari za leo Doctor,
Asante saana kwa Ushauri wa kitaalamu.

Habari za muda huu kiongozi.
Asante saana kwa ushauri na mwongozo wa kitaalamu.
Ninayo namba yako inayoishia 65 nitakupigia tuongee zaidi.
Asante
Hakuna neno mkuu
 
chanjo yao inaitwaje?.
 
Wana Jamvi salama jamani.
Karibuni katika jukwaa let us la kilimo na mifugo.
Mimi ni mmoja wa wafugaji wadogo magharibi mwa Tanzania ninafuga ng'ombe na mbuzi wa kienyeji.
Nina hitaji la kuboresha mbegu ya mbuzi wangu ili kupata mbegu bora ya mbuzi wa nyama wanaokua kwa haraka zaidi.
Nina shida na mbegu ya madume wafuatao kama wapo hapa Tanzania:
1. Savanna
2. Boar
Nimekuwa nikifuatilia mafundisho ya mjasiliamali mmoja aliyepo Uganda anaitwa HAMIISI SEMANDA ambapo amekuwa akionyesha kuwa mbegu hizi za mbuzi aina ya Savanna na Boar ni nzuri sana na tayari wao kule Uganda wameenda mbali hadi level ya Ranchi kubwa za maelfu ya mbuzi..
Sijui ka
 
Wana Jamvi salama jamani.
Nilikuja kwenye jukwaa hili nikiwa na lengo la kupata msaada wa tatizo langu lakini kimya. Nadhani sio jukwaa sahihi:

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Mimi ni mmoja wa wafugaji wadogo magharibi mwa Tanzania ninafuga ng'ombe na mbuzi wa kienyeji.
Nina hitaji la kuboresha mbegu ya mbuzi wangu ili kupata mbegu bora ya mbuzi wa nyama wanaokua kwa haraka zaidi.
Nina shida na mbegu ya madume wafuatao kama wapo hapa Tanzania:
1. Savanna
2. Boar
Nimekuwa nikifuatilia mafundisho ya mjasiliamali mmoja aliyepo Uganda anaitwa HAMIISI SEMANDA ambapo amekuwa akionyesha kuwa mbegu hizi za mbuzi aina ya Savanna na Boar ni nzuri sana na tayari wao kule Uganda wameenda mbali hadi level ya Ranchi kubwa za maelfu ya mbuzi..
Sijui katika nchi yetu ranchi kama hizi ziko wapi?
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
 
Habari mkuu. Kuhusu upataikanaji wa hao mbuzi kwa hapa Tanzania wanapatikana na kama ni suala la kuboresha mbuzi wako hata ukichukua crossbreed wa Boer sio vibaya bado matokeo yatakuwa mazuri.

Ila pia ukijitaji pure Boer goat wapo pia. Nadhani una namba yangu unaweza nipigia kwa mawasiliano zaidi..
 
NAOMBA KUJUA KAMA ULIFANIKIWA KUTATUA TATIZO HILO MAANA NINA NG'OMBE WANGU NA AMEPATWA NA TATIZO HILO LA KUTOTOA MAZIWA BAADA YA KUPEWA DEXAMETHASONE.
Vipi ng'ombe wako amerudi katika hali ya kawaida?
 
Mkuu kama uko Dar naomba unielekeze jinsi ya kupata pupy 2 jike na dume wa mbwa aina hii. Mimi nipo tabata kimanga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…