Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mahindi 200 unachoma kwa mkaa wa Tsh 2,000/=?Sasa namuelewa sana JPM !
Jamani mtaani kuna pesa nyingi sana ambayo haina pa kwenda. Inatafuta mwenye uhitaji , ipo nyingi sana.
Ukiwa mbunifu (creative), mjanja na mhangaikaji hukosi pesa , tena nyingi tu. Ukiumiza kichwa ukachapa kazi (bila ubaguzi) unapata pesa tena kiulaini kabisa.
MAHINDI YA KUCHOMA
Hindi moja nimekuwa nikinunua kwa TZS 50 mpaka 100 shambani kulingana na wingi wake.
Nikishalifikisha mjini umbali wa 20 km nikalichoma , naliuza TZS 500 hadi 600.
Nikinunua mahindi 200 nitauza TZS 120, 000.
Matumizi:
Bei ya kununulia ni TZS 20,000 ; Usafiri 3,000 ; nauli yangu 3, 000 ; mkaa TZS 2,000. JUMLA YA MATUMIZI NI TZS 30,000 per day
Faida = 120,000 - 30,000 = 90,000 per day.
Kwa siku 20 = 1,800,000.
Endelea kudai kupandishwa madaraja na nyongeza ya mshahara mpaka Yesu arudi.